Mahakama Kuu yaridhia mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) kuapishwa. Maombi ya Lissu kupinga mambo kadhaa kutolewa uamuzi Sept 9

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,075
4,111
Kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge wa Mh Lissu kuunguruma leo kuanzia saa mbili kamili asubuhi katika Mahakama Kuu.

Agosti 23, 2019 Mahakama Kuu chini ya Jaji Silius Matupa ilisikiliza maombi ya msingi ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki yakiwemo ya kutaka mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) asiapishwe bungeni.

Mahakama Kuu ikaitupilia mbali mapingamizi ya upande wa Jamhuri dhidi ya kesi hiyo na badala yake Mahakama imekubali kuendelea na usikilizwaji wa maombi ya msingi ya Lissu, uamuzi huo ulitolewa Augost 26,2019.

Nitaendelea kueleza yanajiri Mahakama Kuu

lissu.jpg


***UPDATE***
Wakili Peter Kibatala amesema,

Mleta maombi, Tundu Lissu hakuwahi kutaarifiwa kuhusu ubunge wake kuenguliwa alisikia tu barabarani

Wakati Lissu anakuja mahakamani ratiba ya bunge ilikuwa haijapangwa kuwa lini Mtaturu ataapishwa kuwa mbunge,kikao kikao cha bunge kinaanza kesho na Mtaturu ataapishwa kiapo Cha uaminifu tunaiomba Mahakama iamuru kuzuia kwa muda kuapishwa kwake.


***UPDATE***

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kuwa ofisi ya Bunge inatambua na ilishiriki baadhi ya hatua katika kuhakikisha Tundu Lissu anatibiwa.

Wakili Kibatala anaainisha namna ya Bunge lilivyokuwa linamlipa Lissu akiwa matibabuni na kuonesha kuwa walitambua alikuwa hospitalini.

Wakili Kibatala anaainisha namna mchakato wa kudai mshahara wa Lissu ulivyofanyika na ofisi ya Bunge na familia kutambua kuwa Lissu alikuwa wapi na anafanya nini. Anashangazwa na taarifa ya Spika Ndugai kuwa hatambui alipo ndio sababu ya kumvua ubunge

Wakili Kibatala anamrejesha Jaji katika maamuzi ya Daud Pete kuendelea kusikiliza shauri hili anamrejesha na kumtaka asome na kuona maamuzi yalivyokuwa

Wakili Kibatala anarejea kesi ya Dickson Mtaimta Vs DPP katika kitabu ni page ya 33. Jaji anarejea.

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kuwa kazi ya kutafsiri sheria ni kazi ya Mahakama na anairejesha katika kesi ya Ally Linusi na wenzake 11 Vs Kampuni ya ........ Nyingine na kuonyesha misingi wa hoja zake.

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kesi ya Masumbuko Rashidi Vs Jamhuri (1997) na kuonesha namna Mahakama ilivyotoa maamuzi na kuendelea kuimarisha hoja zake.

Wakili Kibatala anasema ni haki ya mtu kusikilizwa kabla ya kuchua haki yake hivyo basi Kamati ya Bunge ingempa Lissu nafasi ya kujieleza kabla ya kumvua ubunge wake.

Wakili Kibatala anawakumbusha warejee mahudhurio na mwenendo wa Lissu bungeni kwa kipind cha miaka saba kabla ya kupigwa risasi.

Wakili Kibatala ameiambia Mahakama mleta maombi hakuwahi kutaarifiwa rasmi sababu za Ubunge wake kutenguliwa alisikia barabarani.

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama na anarejea ya kanuni za bunge 8a inayomtaka Spika kufanya yafuatayo katika utoaji na maamuzi kwa haki na bila upendeleo kwa kungozwa na Katiba na Sheria za nchi na kanuni nyingine pamoja na maamuzi na mila za mabunge mengine

Wakili Kibatala anaikimbusha Mahakama juu ya kiapo cha Spika na kusema aliapa kutenda haki na kusimamia sheria kanuni na Katiba hivyo amekiuka hata kiapo chake.Anasoma kiapo cha Spika kuionesha Mahakama

Wakili Kibatala anasoma barua iliyomvua Lissu ubunge huku akisema ameikuta hapa Mahakamani

Wakili Kibatala anaainisha makosa ya barua iliyomvua Lissu ubunge.Anaonesha makosa ya kanuni zilizotumika na kuanisha kanuni zilizotumika kimakosa

