Mahakama yaamuru Lissu afike Mahakamani Desemba 19

Kama mtu huwezi kwenda na mapigo ya muziki unaotumbuiza kwa wakati huo ni bora tu uwe mpenzi mtazamaji maana kinyume chake utaonekana kituko mbele ya wacheza muziki wenzako na kwa wapenzi watamazaji. Unakata tawi la mti huku ukiwa umekaa juu yake! So weird!
 
Mh Hakimu anasema hataki siasa: "Hatutaki mambo ya siasa hapa namtaka Lissu aje hapa mahakamani kesi yake iendelee".

Ndugai: Sijui Lissu alipo, namvua ubunge
Rais: Ametelekeza jimbo
Hakimu: Sitaki siasa, aje kesi iendelee

====


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imemwagiza mdhamini Ibrahim Ahmed wa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi kumtaka afike mahakamani Desemba 19, mwaka huu kusikiliza kesi yake.

Mahakama hiyo imesema kwa kuwa mdhamini ameieleza mahakama kwamba Lissu amepona, afike mahakamani siku iliyotajwa ili kesi iweze kuendelea.

Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kumhoji mdhamini.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ya hakimu na mdhamini:

Hakimu: Mdhamini wa mshtakiwa, Lissu yuko wapi?

Mdhamini: Mheshimiwa hakimu Lissu amepona, lakini amekataa kuja kwa sababu anahofia usalama wake.

Hakimu: Hatutaki mambo ya siasa hapa namtaka Lissu aje hapa mahakamani kesi yake iendelee.

Alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 19, mwaka na Lissu anatakiwa afike mahakamani siku hiyo.

Mapema mahakama hiyo iliagiza wadhamini wa Lissu kupeleka taarifa jana kuhusu mshtakiwa huyo.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni, wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, 'Machafuko yaja Zanzibar.'

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13, 2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Chanzo: IPP Media
Hii ni moja ya amri mfu,isiyotekelezeka! Tujiulize,asipokuja siku hiyo itakuwaje? Yetu macho.
 
Hizi mahakama za kitumiwa na Jiwe hizi'
Haki ya Mungu niliumia sana siku nasikia redioni
Maagizo ya huyo hakimu khs Lisu.
Basi tu.
Mungu amlaani pmj n hao wanaozitumiA.
Hovyo sana.
 
Ni wazi kuwa mahakama haitambui tukio la Lissu kupigwa risasi inaona ni siasa tu zisizo na madhara kwa Lissu! Hebu tuangalie jaji aliyesema kwani ni uhai wa nani (who's life is it anyway) hukumu hii ilitolewa kwa mtu aliyekuwa akiishi kwamateso ya jeraha la ajali na akaamua kufungua kesi ili hosipitali iondoe vifaa vinavyomsaidia aishi, jaji alimpa ushindi mgonjwa aliyetaka afe kwa kusema who's life is it anyway, atakayekufa ni wewe ushauri yako. Hapa mahakama haijali usalama wa Lissu kwani haikutaka kuwauliza polisi kuhusu uchunguzi na upelelezi wa jaribio lile na kama akija itamlindaje kama raia wengine.
 
Tanzania si salama tena kama zaman, lisu abaki huko mpaka upepo ukae vizur, na sidhani kama atakanyaga huku kwa mda huu.
 
Mtu kuhofia usalama wake ni siasa? Huyo hakima ajiandae kupokea tamko rasmi kutoka kwa Tundu Lissu linaloelezea kutokuwa tayari kufika mahakamani kwa sababu za kiusalama.
Pia mkumbusheni huyo Hakimu kwamba anaposema hiyo kesi itatajwa tena tarehe 15 December, 2019 asisahau kuwa huwa kuna likizo ya mahakama
Mahakama imekuwa kama gari lisilo na dereva, breki, wala mwelekeo linapuyanga tu!
 
Back
Top Bottom