MAHAKAMA ya hakimu mkazi ya SONGEA yamtia hatiani mwandishi wa habari kwa kosa la RUSHWA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAHAKAMA ya hakimu mkazi ya SONGEA yamtia hatiani mwandishi wa habari kwa kosa la RUSHWA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by moma2k, Jun 18, 2012.

 1. m

  moma2k JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Tarehe 14 June,2012 Mahakama ya hakimu mkazi ya mjini Songea mkoni Ruvuma ilimtia hatiani mwandishi wa habari wa kujitegemea KWIRINUS MAPUNDA kwa kosa la RUSHWA(corruption), ambaye amekuwa akiandikia habari zake katika gazeti la Mwananchi. Baada ya kumtia hatiani(convict) mahakama hiyo ilimpa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela au fine ya Tsh.Milioni moja. PCCB(TAKUKURU)-SONGEA(RUVUMA)ndio waliokuwa wakiiendesha kesi hiyo.
   
 2. h

  hoyce JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Alikula rushwa ya nani, ili afanye nini? Atajiju, huyo hana lake tena, maana Mwananchi Songea huwatumia waandishi wa kujitegemea. Na kwa songea huyo nje ya kambi ya Nchimbi.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Waandishi wengi wa habari (siyo wote) ndivyo walivyo!! Na siyo waandishi wahabari tu, rushwa nchini ni janga likiwa na mizizi yake ndani ya chama tawala!!
   
 4. m

  moma2k JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Alikuwa akiandika habari mbaya dhidi ya taasisi mojawapo, bila kwenda kupata taarifa sahihi kwa uongozi wa taasisi hiyo.
  Hivyo alikuwa anaandika habari za uwongo, uzushi na uchochezi dhidi ya taasisi hiyo ili kuitisha(Habari hizo za uwongo na uzushi alikuwa akiandikia katika gazeti la MWANANCHI). Uongozi wa taasisi hiyo ulikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote(no reaction).Baadaye yeye mwenyewe mwandishi wa habari hizo (aliyetiwa hatiani kwa kosa la rushwa) akaenda kuuona uongozi huo na kuomba aandike habari ya kuisafisha taasisi hiyo, akidai alipwe Tsh.milioni 2.5 cash kwa kazi hiyo. Alitoa sharti jingine kuwa malipo hayo yafanyike kwa SIRI KUBWA. Uongozi wa taasisi hiyo ukachukua hatua ya kwenda kuwataarifu PCCB(TAKUKURU). Siku iliyofuata PCCB(TAKUKURU) baada ya kutega mtego wao, walifanikiwa kumkamata akiwa anapokea fedha za PCCB(TAKUKURU) ktk eneo la taasisi hiyo. Ndo ukiwa mwisho wake.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  amevuna alichopanda!
   
 6. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  "PCCB(TAKUKURU)-SONGEA(RUVUMA)ndio waliokuwa wakiiendesha kesi hiyo."

  PCCB tangu lini wanaendesha kesi jamani!?
   
 7. T

  Tyegelo Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PCCB si tu kwamba wanayo mamlaka ya kupeleleza, bali pia wanayo mamlaka ya kuendesha kesi. wana waendesha mashtaka wao.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Hii pia ni habari mbaya kwa tasnia ya habari!.

  Hiyo inaitwa black mail!. Mwandishi anatunga au anaandika habari mbaya za mtu au taasisi fulani, wengine huionyesha habari hiyo kabla ya kutoka ili kuicompromise kwa rushwa ili isitoke na akigomewa ndipo anailipua!. Au wengine kuanza na ulipuaji kisha kujidai kutaka kusafisha na kudai chochote!.

  Hakuna any justification kwa vitendo hivi vya aibu kwa waandishi wetu. Ila pia lazima nikiri kuwa huu ni ukosefu wa maadili!.

  Mbona waandishi waadilifu tupo, sio tuu hatuombi rushwa bali hata kukataa zile free bies za sources!.

  Uandishi ni kazi ya wito, kwa sasa fani imevamiwa!. Waandishi wenye wito tupo tukiitumikia fani kwa uadilifu mkubwa huku tukidumu pamoja na umasikini wake huku wavamizi wakizidi kuongezeka kila kukicha na kuitia doa fani yetu!.

  NB. Angalizo: Msije kuchanganya mambo. Zile little brown envelopes ambazo huitwa "lunch" au " transport" zile ni haki stahili na sio rushwa!. Hizi mimi huwa nasimamia kuhakikisha waandishi wanapatiwa!.
   
 9. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Kifungo miaka 3 au fine million moja? Duu hapa mahakama...., kosa la kupokea rushwa lina fine kumbe? Mi nilikuwa cjui. Duu anabahati sana
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yani mtu mla rushwa anapewa fine ya 1million shs, hii si change tu kwake..
   
 11. m

  moma2k JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Webondo ni mbumbu wa sheria. PCCB wana mamlaka ya kupeleleza na kuiendesha kesi iliyo chini ya jurisdiction yao kwa mujibu wa sheria inayoiweka taasisi hii.
   
 12. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mla rushwa anapigwa faini!
  Kesi hii inafanana sana na ya Jerry Muro. Kumbe hata yy angepata mwanya wa kuchomokea mlango wa faini!
  Tofauti ni kuwa faini yake ingekuwa ndefu
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  ya mbunge vipi?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu hakuwa 'mwandishi' bali 'magumashi'
   
 15. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Alah.... kumbe!!!
   
 16. H

  Hute JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  waandishi wa habari wasiokula rushwa ni wachache sana. nafikiri huyu aliyetiwa hatiani ni mfano mzuri, Jerry muro naye ameonyesha picha halisi ya waandishi wahabari wa tanzania na africa kwa ujumla.
   
 17. H

  Hute JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  ni kweli wanaendesha mashitaka, lakini lazima wapate consent ya dpp, hakuna sheria inayowapa moja kwa moja mamlaka wao kupeleleza kukamata na kushitaki, wao wanapeleleza, wanakamata alafu wanapeleka maombi kwa dpp yanayoambatana na jalada husika kuomba waendeshe shitaka. ukienda pale kwa dpp, majalada yaliyo mengi ni ya kwao...cha ajabu ni kwamba, ni wabovu mno wa prosecution, hata huyo mwandishi wa habari aliyekuwa convicted, ni bahati tu....skills zao za prosecution na uzoefu wao wa kazi ni mdogo sana....kesi zilizo nyingi wanashindwa, na hawataki kuonekana hawajui...hawashauriki hawa jamaa. PCCB pia ni wala rushwa wakubwa mno...
   
 18. blackberry m

  blackberry m JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 542
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 80
  Wacha apate kile alichokitaka
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wale wanaohongwa vyeo vya kisiasa kama tuzo kwa kuwaandikia watu habari za kilaghai unawasemaje Bwana Pasco?
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huo kwenye alama nyekundu ni ushahidi usiosemwa na wengi!
   
Loading...