Wakili Kibatala anainisha kigungu namba 146 (1) kuhudhuria vikao vya Bunge ni jukumu la kila mbunge
(2) kutokuhudhuria Spika ataitaarifu tume ya uchaguzi. "Mbunge atakaposhindwa kuhudhuria vikao vya bunge spika atampa onyo'' Hii Sheria hii imekaa kimtego mtego sana.Mleta maombi hakupewa nafasi ya kusikilzwa kama kanuni zinavyosema

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kuwa wakati Lissu analeta maombi mahakamani ratiba ya bunge ilikuwa haijapangwa hivyo ratiba ya Bunge imepangwa wakati kesi ikiendelea na kuweka ratiba kesho 3/09/2019 na moja ya jukumu katika kazi za Bunge ni kiapo cha uaminifu.

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kuwa kesho vikao vya Bunge vitaanza hivyo anaiomba Mahakama kutoa notice ya kutokuapishwa kwa Mbunge mteule Mtaturu kupisha kesi ya msingi kusubiri maamuzi ya Mahakama yako tukufu

Wakili Kibatala anaikumbusha Mahakama kuwa ratiba ya Bunge imekuja bada ya kesi ya msingi dhidi ya ubunge wa Lissu imeshafunguliwa hivyo tunaomba Mahakama yako tukufu itoe notice kwa Bunge kwani shunguli ya kwanza kabisa ya kesho ni kiapo cha uaminifu.

Wakili Kibatala anaikimbusha Mahakama hatua zinazohitajika juu ya upatikanaji wa Mbunge na kuanisha ambazo ni tayari hivyo hatua moja ya kiapo cha uaminfu ndio inayosubiriwa kwa mujibu wa ibara ya 64 na kanuni hizo hivyo lazima ale kiapo kwanza ili kukamilisha taratibu zote awe mbunge kamili na kushiriki shunguli za kibunge.

Wakili Kibatala anajibu baadhi ya maswali wakati mahakama ikisubiri kutoa maamuzi


SWALI: Je, Mahakama ina uwezo wa kutoa notice kuzuia uapisho wa mbunge mteule ?

Anawarejesha katika maamuzi wa majaji 3 wa Mahakama Kuu kwa kurejesha kumbukumbu ya Mahakama kuzuia moja ya mjadala bungeni usiendelee kulinda hadhi ya kesi ya msingi iliyokuwa Mahakamani

Wakili Kibatala anaiambia Mahakama kuwa Mahakama kutoa notice kwa kuzuia mijadala ama viapo sababu ya kupisha kesi ya msingi ni jambo la kawaida na si jambo la kushangaza hata kidogo

Wakili Kibatala anaiambia Mahakama, Mtaturu ametangazwa na tume kuwa ni Mbunge hajala kiapo bado ila mbele yako mhe Jaji kuna kesi ya msingi hivyo kulingana na shauri likiwa linahusu ubunge ambao bwn Mtaturu ataapishwa basi Mahakama yako tukufu ina haki na wajibu wa kusimamia haki ya kila mmoja na ndio jukumu la Mahakama hii tukufu. Mahakama hii haitakiwi kuacha mchakato huu kuendela

Wakili Kibatala anasema na kama mchakato wa kumwapisha bwana Mtaturu unaendelea basi itasabisha kesi hii ya msingi kuwa ngumu zaidi kupata maamuzi na haki ya mlalamikaji Tundu Lissu na kusabisha hata mlalamika kuchelewa ama kukosa haki yake.

Wakili Kibatala anaendela kuweka kumbukumbu za kesi za nyuma zenye mwonekano kama kesi iliyo mbele ya Mahakama hii tukufu huku akirejea mahakama na maamuzi haya kuonyesha haki ya mlalamikaji na kuzuiwa kuapishwa kwa mteule Mtaturu kupisha kesi ya msingi kusikilizwa katika Mahakama hii tukufu

Wakili Kibatala anairejesha Mahakama katika hotuba za Majaji zilizopita kuweka sawa hoja zake na kusimamia haki ya mlalamikaji wake ambaye ni Tundu Lissu dhidi ya Spika Nduga


HOJA ZA MAWAKILI WA JAMHURI

Wakili wa Jamhuri:
Baadhi ya aya katika viapo vya waleta Maombi Viliondolewa Na anaorodhesha Aya Hizo. Anadai utetezi wa Wakili Kibatala bado haujakidhi vigezo.


