Mahakama yaamuru Mbowe akamatwe

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
*Ni baada ya kushindwa kufika mahakamani
*Anakabiliwa na shitaka la kufanya vurugu


MAHAKAMA ya Wilaya Hai, mkoani Kilimanjaro, imetoa hati ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, baada ya kushindwa kufika mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.

Hati ya kukamatwa kwa Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Denis Mbelembwa, baada ya mbunge huyo kutohudhuria mahakamani hapo bila taarifa yoyote.

Pamoja na kutolewa hati ya kukamatwa Mbowe, pia hakimu huyo alitoa hati ya kumkamata mdhamini wa Mbowe, Awadh Uronu, kwa kile kilichodaiwa kuwa amekiuka masharti ya udhamini.

Hakimu huyo alitoa hati hiyo, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Marwa Mwita, kuiambia Mahakama kuwa, kitendo cha Mbowe kutohudhuria mahakamani hapo amekiuka masharti ya dhamana.

Katika shauri hili, Mbowe anakabiliwa na mashitaka ya kufanya vurugu na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi, siku ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mbowe anadaiwa kufanya vurugu huzo Oktoba 31, katika kituo cha Uchaguzi kiitwacho Lambo.

Inadaiwa kwamba, mshitakiwa huyo alimshambulia msimamizi huyo, Nasri Othmani na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mbowe ameshitakiwa kutokana na kuvunja kifungu namba 240 sura 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Pamoja na kutolewa hati ya kumkamata Mbowe na mdhamini wake, kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa Septemba 18, mwaka huu.

CHANZO: Mtanzania
 
kwani ni lazima afike mbowe mwenyewe mahakani? wakili wake anatosha sana!
 
Kuna mambo siyafahamu, mnaojua nielezeni, hasa kwa kuwa hili ni shauri la muda mrefu (Oktoba 2010-Septemba 2012):
- Mbowe alishitakiwa lini kwa vurugu hizo?
- Hiyo kesi ilikuwa ikiendelea au iliahirishwa hadi sasa?
- Kwa nini imechelewa kusikilizwa/kuamuliwa?
 
Tehe tehe te te teee hii ndiyo serikali ya ccm iliyojaa majuha hata mahakama zinafanya kazi kwa amri na utashi wa viongozi wa serikali ya kifisadi ya ccm
 
Hiyo kesi tangu 2010 hukumu bado? tatizo nini Upelelezi haujakamilika? au wanataka wamuukumu ikikaribia 2015, magamba bana wanamatatizo kweli Kamuhanda yupo kitaa anakula good time wakatia alitakiwa awe amekwisha nyongwa kwa mauaji ya Mwangosi.
 
kesi toka 2010 mpaka leo hukumu bado? ni njama za kumdhoofisha sauti zege mzee wa anga bila sababu za msingi!
ok hakimu umepata umaarufu subiri liwalo na liwe akuhamishe@!
 
hawajapanda sikunying helkopta sasa wanajifanya wamkamate ili wapate nafasi hiyo yakupanda na kulipana viposho.polic bwana.
 
Hayuko juu ya sheria huyo. Akamatwe apelekwe au ajipeleke mwenyewe.
 
Duh, saga lingine limeanza! Mbona ahukumiwi? tangu 2010! Kaazi kweli kweli!
 
Nazani ningekuwa hakimu huu mrundikano wa kesi usingekuwepo!
Ivi mwaka wa tatu sasa mnadeal na kesi za uchaguzi wa 2010 labda ni sifa kwa mahakimu kuwa na utitiri wa kesi
Naona kuna haja ya yankuwa na target interms of minimum no of targets ya kesi ambazo zasubili hukumu bse hii ina encourage rushwa
 
Dah! Kamanda wangu wa anga Mbowe sasa offer nyingine hiyo ya kupanda helcopter ya bure....

Raha hizi jaman.....................!
 
Walikuwa wapi siku zote hii nikupotezeana muda tu kwa vile wanajua tuko kasi m4c, isitoshe wakili wake anatosha kumuakilisha. waache ujuha....
 
Back
Top Bottom