Mahakama Yatupa Maombi Ya Kupinga Uteuzi Wa Askofu Mwakihaba

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imetupilia mbali maombi ya kupinga kusimikwa Askofu mpya mteule, Geofrey Mwakihaba na kupinga kuondolewa madarakani kwa Askofu Dk Edward Mwaikali katika mkutano Mkuu wa Dayosisi uliofanyika Machi 22, 2022.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na askofu aliyeondolewa katika Dayosisi ya Konde ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Mwaikali ilianza kuunguruma juzi Jumatano.

Leo Ijumaa Juni 3, 2022 Jaji wa Mahakama hiyo, James Karayemaha ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pande zote kupitia kwa mawakili wao.

Jaji Karayemaha amefafanua kuwa upande wa mleta maombi ukiwakilishwa na wakili William Mashoke amesema ilipokea mapingamizi yote mawili yaliyosikilizwa kwa pamoja.

"Hivyo mleta maombi aliruka vipengele vya maamuzi kwa kutofuata utaratibu kwa kuzingatia Katiba ya KKKT ya mwaka 2015 ila kama hajaridhika na uamuzi wa mahakama anaweza kukataka rufaa," amesema Jaji Karayemaha.

FUVACLbWUAAdv0a.jpg


FUUiTE0XwAAFNMb.jpg

Source: Mwanahalisi
 
Biblia imeweka wazi kwamba wakristo katika mambo ya kikanisa na kiimani wasipelekane mahakamani.

Hawa maaskofu wanatumia biblia ya wapi? Pengine hata sio wakristo.
 
Ata Yesu alipelekwa kwenye mahaka ya kisheria ingawaje alituhumiwa kwa makosa ya kiroho kwahiyo mahama ni chombo pekee cha kufafanua sheria na kutoa mapendekezo sioni walipokosea mwishoni Jaji anasema ambaye hakuridhika anaweza kukata rufaa.
 
Back
Top Bottom