Mahakama na Misuse of Power: Uhalisia wa Kuvunjwa kwa Haki za Kikatiba kwa Kesi ya Tundu Lissu

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
519
Reaction score
1,463
Ni dhahiri kuwa mahakama ya Tanzania imeteleza vibaya kwenye kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu. Hii siyo tena kesi ya kawaida, bali ni landmark case ya kuonesha ni kwa namna gani mhimili wa mahakama umegeuzwa kuwa chombo cha kisiasa na si tena kimbilio la wanyonge. Juzi, wakati kesi ya Lissu ikisikilizwa, hakimu alitoa kauli ya kushangaza akisema kwamba “Mahakama haiwezi kusikiliza hoja zinazotolewa na upande wa utetezi kwa kuwa hazina mashiko katika mazingira ya sasa ya usalama wa taifa.” Hii statement ya kihuni ni ushahidi tosha kuwa hakuna uhuru wa kimahakama. Kauli hii haikutokana na tafsiri yoyote ya kisheria bali ni direct orders from above, jambo linaloashiria wazi kuwa mahakama haijajisimamia bali imetekwa na watawala.

Tundu Lissu si mtu wa mtaani, ni mwanasheria nguli, aliye na track record ya kutetea haki na sheria. Amepeleka evidence ya kutosha mbele ya mahakama kuonesha kuwa kesi ya uhaini inayomkabili ni ya kubambikizwa na haina msingi wowote wa kisheria. Lakini bado mahakama ikaamua kuahirisha kesi hiyo kienyeji tu—hakuna legal grounds, hakuna maelezo ya msingi. Yaani wanasema case adjourned, no explanation, no nothing. Huu ni uchafuzi mkubwa wa sura ya mhimili wa haki.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 13(6)(a) inasema wazi kuwa kila mtu ana haki ya kusikilizwa mbele ya mahakama huru na isiyopendelea. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) sura ya 20, kifungu cha 194(1), upande wa mashtaka unapaswa kutoa vielelezo vyote kwa wakati ili upande wa utetezi uweze kujitetea kikamilifu. Tundu Lissu alifanya hivyo, lakini bado mahakama ikakataa kumsikiliza. That’s gangster level injustice.

Jamuhuri imeshindwa kutekeleza wajibu wake kisheria. Kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16, kifungu cha 94(1), kutoa mashtaka ya uongo ni kosa la jinai. Vilevile, Ibara ya 30(3) ya Katiba inasema kuwa mtu ana haki ya kwenda mahakamani kupinga vitendo vyovyote vinavyomnyima uhuru wake kinyume cha sheria. Hii inamaanisha kuwa Tundu Lissu anaweza kuwashtaki watu waliomfungulia kesi ya uhaini kwa makusudi, kwa kutumia sheria hiyo pamoja na Sheria ya Usalama wa Raia (National Security Act) ambayo inapaswa kutumika kwa haki, si kwa hila na chuki.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, mkataba wa ICCPR (International Covenant on Civil and Political Rights) ambao Tanzania imeridhia, Ibara ya 9(1) inampa kila mtu haki ya kuwa huru dhidi ya kukamatwa kiholela. Lissu alikamatwa na kushitakiwa bila misingi, jambo linaloonesha kuwa Jamhuri messed up, big time.

Na sasa, tukirudi kwa upande wa mahakama, kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama za Tanzania, kifungu cha 3(1) cha The Magistrates’ Courts Act, mahakama inatakiwa kufuata taratibu sahihi za kimahakama na kutoa hukumu kwa kuzingatia ushahidi. Pale ambapo mahakama inashindwa kufanya hivyo, inaweza kushtakiwa kwa kupitia Judicial Review chini ya kifungu cha 17 cha Sheria ya Mahakama Kuu (The High Court Rules).

Tumechoka kuona mihimili inayopaswa kulinda haki ikigeuka kuwa mashine za kubeba ajenda za kisiasa. Kama Tundu Lissu atashinda hii kesi (which is highly likely), upande wa Jamhuri unakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kushtakiwa kwa malicious prosecution. Hii ni kesi ya wazi ambayo inaweza kuvuta hisia za kitaifa na kimataifa—na trust me, huu ni wakati wa kusema “enough is enough.”

Hatutafumbia macho dhuluma, uhuni na utapeli wa kisheria. We’re watching, we’re documenting, and we’re coming for justice with receipts. Hii sio tu kesi ya Lissu, ni kesi ya kila Mtanzania anayethamini haki na uhuru. Mfumo wa sheria umerudi kwenye giza, na ni jukumu letu kupaza sauti hadi taa za haki ziwake tena.

#FreeLissu
#GangsterJusticeMustFall
#MahakamaS
iChomboChaWatawala
 
Mkuu hakuna mahakama hapo. Nilisikiliza kesi ya Mbowe ya kubambikiwa ya ugaidi. Ushahidi uliokuwa unatolewa na wanasheria wa serekali ulikuwa ni utopolo mtupu, na utetezi wa upande wa mawakili wa mshitakiwa walikuwa na hoja zenye mashiko, cha ajabu jaji akawa anatoa maamuzi yaliyo nje kabisa ya ushahidi. Unapoona wanawazuia wanasheria wa nje, lengo ni kuficha huo upuuzi unaopangwa na serekali. Hapo hakuna kesi bali wanamkomoa Lisu kisha DPP atapanga kutoendelea na kesi, ila Lisu atakutwa na kesi ya kujibu. Huo ndio upuuzi uliopo humu nchini kwa sasa.
 
Back
Top Bottom