Mahakama Kuu yaridhia mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) kuapishwa. Maombi ya Lissu kupinga mambo kadhaa kutolewa uamuzi Sept 9

Kwanza inanibidi nimpongeze aliyeandika huu mhtasari wa yaliyojiri mahakamani. Kama ni wewe 'Mwananamwa' mleta mada; nakupongeza kwa kufanya kazi nzuri iliyonyooka na kueleweka na kuiwasilisha hapa JF.
Ni kazi inayosomeka vizuri na kueleweka, hasa kuhusu maelezo aliyoyatoa Msomi Kibatala. Huko mwisho mwisho hapakueleweka vizuri walipokuwa mawakili wa serikali wakieleza ya kwao. Hii inawezekana mwandishi alikuwa kaanza kupoteza umakini kutokana na uchovu au mawakili hawakufanya kazi nzuri katika uwasilishaji wao.

Pili, kutokana na yaliyowasilishwa, ni matumaini yangu makubwa kwamba sheria haitapindishwa hapa kwa sababu za kisiasa. Hii mahakama ni lazima ionekane inatenda haki.
Sitegemei kamwe kuona mizengwe katika hili.

Tatu, natamani maeneo yote nchini waliko wasomi wetu wote katika nyanja mbalimbali wakifanya kazi zao kwa umakini kama hawa mawakili akina Kibatala. Huu ni mfano wa kuigwa sana sehemu zote.
 
Mara paap, mahakama yatoa amri ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge naniliu! Mara paap, amri ya mahakama yakimbizwa idodomya kwa kutumia ndege ya kukodi na nakala ya amri ikitumwa kwa whatsapp, email, n.k kwenda kwa anuani za mjengoni na kwa ofisi ya sabwuufa! Mara paap, wapokea nyaraka wa ofisi ya sabwufa wote wana udhuru, hawajafika kwa ofisi. Mara paap! Subwufa anaingia mjengoni, Dua inasomwa, na shughuli za mjengoni zinaanza!

Hivi nimeandika nini jamani? Kama naota vile!???
Kuna wakati ndoto zinakuwaga kweli... Bunge liko Dodoma na mahakama iko Dsm na wanasemaga "government works on paper"

Ili ngoma iwe droo itabidi amri ipelekwe kwa vyombo vya habari waifikishe kwa wananchi na spika aipate huko kama mlalamikaji alivyopata taarifa ya kuvuliwa ubunge barabarani!!!
 
Maamuzi aliyotoa Ndugai hayapo katika sheria zataasisi anayoiongoza hivyo ni yake na ndio matumizi mabaya ya madaraka.
Kanuni zote hajafuata hivyo aje tuu atoe ushahidi.
Kama Mkapa aliitwa kutoa ushahidi kesi ya Mahalu itakuwa Ndugai?
Ni mtazamo wako na hauondoi ukweli kuwa maamuzi ya Ndugai ni ya kitaasisi na ndio maana hashtakiwi Ndugai. Yanahojiwa maamuzi ya Spika. For a layman it's very difficult to comprehend.
 
Ni mtazamo wako na hauondoi ukweli kuwa maamuzi ya Ndugai ni ya kitaasisi na ndio maana hashtakiwi Ndugai. Yanahojiwa maamuzi ya Spika. For a layman it's very difficult to comprehend.
Ni kipi hapo kigumu mkuu hadi "layman" ashindwe kufahamu?
 
Mawakili wamekiri kuwa Lissu aliwaandikia Barua akiwa Nairobi na Belgium
Wanaulizwa anafanya nini
Wanajibu hawajui
Nimeshangaa sana nilipojisomea kule titwer wanajichanganya sana hawa mawakili uchwara WA serikali.
 
Mhe Jaji: Barua aliziandika Akiwa wapi?

Wakili wa Serikali: Aliandika Nyingine akiwa Nairobi na Nyingine Akiwa Ubelgiji

Mhe Jaji: Huko Alikuwa anafanya Nini?

Wakili wa Serikali: Hatujui, hakulitaarifu Bunge


😂😂😂😂😂
 
Mahakama ya Tanzania ni huru na haijawahi kuacha kutenda haki. Mimi kinachonishangaza ni kwamba wakishinda watu fulani mahakama imetenda haki lakini wakishindwa mahakama haijatenda haki! Hii siyo sawa hata kidogo.
Wanasema eti haki itendeke na ionekane imetendeka
 
Ndugai alitoa maaamuzi kama Taasisi not as a person. Na Taasisi hiyo ndio iko mahakamani. For laymen ni ngumu kutofautisha.
Kama ni taasisi ndiyo inayotumika basi ni kweli ni mkusanyiko wa vilaza. Ndiyo maana bunge sijui ni bange lazima ni dhaifu sana
 
Mhe Jaji: Sasa Hapo Umesoma Nini Na Unatetea Nini Hapa ? Kasome Katiba Kifungu Cha 71 katiba ya JMT inasemaje...
 
Mhe Jaji: Nendea Kwenye Sheria kifungu Cha 83 Katiba ya JMT inasemaje?

Wakili wa Serikali: Nimepaona na inaelekeza kukoma kwa Ubunge wa Mbunge

Mhe Jaji: Ombi la Mlalamikaji Linasemaje ?

Wakili wa Serikali anajibu

Mhe Jaji: Sasa Hapo Umesoma Nini Na Unatetea Nini Hapa ? Kasome Katiba Kifungu Cha 71 katiba ya JMT inasemaje...

Wakili wa Serikali: Inasema Mbunge atakosa Sifa za Kuwa Mbunge kwa Kukosa Vigezo Vifuatavyo
(A)Atakosa kuhudhuria Vikao 3 mfululizo.

Mhe Jaji: Nitawabana Maswali Mengi sana. Je, Mpo Tayari?


Dah wameshikwa pabaya sana
 
Hawa mawakili wa serikali Ni mzigo.watanzania wote tunajua kilichompata lissu na wapi alipo.huu uhuni aliofanya ndugai wapaswa kupingwa na kila mpenda haki popote alipo duniani.
 
Back
Top Bottom