zimwimtu
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 1,988
- 1,095
wordHahaha kwa lugha nyepesi ni kwamba wamekosa ushahidi au kama wameupata basi kuna chain ya vigogo ambao wao na familia zao hawatakiwi kuguswa.
wordHahaha kwa lugha nyepesi ni kwamba wamekosa ushahidi au kama wameupata basi kuna chain ya vigogo ambao wao na familia zao hawatakiwi kuguswa.
Nyumba sabini sii zakwake alijenga na mshahara wake,kwani alishikiliwa kwa ajili ya nyumba? Mtu kafanya kazi tangu miaka ya themanini atashindwaje kujenga nyumba sabini nyumba zenyewe nje ya mji Kiwanja hela kumi alinunu kwa milioni tano?mchanga lory huko 30,000?Sijawahi kuwaamini hawa mapopoma wa sheria wa serikali hii! unawaachiaje watu mlituaminisha wana nyumba sabini na ngapi sijui
Tangu lini salary slip akawa Lumumba.salary slip ni wewe umeandika hapa au account yako imehakiwa mkuu, kama sikosei wewe jingalao, simiyuyetu, lizaboni, mudawote ni wale wale wa lumumba sasa nashangaa leo umetoa hii kitu, nimebaki nimeganda aisee, ni wewe au macho yangu
Lumumba mwenzio hajawahi kushinda case hata ya samaki aliangukia pua,zote zitaishia hewani mana wezi ni nyie wenyeweAtakua kajifunza kama Lema
Toa avatar ya putin weka ya lusindeAtakua kajifunza kama Lema
Kumbe nchi hii ukiipiga Serikali pesa ndefu wala hawana shida na wewe, ole wako uibe vihela vidogo vidogo vya mboga mbona utakiona cha mtema kuniAtakua kajifunza kama Lema
Kuna uwezekano mkubwa Kwa hao walioachiwa kuwa wametoa ushirikiano Kwa serikali Kwa kukubali mali zao kuwa mali Za serikali Na kwenye Kesi ya msingi wao watakuwa mashahidi, Na wafanyabiashara husika kutakiwa kulipa hizo kodi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.
Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA) kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.
Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.
Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya (51).
Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.
Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.
Chanzo: Michuzi Blog
Unahisi?? Mbona mlitaka front page, mkasema wana nyumba sabini, semeni mmezitaifisha ili mpate tena front pageNadhani serikali imeshachukua chake kutoka kwao kwa kuwafilisi mali walizokuwa wanamiliki,kwahiyo "nahisi" wanarudi uraiani kuanza moja,Magufuli hawezi kuwaachia watu waliokula mabilioni ya pesa kiurahisi hivo.
Nani kasema imekurupuka?Serikali iache kukurupuka na kufungulia watu kesi za mwendokasi zisizo na kichwa wala miguu.
huwezi kushitaki mtu kwa kutumia Font fage za magazetini ama mitandaoni,kuna uwezekano mkubwa hii kesi ikawa drafted upya ili kuipa uwezo wa kisheria mahakama ya mafisadi kuwafunga hakina masamaki.
DPP ameona loopholes zilizopo kwenye sheria za mahakama za kawaida kabla ya kuundwa kwa mahakama ya mafisadi. So ameamua aondoe kesi huku ili ashitakiwa kwenye mahakama ya mafisadi. If this is true then it is a good move.