Wakili wa Jamhuri(Abubakari Mrisha): Anarejea Aliyozungumza Mkuu wao wa Utetezi. Anakazia kuwa Vipande vya Kiapo Vilivyondolewa na Mahakama vinaleta picha kuwa hoja za Wakili Kibatala Dhidi ya Mteja wake hazina mashiko

Mhe Jaji anawakumbusha mawakili wa Jamhuri wanakotakiwa Kusimamia na wasiipotezee Mahakama Muda wake.Anamrejesha Wakili wa Serikali katika Sheria asimamie wapi.

Wakili wa Jamhuri anamrejesha Mhe Jaji Katika Vifungu Vilivyondolewa Huku Akivijengea Hoja Kutetea Hoja zake Kuhusu Majibu ya Msomi Kibatala

Wakili wa Jamhuri anatetea Hoja zake na Kuomba Hoja za Wakili Kibatala Zisizingatiwe Kwa Kuwa Mifano na Marejeo aliyoleta Hayaendani Na kesi Iliyopo Mbele ya Mahakama Tukufu

Wakili wa Jamhuri, Anaiambia Mahakama Kuwa Haina Uwezo wa Kuzuia Kuapishwa kwa Mtaturu

Anasema Ili Mahakama Iweze Kusikiliza Na Kutolea Maamuzi Suala La Bwana Mtaturu Kuapishwa Lazima Kuzingatia Mambo Kadhaa ambavyo Amereja na Kutoa rejea Ya Case Kama Hizo

Anaiambia Mahakama Kwa maombi Yaliyoletwa na paragraph zilizoondolewa ni Maombi Yao Kuwa maombi Haya hayatimii Matakwa ama Vigezo alivyotimia Wakili Kibatala katika ambatanisho na kesi kama hii ya Mohamed intapreses aliyotoa Hapa katika Hoja zake

Anaiomba Mahakama Kueleza Vigezo Kwa kuweza Kuonesha Ni kwa namna gani hoja za Msomi Kibatala Hazijaambana na Maombi Yaliyo Mbele Yako



Wakili wa Jamhuri (Mrunde): Anasema wasomi Sana waliotangulia Msomi Kibatala na Wakili wa serikali Mrisha wameeeleza mambo Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Maombi Ya Kuomba notice

..speech of applicant, na huwezi kuchukua kazi za document moja ukaamishia kwenye statement. Kwenye kesi hii wamefanya hivyo kwa hiyo Mh. Jaji ni documents zilizowasilishwa na applicant ndio zinapaswa ziangaliwe kama zinakidhi vigezo.

Katika shauri la Kamishina General, Kenya Revenue Authoury, pamoja na Silvano Uwaki, Mahakama iiliekeza kwenye oda ambazo zipo pamoja na rule ambayo alisema mwanzo, majaji walisema "the statement should not contain more than name,.....

Mlalamikaji anatakiwa kuwepo mahakamani.Kati ya vitu ambavyo Mahakama inapaswa iangalie ni uwepo wa huyu Applicant. Mhe Jaji ktk documents hizo silizowasilishwa Mahakamani, hiyo affidavit haina ushahidi wa kutosha. Rejea kesi ya Mathias Mrumba (2016)

Kiapo cha Alutte Simon Mughwai ina paragraph nane, Paragraph saba zipo kamili Paragraph ya nane baadhi ya vipengele havipo hivo alitupotosha aliposema kuna paragraph nane. Kwa purpose ya kile alichowasilisha msomi Kibatala, baada ya hizo nilizotaja kuna paragraph 9A, 9B, 9D... .....9F, 9G, 9H, 9I, 9J, 9K, 9M, 9N, 9O, 9P, 9Q, 9R, 9V, and 9W

Paragraph nyingine zilizopo ni 11 na 12.Mhe Jaji hizo paragraph nane zilizopo kwenye kiapo cha Allute ndizo zinapaswa zisaidiane na paragraph zilizopo kwenye kiapo cha Lazaro.

Kilichoanishwa Katika paragraph 9D ni maelezo tu ya kilichojiri tar 28/06/2019.

Mhe Jaji: Wewe Unaelewa Nini ?

Wakili wa Serikali
Anasoma Tena Na Paragraph Hiyo Na Kusema Mnamo Tar... Tajwa Hapo Mhe Spika Aliandikia Tume ya.Uchaguzi Barua na Kuitararifu Kiti Cha Ubunge singida Mashariki Kipo wazi Kwa Mujibu Wa Kanuni.

Mhe Jaji: Hamna Barua Yoyote ya Lissu Ikiwajuza Yupo Wapi !?

