Mahakama Kuu yaridhia mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) kuapishwa. Maombi ya Lissu kupinga mambo kadhaa kutolewa uamuzi Sept 9

MAAMUZI YA JAJI YAKO WAZI:

Ili ndilo tatizo la ukilaza walionao watu wengi, nani kasema fulani kashinda kesi na fulani kashindwa?

Kwa mtu mwenye akili zake timamu uelekeo wa hii kesi unaonekana tu.

JAJI kasema kuapishwa kwa huyo mbunge hakuawezi kuathiri kesi iliyopo mahakamani, Kwa akili ya kawaida ungejiuliza kesi ikiyopo mahakamani inahusu nini? Ukijiuliza ilo swali linaweza kukufanya uelewe nini Jaji ameeleza.

Ipo sheria inayosema mbunge akishaapishwa ubunge wake hauwezi kutenguliwa na mahakama?

''...… But Judge Matupa ruled that in cases involving representation in the parliament, a person can be stripped off of his/her seat even after he/she has been already sworn-in''.

Wacha kupotosha.
 
Utafanya nini ww wakati 95% ya wananchi wako wanavaa mitumba toka ulaya?

Kuvaa mitumba ni choice. Awamu ya kwanza hakuna aliyevaa mitumba, Je, kimetokea nini? Sio lazima kuwategemea, tatizo lako husomi ukaelewa umejaa visasi huko kichwani na aliyekuloga kesha kufa.
 
Ni choice au ni no choice? Awamu ya kwanza hawakuvaa mitumba ila waliishia kuvaa viraka. Na kwa ile aibu ya kuvaa viraka ndio iliyopelekea mitumba kuja nchini, na leo huu mitumba ukizuiwa zaidi ya nusu ya watanzania watavaa matambara.
 
Una miaka mingapi wewe? Kabla ya vita ya kumtoa nduli Tanzania hakuna aliyekuwa anavaa viraka labda kama yeye mwenyewe alikuwa hana uwezo. Kumbuka masikini wapo kila nchi, achana na nadharia unayoisikia. Kumbe hata historia hufahamu upo hapa kupotosha tu.
 
Unajua kusoma lakini huna uwezo wa kuelewa, angalia nimesema awamu ya kwanza hawakuvaa mitumba lakini waliishia kuvaa viraka, au hujui awamu ya kwanza ilishia vipi? Kwa hiyo vita vya Uganda ndio pekee vilichangia watu kuvaa viraka? Kwa hiyo leo tukienda Libya watu wanavaa viraka kisa wana vita? Ukija kwangu ujipange, uzalendo uchwara haukubebi hapa.
 
Level yako ya understanding ni sawa na sifuri, sasa ndio umeandika nini hapo then wewe na vikuwadi vyako unafikiri kutawala hii nchi? Phew!
 
Kajipange dogo, uzalendo wa mihemko haukubebi hapa. Huku umepotea njia dogo.
 
Nakumbuka wakati ule Bunge lilipokuwa likionyeshwa moja kwa moja(live),mara kadhaa tulishuhudia Spika,Naibu Spika ama Wenyeviti wa Bunge wakizuia baadhi ya mijadala kwa hoja kuwa jambo husika liko mahakamani.

Cha ajabu,ni Bunge hili hili lililoko katika nchii ile ile yenye katiba ile ile linamuapisha mbunge ambae ubunge wake unahojiwa mahakamani katika mahakama za nchi ile ile zinazotambuliwa na katiba ile ile.
 
No wonder kuna mwanasiasa aliwahi sema, "this is United Republic of Gan......!!"
Kinachohojiwa mahakamani siyo ubunge wa Mtaturu bali uhalali wa matendo ya Spika Ndugai!
 
Ni uamuzi huo unaohojiwa ndio uliosababisha kupatikana kwa huyo mbunge anaeapishwa, mbunge ambae uhalali wake ungetegemea maamuzi ya mahakama.
Hahahaa...... Yule mbunge amechaguliwa kwenye uchaguzi halali kwa mujibu wa sheria.

Mambo ya sintofahamu ya Tundu Lisu na Spika Ndugai hayamuhusu.

Kama Spika Ndugai alikosea kumfukuza Tundu Lisu basi ataadhibiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na itamlazimu amlipe fidia Tundu Lisu na wapiga kura wa Singida mashariki kwa " ukatili" aliowatendea.

Mbunge mteule mh Mtaturu hausiki kwa chochote hapo!
 
Kinachohojiwa mahakamani siyo ubunge wa Mtaturu bali uhalali wa matendo ya Spika Ndugai!
Ngoja, katika pitiapitia jf nimesoma wewe ni KE! Nikashangaa sababu ya avatar! Nikashangaa pia P. anapomuita Wakudadavua ME! Nchi ya viwonder kibao. Nakupongeza kwa hili bandiko. Umekuwa makini kuliko jaji wa ujaji wa fadhila. Kilichohojiwa ni uhalali wa Spika kumvua Lisu ubunge. Hayo mengine ni matunda ya uhalali au uharamu wa tendo hilo la Spika. Likiwa halali, matunda pia ni halali. Likiwa haramu, matunda ni haramu pia. Hili ni dhahili.
 
Haki iko mbinguni tu kwa wanaoamini tu. Ila kwa mahakama zetu no please ila Lissu amebeba kitu kikubwa kwenye maisha yake ndio maana Mungu kamwacha Hai ili watesi wake washuudie ukuu wa Mungu aliye Hai. Jana nilikuwa nasoma biblia kitabu cha Daniel 6 jinsi Daniel walivyomfanyia lakini faraja ni pale wale watesi wake ndio walioangamia wao, watoto wao mpaka wanaowazunguka.
 
Nakumbuka wakati ule Bunge lilipokuwa likionyeshwa moja kwa moja(live),mara kadhaa tulishuhudia Spika,Naibu Spika ama Wenyeviti wa Bunge wakizuia baadhi ya mijadala kwa hoja kuwa jambo husika liko mahakamani.

Cha ajabu,ni Bunge hili hili lililoko katika nchii ile ile yenye katiba ile ile linamuapisha mbunge ambae ubunge wake unahojiwa mahakamani katika mahakama za nchi ile ile zinazotambuliwa na katiba ile ile.
Ahaaaa mkuu hii ni Tanzania hakuna kinachoshindikana chinoi ya Tanzania ya Sipika
 
Nchi ya ajabu sana hii ndugai kinachowekwa akiba sio fedha tu benki hata maneno huwekwa akiba wewe ropoka tu miaka iliyo baki ni mitano tu.
 
Back
Top Bottom