Mahakama ya Rufaa yamrejeshea ubunge Aesh Hilal wa CCM

Kwahiyo mahakama ya rufaa imejiridhisha kwamba aeshi hilary na ccm yake hawakumwaga rushwa huko sumbawanga kama ilivyobainika au ndio imeamua kutekeleza maelekezo ya ccm na mwanasheria mkuu wa ccm Werema kwamba chaguzi ndogo zinawagharimu sana?

Je kwa hali hii kuna matarajio yoyote ya haki kutendeka katika rufaa ya Peter Kafumu wa Igunga? kama hali yenyewe ndio hii ya watu kutumia rushwa za waziwazi lakini mahakama inaamua kuwarudisha katika uongozi wa sababu tu ya kuepuka gharama? Demokrasia ni gharama kubwa sana ni lazima tukubaliane hilo kwani vinginevyo watu watakuwa wanafanya juhudi za kumwaga rushwa na kuchakachua matokeo ili watangazwe washindi them amahaka ije ituambie kuwa kurudia uchaguzi ni gharama kubwa.
 
Mahakama ya Rufaa imemrejeshea ubunge mbunge wa Sumbawanga Aesh Hilal leo.

Awali mahakama kuu ilikuwa imemvua ubunge lakini akakata Rufaa.

Mwaka jana Mahakama kuu ilikuwa imekubaliana na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Mwl Norbert Yamsebo aliyekuwa amefungua kesi kupinga ushindi wa Hilal.Mojawapo ya mambo yaliyokuwa yamethibitishwa na mahakama kuu mwaka jana ni matumizi makubwa ya Rushwa.

rushwa ni rushwa tu. Hakuna rushwa KUBWA wala Ndogo.
 
Lakini kwa nini Watanzania tunakua na double standards? Mahakama ya rufaa ilivyo rejesha ubunge wa Lema ilipongezwa leo hii kwa vile imerudisha ubunge wa mbunge wa CCM inasemwa vibaya.
Unachotaka kukisema sio kweli kabisa. Hukumu ya Lema iko wazi kabisa hata kwa mtu anayeanza kujifunza sheria leo. Ni ubishi tu wa wanaCCM wachache ndio hawataki kuonyesha kukubali.Kwa vyovyote vile Lema angerudishiwa ubunge wake, Kwanini? CCM haikuwa tayari kwenda kwenye marudio ya uchaguzi wa Arusha mjini.

Watu wengi humu ni waelewa na wanaweza kupima mambo mbalimbali, ikiwemo ya Kisheria.
Suala la Uchaguzi wa Sumbawanga kila mtu alikuwa anajua CCM mwaka 2010 walicheza faulo nyingi sana ili kupora ushindi.
Na hayo yalidhihirika pia mahakama kuu na mahakama ya rufaa pia ambao Aish alivuliwa ubunge.
Sasa hili la hukumu ya marudio(Review) ya Mahakama ya rufaa la leo, kwa wengi linatia mashaka sana, ndio maana watu wengi wanashtuka.

Kifupi mwenendo wa CCM katika kuchakachua haki za wanyonge katika kila eneo(mahakama zikiwemo) ndio linalotia mashaka kila mpenda haki kuhusu hukumu hii kama kweli Haki ametendeka na je Haki alionekana ikitendeka?
 
Nakubaliana na hukumu ya mahakama hata kama naamini kuwa haikutenda haki,tuna la kujifunza hapa na kujipanga upya mwaka 2015.
 
CDM imeangukia pua, hivyo CCM inaendelea kushika ubunge wa jimbo husika, baada ya mahakama ya rufaa TZ kutengeua maamuzi ya Mahakama Kuu
 
Wameamua kuiweka mizani balance.
Nchi hii hakuna haki kabisa!
Hii biashara ya uteuzi wa majaji unaofanywa na mwenyekiti wa chama cha siasa unafikia ukingoni.
Tunataka free judicial commission!!!

Hapo ndio huwa najiuliza kuhusu uwezo wa wapenzi wa Chadema, mnataka kujitoa kwenye mchakato hapo hapo mnatamani na kutaraji mabadiliko kwenye katiba..??? hivi nyie mnashikiwa akili zenu na viongozi wenu?
 
Unachotaka kukisema sio kweli kabisa. Hukumu ya Lema iko wazi kabisa hata kwa mtu anayeanza kujifunza sheria leo. Ni ubishi tu wa wanaCCM wachache ndio hawataki kuonyesha kukubali.Kwa vyovyote vile Lema angerudishiwa ubunge wake, Kwanini? CCM haikuwa tayari kwenda kwenye marudio ya uchaguzi wa Arusha mjini.

Watu wengi humu ni waelewa na wanaweza kupima mambo mbalimbali, ikiwemo ya Kisheria.
Suala la Uchaguzi wa Sumbawanga kila mtu alikuwa anajua CCM mwaka 2010 walicheza faulo nyingi sana ili kupora ushindi.
Na hayo yalidhihirika pia mahakama kuu na mahakama ya rufaa pia ambao Aish alivuliwa ubunge.
Sasa hili la hukumu ya marudio(Review) ya Mahakama ya rufaa la leo, kwa wengi linatia mashaka sana, ndio maana watu wengi wanashtuka.

Kifupi mwenendo wa CCM katika kuchakachua haki za wanyonge katika kila eneo(mahakama zikiwemo) ndio linalotia mashaka kila mpenda haki kuhusu hukumu hii kama kweli Haki ametendeka na je Haki alionekana ikitendeka?

Mkuu wangu Kwa hiyo mkuu unacho sema ni kwamba hukumu ya Lema ilikua wazi kabisa lakini hii ya Hilal haikua wazi? According to who? You? Au mwenzangu una access na ushahidi ulio tolewa mahakamani unao taka kushare na sisi mkuu?
 
i expect something like this before. hakuna haki hapa.

Tusiwe double standard kwa vile CCM imeshinda haki haijatendeka ila ingeshinda CDM haki ingeonekana imetendeka hii siyo sawa hv kwanini uko hivyo huu ni upuuzi yani unakipenda chama kushinda chochote araaaa!!
 
Back
Top Bottom