Wakili wa Serikali: Katika Ambatanisho hizi Mhe Lissu kashaliandikia Bunge jumla Ya Barua 6 akiwa Hospitali na Katika Kifungu F ameanisha Viongozi waliomtembelea akiwepo Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT

Mhe Jaji: Barua aliziandika Akiwa wapi?

Wakili wa Serikali: Aliandika Nyingine akiwa Nairobi na Nyingine Akiwa Ubelgiji

Mhe Jaji: Huko Alikuwa anafanya Nini?

Wakili wa Serikali: Hatujui, hakulitaarifu Bunge

Wakili wa Serikali anaendelea, Kiapo Cha Allute Mughwai Lissu hakijakamilika sababu hakijaonyesha mleta Maombi Alikuwa na Interest Gani Kuleta Shauri Hili Katika Mahakama Hii Tukufu, In Case Mtaturu akiapishwa mlalamikaji ataumia kwa kiasi gani.

Kesi za Jamhuri zilizoainishwa na Wakili Kibatala zilishatenguliwa maamuzi hayo.

Mhe Jaji sio mara ya kwanza kwa Mahakama hii kupuuzia ombi la mtu yeyote aliyeshindwa kuainisha interest zake. Anarejea baadhi ya kesi zilizopita.

Mhe Jaji: Mlalamikaji alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki?

Wakili wa Serikali:Hilo sina Ubishi Nalo

Mhe Jaji: Nini Kilitokea Tarehe 28/06/2019

Wakili wa Serikali: Kilichotangazwa Ubunge wa Lissu Ulikoma kwa mujibu wa sheria za Tanzania

Mhe Jaji: Nendea Kwenye Sheria kifungu Cha 83 Katiba ya JMT inasemaje?

Wakili wa Serikali: Nimepaona na inaelekeza kukoma kwa Ubunge wa Mbunge

Mhe Jaji: Ombi la Mlalamikaji Linasemaje ?

Wakili wa Serikali anajibu

Mhe Jaji: Sasa Hapo Umesoma Nini Na Unatetea Nini Hapa ? Kasome Katiba Kifungu Cha 71 katiba ya JMT inasemaje...

Wakili wa Serikali: Inasema Mbunge atakosa Sifa za Kuwa Mbunge kwa Kukosa Vigezo Vifuatavyo
(A)Atakosa kuhudhuria Vikao 3 mfululizo.

Mhe Jaji: Nitawabana Maswali Mengi sana. Je, Mpo Tayari?

Wakili wa Serikali: Anakubali Kujibu

Wakili wa Serikali anarejea kesi Ya Joshua Nassari huku akiomba Mahakama Kumuelewa.


WAKILI MKUU WA SERIKALI (Alesia Mbuya)
Maombi hayo hayana nia njema kama ambavyo sheria inaelekeza.

Ingawa suala la ugonjwa linatokea kwa mtu yeyote na wakati wowote lakini si kigezo cha kukiuka sheria ili baadaye alete maombi kama hayo mahakamani.

Alikuwa na mwakilishi wa familia, ambaye ni kaka yake aliyemtaja kwa jina la Mughwai, akibainisha kuwa alikuwa akifanya mawasiliano na Bunge kuhusu stahiki za Lissu lakini hakuwahi kumwandikia barua spika kuomba ruhusa.

"Hii inatufanya tuone mwombaji hakuwa na nia njema. Katika kiapo chake hajasema anarudi lini. Anasema hana tatizo na uchaguzi wa Mtaturu, lakini hataki aapishwe, maana yake ni ili wakose wote. Ndio maana tunasema hana nia njema,” amesema Mbuya.


Wakili wa Jamhuri(Tango)
Kuhusu kusimamishwa kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu, Kwa mujibu wa katiba inazuia mhimili kuingilia mwingine katika utekelezaji wa majukumu yake.

Katika kuunga mkono hoja hiyo, nawasilisha mahakamani uamuzi wa mahakama katika kesi mbalimbali ikiwemo ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) dhidi Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na ya waziri wa zamani, Augustine Mrema.


UPDATES: 2130HRS;

Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam itatoa maamuzi kuhusu maomba kadhaa ya Tundu Lissu Septemba 9, 2019 hivyo mbunge mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraj Mtaturu (CCM) ataapishwa hapo kesho na iwapo kuna ulazima wa kutengua kiapo chake itajulikanabaadaye.

Kujua kesi ilivyoanza, soma

Kujua mapingamizi, soma

Uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya mapingamizi ya Serikali, soma
 
Mahakama za Tanzania ni kama hazina consistent katika utendaji wake. Zimengiliwa sana siasa
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom