Mahakama Kuu yaridhia mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) kuapishwa. Maombi ya Lissu kupinga mambo kadhaa kutolewa uamuzi Sept 9

Mahakama za Tanzania ni kama hazina consistent katika utendaji wake. Zimengiliwa sana siasa

Mahakamaccm mawakiliccm ingawa Jaji siyo jajiccm ameonyesha kuwa moyoni hapendi uonevu dhidi ya Tundu lisu lakini leo watakesha kwake mpaka atoe maamuzi yasiyo ya kisheria ya kuishangaza Dunia yote
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kama ni taasisi ndiyo inayotumika basi ni kweli ni mkusanyiko wa vilaza. Ndiyo maana bunge sijui ni bange lazima ni dhaifu sana
Hayo pia ni maoni yako. Yako tolerated. Lakini hayaondoi ukweli hiyo Taasisi ya Bunge ndio inawaongoza wote Bungeni. Na ukijifanya mjuaji unashughulikiwa. Lissu kajifanya mjanja habari take anaipata.
 
Kabisa Mkuu wanamuhofia yule dhalimu anayeteka, kutesa, kubambikia lesions hata KUUA ili tu kutimiza matakwa yake na kuwakomoa wale wasiokubaliana na maovu yake mbali mbali nchini.

Sitarajii kuona haki ya Lissu kwenye hili. Mahakama imejaa hofu kuwatendea haki wapinzani.
 
Kwanza inanibidi nimpongeze aliyeandika huu mhtasari wa yaliyojiri mahakamani. Kama ni wewe 'Mwananamwa' mleta mada; nakupongeza kwa kufanya kazi nzuri iliyonyooka na kueleweka na kuiwasilisha hapa JF.
Ni kazi inayosomeka vizuri na kueleweka, hasa kuhusu maelezo aliyoyatoa Msomi Kibatala. Huko mwisho mwisho hapakueleweka vizuri walipokuwa mawakili wa serikali wakieleza ya kwao. Hii inawezekana mwandishi alikuwa kaanza kupoteza umakini kutokana na uchovu au mawakili hawakufanya kazi nzuri katika uwasilishaji wao.

Pili, kutokana na yaliyowasilishwa, ni matumaini yangu makubwa kwamba sheria haitapindishwa hapa kwa sababu za kisiasa. Hii mahakama ni lazima ionekane inatenda haki.
Sitegemei kamwe kuona mizengwe katika hili.

Tatu, natamani maeneo yote nchini waliko wasomi wetu wote katika nyanja mbalimbali wakifanya kazi zao kwa umakini kama hawa mawakili akina Kibatala. Huu ni mfano wa kuigwa sana sehemu zote.
Kikundi cha watesi na mawakili wa Serikali ambao wao hawajui kitu zaidi ya kuwabambikia watu kesi tu vichwa vinawauma sana
 
Kabisa Mkuu wanamuhofia yule dhalimu anayeteka, kutesa, kubambikia lesions hata KUUA ili tu kutimiza matakwa yake na kuwakomoa wale wasiokubaliana na maovu yake mbali mbali nchini.
Mmejazäna vyumba vya mahakäma na kusähau kampeni za uchaguzi serikali za mitaa. Mkishindwa mnatafuta mchawi.
Aliyewaroga Mungu ambariki kwa kweli.
 
Duuh kwa Aina hii ya haya Maswali ya huyu Jaji, napata tumaini Jipya naendelea Kumuombea Kwa Mungu Muweza wa Yote Huyu Jaji naamini kupitia Yeye Kuna funzo la kisheria litadhihirika.

Haki Huinua Taifa.
 
Mkuu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya Ndugai na Spika. I think their naivety makes them so.
Hapa sijui unataka kusema nini! Au ndo yale yale ya huyo huyo Ndugai kwamba hataki kufanya kazi na Prof Asadi ila atafanyakazi na CAG!

Watu mlioenda darasani kukariri vitabu mnatusumbua sana sisi tuliobaki mtaani huku tukihangaisha bongo zetu kufikiri.

Labda nikupe changamoto kidogo unaposema watu wanatakiwa kumtofautisha Ndugai na Spika!

1. Kwa sasa Spika ni nani?

2. Je, kiti cha Spika kikivurunda tuseme amevurunda nani!?

3. Ni halili kutenganisha maamuzi ya Spika na maamuzi ya Ndugai anapoyatoa akiwa bungeni?

4. Ikitokea kiti cha Spika kinatakiwa kuwajibishwa awajibishwe nani!?
 
Mahakama ikiridhia huyo bwana aapishwe sasa nini itakuwa hatima ya kesi? Will it still be relevant? Won't such decision affect the credibility of the case???
 
Vyumba vya mahakama vimetosha watanzania wafuasi wa vyama wa nchi nzima?
Mmejazäna vyumba vya mahakäma na kusähau kampeni za uchaguzi serikali za mitaa. Mkishindwa mnatafuta mchawi.
Aliyewaroga Mungu ambariki kwa kweli.
 
Hata kama Lissu akinyanganywa haki yake.
Serikali itapata hasara kwa kulipa kule Afrika kusini
 
Mara paap, mahakama yatoa amri ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge naniliu! Mara paap, amri ya mahakama yakimbizwa idodomya kwa kutumia ndege ya kukodi na nakala ya amri ikitumwa kwa whatsapp, email, n.k kwenda kwa anuani za mjengoni na kwa ofisi ya sabwuufa! Mara paap, wapokea nyaraka wa ofisi ya sabwufa wote wana udhuru, hawajafika kwa ofisi. Mara paap! Subwufa anaingia mjengoni, Dua inasomwa, na shughuli za mjengoni zinaanza!

Hivi nimeandika nini jamani? Kama naota vile!???
Tutarajie isidingo la aina hiyo...
 
Back
Top Bottom