Mahakama ya Kadhi ni nini?

Mahakama ya Kadhi ni nini?

Hakuna haja ya kutowa povu kama hamjuwi nini toka siku hizo inazungumziwa nendeni zanzibar mukaione inafanya nini kama watanzania wenzenu hamuwaamini mbona hata Kenya ipo ..kama vile viongozi wanapokwenda nchi mbalimbali kujifunza mambo wafunge safari kwenda Kenya ili waje kuwaelezea wananchi wao walichojifunza
 
Mahakama ya kadhi ni mahakama inayoshughulikia masuala ya wale wenye imani ya Kiislamu. Tanzania haijawanyima Waislamu kuwa na hiyo mahakama ila waiendeshe wenyewe.pasipo kuishusisha serikali. Waisalmu wanataka kadhi atambuliwe na kulipwa Serikali huku wakijua dini ni hiari ya mtu. Itakuwaje na imani nyingine zikadai nazo viongozi wa sheria kwenye imani zao nao watambiliwe na Serikali? Hili ni jambo lisolowezekana ingawa Mrema ndo mchochezi wa jambo hili akitafuta kura za Waslamu. Kwa kuwa Mungu hadhihakiwi angalia Mrema alikofikia kisiasa. Yote haya ni kutokana na ulaghai wake. Shame on him.

Umemtaja mrema, OK. Vipikuhusu waziri mkuu kutoa ahadi ya kuwasilisha huu muswada wa mahakama ya kadhi. Nadhani hakufikiri vizuri kuingiza jambokama hili lakiimani katika bunge la nchi ambayo katiba haijishughulishi na mambo ya dini za wananchi. Where did he get this, and what the reason behind.
 
Kwani wakiristo walikatazwa kuomba mahakama yao ya kichungaji au kiaskofu?
Kwa maana nyingine ni kama sheria zilizopo hasa za ndoa na mirathi haziwakwazi hivyo sio mbaya tukiziita ni mahakama za kikiristo tena ukizingatia tulizirisi toka wakristo waingereza ambao wao kipindi hicho waliruhusu mahakama ya kadhi ikaja futwa MWENYE HERI MTARAJIWA

Anzisheni hatakesho kwa gharama zenu, that's all.
 
Na hospital za kannisa madaktari wanalipwa na serikal.

Wale ni madaktari wa serikali na ndio maana wanalipwa na serikali.Serikali ndio inasaidiwa na makanisa kwa hospitali kwa maana yenyewe ni lofa kazi kuiba tu.
 
Mahakama za kadhi ni mbinu ya kuingiza utawalal wa sharia Tanzania kama wanavyopigania boko haram huko Nigeria, tafadhali kataa kitu hiki kwa nguvu zote!
 
Hodi wakuu. Nmevutiwa na mjadala lakn pia nmesikitishwa na jazba za wanajamvi! Hatuend ivyo hata kidogo, hebu tujadili juu ya uhalisia wa jambo hili ili kila mmoja aweze kuwa criticzed. Mfano: una watoto sita, mtoto mmoja akaomba apewe chake mapema asepe, so akapewa sasa tujadili hapa ni nn kitatokea kwa waliobaki? Je umoja wa familia utakuwaje? Je wazaz watakuwa na hali gan? Je unafikiri wale waliobaki wanaweza kunyamanza kimya bila kudai vyao na wao? Kwa upande wa pili ni lazima tujue kuwa hii mahakama itajitegemea au itategemea serikali? Na je kuna taasisi nyngne ya kidn ambayo inategemea serikali? Lakn pia tusisahau haya; kuna Waislam walio oa au kuolewa na wakristo na wanaish pamoja nahuenda wana watoto sasa hawa watasimama ktk mahakama ipi? Kuna watakao amua kukimbilia ukristo kwa ama kibur cha kuogopa sheria ya dini baada ya kuwajbishwa, je hawa watapelekwa wap. Hili suala n kama kuwa na uraia wa nch mbili ambalo bad n changamoto. Let's us reason together.
 
WAISLAM WENGI TU WA MADHEHEBU MENGINE WANAPINGA MAHAKAMA YA KADHI

KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.

1. Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.

2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.

3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.

4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?

5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.

6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.

8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.

KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.

10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.

11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.

12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!

WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.

14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:

(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.

(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!

16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.

WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.

Duh kweli hii mahakama majanga
 
Majanga hii mahakama
 
Hivi Lyatonga Mrema alipokuwa anaishabikia alikuwa anajua maana yake au alitaka kuwarubuni waislamu? Na huyu.AG mpya anaposema mahakama ya kadhi haina madhara kwa katiba anajua amachozunguma au naye anataka kuwarubuni hao wanaoidai? Naona kwenye nchi kama Tanganyika siyo sahihi kudai mahakama ya kadhi. Hivi serikali ilipowapa waislamu.chuo cha Morogoro Wakristo walipewa nini?
 
Tafsiri nzuri ya KADHI itafute vizuri ktk bibilia ipo .Kadhi ni Mwamuzi au Mshauri ktk MASHAURI yenu iwe kufungisha Ndoa ama Talaka kwa kosa linalopasa na sio kuonja Bint wa mtu kisha utowe Talaka utakavyo.Miradhi kwa waridhi bila kudhulumiana.Kutoa Haki kwa anayedhulumia nk.
achana na Biblia bro!; qaraa inasema kila ummati tumewajaalia kawaida yao ya Ibada na Sheria zao! Biblia nayo Mungu anasema Ataweka Agano Jipya si kama lile la zamani, ambalo babu zenu walishindwa kutekeleza! Tukirudi kwenye Mahakama ya qadi, waislamu wanadai misingi na rejea ya hukumu zake ni allah! hapo hakuna pungufu, kwamba eti mirathi, ndoa.. Tusidanganyane!; hiyo si mahakama ya qadi, ni heri waseme wanataka waanzishe ngo! Sababu qadi pia haina ziada ni hukmu za allah tu!; la sivyo wanaotaka qadi watupe ushahidi wa ayat kwamba; mahakama ya qadi ni ndoa, talaka, wakfu na mirathi! Halafu hizo Sheria za allah hata muhammad alishindwa kuzi-tekeleza!; muhammad aliibiwa ngamia wake, na akaamrisha wezi wasakwe, na walipokamatwa!; kwa mujibu wa sharia ya allah wakatwe mkono! Lakini muhammad aliwakata miguu, na mikono yote na kuwang'oa macho.Abu dawud.38:4350! Hofu; allah anasema amewapa kigezo chema waislamu naye ni muhammad! Jee akitokea qadi katoa hukumu, kama aliyoitoa muhammad kwa kisingizio anamgeza muhammad, ana kosa?...Mbona waislamu wanaelekezwa na allah kwamba wakihitilafiana warejee kwenye qaraa, hadith, na miratul rasul!
 
Kadhi Court is a Satanic institution governed by Satanic verses.

1. There is no valid basis whatsoever for the inclusion of the Kadhis' Courts in the Constitution;
2. If Muslims alone get preferential treatment for setting religious Courts, then other communities and faiths would come forward to have separate courts
3. Provision such as Kadhis' Courts is normally covered under the general law. It should not be part of the main body of the Constitution,

Islamic "Kadhi" courts is illegal and discriminatory. The Kadhi court system will elevates Islam over the country's other religions, and should be deemed unconstitutional because it does not coincide with Tanzania's secular mandate and should not be included in the nation's new constitution.
 
mou mou si mjenge horpitali na shule nanyi mpewe mou yenu!

mkuu mgen,hawa watu hawawezi kuelewa kamwe,hata uwaeleweshe vipi.
kuna kipindi mwaka jana nilikuwa nina semina pale Edema,jirani kabisa na chuo chao cha kiislamu,nikashangaa kuwasikia wasomi wao eti wanasema nchi hii inaendeshwa kwa mfumo kristo ndio maana hata wimbo wa taifa kuna maneno ya Kikristo kama "Mungu Ibariki".
Sasa kama hao ndio vichwa,je hao walioishia kwenye elim akhera itakuwaje?
 
Back
Top Bottom