Mahakama yaamuru Mbowe akamatwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yaamuru Mbowe akamatwe

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by EMT, Mar 20, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  WAKATI bado anakabiliwa na kesi ya kufanya maandamano bila kibali mjini Arusha, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameingia matatani kwa mara nyingine, safari hii Mahakama ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imeamuru akamatwe.

  Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, anatakiwa akamatwe kwa madai ya kushindwa kufika mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.

  Hati hiyo ilitolewa Machi 18, baada ya Mbunge huyo kutohudhuria mahakamani hapo, bila taarifa wala mdhamini wake.

  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Denis Mpelembwa, aliagiza kutolewa kwa hati hiyo, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Kassim Mgwambi kutoa maelezo ya kutohudhuria kwa mtuhumiwa mahakamani hapo, bila hivyo kukiuka masharti ya dhamana.

  Mwendesha mashitaka alisema, pamoja na kutoa hati ya kumkamata mshitakiwa huyo, pia alitoa hati ya kumkamata mdhamini wake na kuandikiwa barua ya kuitwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata masharti ya kumdhamini mtuhumiwa huyo.

  Awali ilidaiwa kuwa, Mbowe anakabiliwa na mashitaka ya kufanya vurugu na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi, siku ya uchaguzi mkuu katika kituo cha Lambo Oktoba 31 mwaka jana.

  Inadaiwa mshitakiwa huyo alimshambulia msimamizi huyo, Nasri Othmani na kumsababishia maumivu makali mwilini.

  Mbowe ameshitakiwa kutokana na kuvunja kifungu cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 240 sura ya 16 ya sheria za Tanzania kutokana na kufanya shambulio hilo katika kijiji hicho saa 11 jioni.

  Pamoja na kutolewa hati ya kumkamata mshitakiwa huyo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa Mei 8.

  Kwa sasa, Mbowe na viongozi wengine wakuu wa Chadema, wanakabiliwa na mashitaka ya kuongoza maandamano mjini Arusha yaliyolenga kupinga uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo.

  HabariLeo
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kazi ya kutafuta ukombozi wa kweli sio lelemama! Yatakwisha haya msivunjike moyo hakuna mapinduzi rahisi ikumbukwe kwamba tunapambana na mtu tuliyempa mtaji sisi wenyewe hivyo tunapaswa kutafuta nguvu za ziada ili kuweza kushinda vita hivi.

  Kwa imani na mapokeo tunaamini kwamba hakuna dola iliyodumu milele katika uso wa dunia hii, siku moja nguvu ya umma itachukua mkondo wake.

  TUSIKATE TAMAA, NCHI NI YETU NA MUDA WA KUFUKUZA MAMLUKI NDIO HUU.

  MAPINDUZI DAIMA!!
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kila mtu ana anayo haki yake
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni criminal mind! Ndio maana, sasa nimeelewa.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hii inanikumbusha lugha aliyokuwa anatumia kilaza Topical ..... kama sio wewe na ID mpya
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Umekosa, jaribu tena!
   
 7. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Wanatafuta makubwa
   
 8. c

  carefree JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wamkamate si anajulikana alipo sihasa za tz mwanzo mwisho cdm watafunguliwa vijikesi mpk basi
   
 9. b

  batadume Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  chenga chenga tuuuu hamna lolote na wata kiona na cdm mwaka huuuu......................................................
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Mwenyekiti anapiga watu ngumi je viongozi wengine itakuwaje
   
 11. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  (a) Hapo kwenye RED naona kuna chembe chembe za UDINI.

  (b) Anyway, naomba kuuliza, ivi mbunge ana protection au limitation gani when it comes to arrest?

  (c) MAJI MSHINDO acha statements za kizushi, changanua mambo si kuropoka ovyo!
   
 12. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sioni udini hapo isipokuwa huo unaouleta. Mbunge hayuko juu ya sheria. Kama hakufika mahakamani taratibu zilizochukuliwa na mahakama ni sahihi. Hata hivyo inawezekana alitoa taarifa kwenye chombo kingine cha sheria kuhusu yeye kutokufika ila haikufika ktk mahakama husika siku ya kesi. Ni Mbowe mwenyewe au mwanasheria wake ndio wenye uwezo wa kutoa ufafanuzi. Tuvute subira.
   
 13. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haki haiombwi wewe mtu hafif,tena bora huyo mbowe kawaonea huruma ingekuwa ni mimi hako ka bwana kangekunya siku hiyo!

  Mchakachue matokeo halafu mtegemee watu wawachekee??,..time imefika to bring about a change!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mabadiliko yanatafutwa kwa ugomvi au kufuata taratibu na sheria zilizopo ? acha kuchanganyikiwa kijana
   
 15. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haki haiombwi wewe mtu hafif,tena bora huyo mbowe kawaonea huruma ingekuwa ni mimi hako ka bwana kangekunya siku hiyo!

  Mchakachue matokeo halafu mtegemee watu wawachekee??,..time imefika to bring about a change!
   
 16. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  naona michezo michafu imesha anza, sidhani kama kuna kiongozi CCM anaweza akakamatwa na mahakama, labda akiwa amekorofishana na wenzake
   
 17. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haki haiombwi wewe mtu hafif,tena bora huyo mbowe kawaonea huruma ingekuwa ni mimi hako ka bwana kangekunya siku hiyo!

  Mchakachue matokeo halafu mtegemee watu wawachekee??,..time imefika to bring about a change!
   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Hizi kesi kesi za viongozi wa CHADEMA mi nazipenda kweli maana zinakimarisha CHAMA, maana siku ya kesi sisi tunagawa kadi mpya za wanachama - ha ha ha

  CCM bado wamelala fofofo hata kujibu hoja ya CHADEMA wameshindwa.
   
 19. S

  Songasonga Senior Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kukiuka sheria sio suruhisho la kuleta ukombozi ni bora kuhakikisha mahakama inaheshimiwa
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sheria zipi bana? kuna kufuata sheria kwenye nchi hii? Hata hao wanaojiita watoa haki wao ndio wavunja haki.
  Nambie kesi ya jaji Lugazia ya traffic iko wapi?
   
Loading...