Mahakama ya kadhi kuanza hivi karibuni

Mahakama ya kadhi kuanza hivi karibuni

Bakwata wanayo haki ya msingi ya kuanzisha hiyo mahakama
 
Kwani hiyo mahakama si ya waislam? Sasa sisi wakristo inatuhusu nini? Kama vp na sisi tudai yetu tukinyimwa ndio tulalamike..

Hakuna hukumu kwenye ukristo ni mwendo wa kusamehe saba x 70, mwenzako akikutandika shavu la kulia unamgezia na la kushoto ukutandike tena. Kazi kweli kweli.
 
Mbona serikali inachangia kanisa kupitia MOU, sasa kwanini serikali hiyo hiyo asichangie kwenye Mahakama ya kadhi kwa ajili ya waislam. Lazima kieleweke.:rockon:
Waisilamu fungukeni akili, MoU sio taasisi, hata waisilamu wanaweza kusaini MoU na pengine zilishasainiwa na waisilamu wajanja wenye macho ya makengeza yanayoangalia fursa. Tatizo waisilamu wa kwa Mnyamani na Tandika wamekaririshwa waone kama vile MoU ni taasisi ya Kikristu, kumbe kuna wenzao wajanja wanaendelea kufaidika na fursa. Huwezi kulinganisha MoU ambayo ipo kwa wote na Mahakama ya Kadhi ambayo ipo kwa ajili ya waisilamu tu
 
Sasa wale Makadhi wa mikoa waliochaguliwa siku zote hizo walikuwa wanafanya kazi zipi? Mimi nilidhani imeshaanzishwa, ila wanachopigania waisilamu ni kwamba walipwe mishahara na serikali kupitia kichochoro cha sheria ya kadhi!
 
Hapo ndio kuna tofauti kubwa. Kwenye MoU serikali inachangia huduma ambazo kila mtanzania anaweza kupata. Mfano hospital ya KCMC - yeyote anaweza kutibiwa pale. Mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu tu. Anzisheni then muombe MoU, Kikwete alisema milango iko wazi.

Usitulazimishe, kila mtu anakipaumbele chake, nyinyi kipaumbele chenu ni kustarehe kwenye hii dunia( kujilimbikizia mali, kujenga majumba makubwa, kujenga mahospitali na kulangua watu), waislamu kipaumbele chao ni kukamilisha ibada zao ili waweze kupata salama baada ya maisha ya duniani (kaburini + akhera), alafu baada ya hayo mambo mengine yanafuata. Hivyo, kwasasa tunataka mahakama kadhi kama sehemu ya ibada.
 
Kwa wakatoliki kuna Marriage Tribunals, ni mahakama za ndoa ambazo zinaendeshwa na wakatoliki wenyewe. Majaji ni wakatoliki wenyewe na hata notaries na watetezi ni wakatoliki wenyewe. Je leo ni haki kwa wakatoliki wadai mahakama hizo zitambuliwe na serikali, zigharamiwe na serikali. Ni mahakama ya ndoa za kikatoliki, zenye maamuzi yanayotambuliwa na wakatoliki, ziko katika domain ya kikatoliki. Wanaodai mahakama ya kadhi wafuate mfano huo, hakutakuwa na shida.
 
Hatufanyi mambo kuiga wakatoliki, ndio maana hatuna wanasesere misikitini.
Tunajua tunacho kitaka. Mlitusumbua sana pepo la kuchinja lilipo wapanda.
 
Kwanini watu wanapenda kujifanya
Kichwa ngumu kwa mambo yaliyo openly that's not lawful kuanzisha mahakama ya kidini na kuhudumiwa na serikali.
 
Hapo ndio kuna tofauti kubwa. Kwenye MoU serikali inachangia huduma ambazo kila mtanzania anaweza kupata. Mfano hospital ya KCMC - yeyote anaweza kutibiwa pale. Mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu tu. Anzisheni then muombe MoU, Kikwete alisema milango iko wazi.

Wezi tu nyie
 
Kwanini watu wanapenda kujifanya
Kichwa ngumu kwa mambo yaliyo openly that's not lawful kuanzisha mahakama ya kidini na kuhudumiwa na serikali.

Serikali ya Kenya na Msumbiji zinahudumia, hii ya Tanzania anashindwa nini! ?
 
Kwani hiyo mahakama si ya waislam? Sasa sisi wakristo inatuhusu nini? Kama vp na sisi tudai yetu tukinyimwa ndio tulalamike..

Wakristo inawahusu........................................Soma Mathayo 5:25 inamtambua Kadhi na Mahakama ya kadhi....
 
Serikali ya Kenya na Msumbiji zinahudumia, hii ya Tanzania anashindwa nini! ?
Kama upo karibu na Msumbiji, nenda ukapate huduma huko. Vivyo hivyo kama upo Kenya.

Karibuni ACT - Chama cha Mabadiliko na Uwazi
 
Hakuna hukumu kwenye ukristo ni mwendo wa kusamehe saba x 70, mwenzako akikutandika shavu la kulia unamgezia na la kushoto ukutandike tena. Kazi kweli kweli.

Ndio maana huwezi kusikia Magaidi wa Kikristo au Wakristo wenye Siasa Kali.Wakristo wanaheshimu sana kanuni ya Mpende mwezako kama nafsi yako.
 
Kuna tetesi kwamba licha ya upinzani wa makundi mbalimbali ya kijamii kuhusu uanzishwaji wa mahakama ya kadhi, mahakama hiyo itaanzishwa hivi karibuni. hii ni kutokana na ukweli kwamba sababu zilizotolewa za kuipinga hazikuwa ni za msingi na wapingaji hawana mamlaka ya kisheria kufanya hivyo. Chanzo ofisi ya Bakwata Makao makuu.

kwa hiyo ninyi mna mamlaka kuliko hao wanaopinga????.
 
Back
Top Bottom