Mahakama kuu Arusha yamvua ubunge Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), yaamuru uchaguzi urudiwe

Agizo liliishatoka kuwa mahakimu na Majaji wahakikishe Serikali na CCM haishindwi kesi yeyote hivyo huo ni utekelezaji wa Agizo la kauli ya yule.
Mnaposhinda case agizo hutoka wapi?
 
Hizi "sababu" CCM walizozitoa hapa kwenye case hii, na zile alizozitoa Kafulila kwenye ile case yake, zipi ni nzito za kusababisha matokeo yafutwe?
 
Mimi ni CCM ila kwa Arusha hata uchaguzi urudiwe mara ngapi hatuwezi kumshinda Chadema.. Tena ndio mkoa wa Lowassa hata iweje CCM hatushindi..

Huyi Jaji kapoteza fedha zetu bure kwa kitu ambacho kiko wazi

Mnafiki hana tofaut na mbwa koko......mimi ni ccm na daima nitaamin ktk kushinda sio kushindwa
 
Nasikia wanarudisha jimbo la Longido huko Dodoma ili kura zipigwe huko CCM washinde....LOL!
 
Kwakuwa Mbinu Hii Ya Kutengua Matokeo Ya Uchaguzi imefanya Kazi Zanzibar Kwa 100%, Wanahisi Ndiyo Njia Mbadala Ya Kubaka Demokrasia??
 
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh ONESMO NANGOLE.

Akisoma hukumu hiyo,Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.

Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole

2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;

"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.
NASHAURI YAFUATAYOO

OLE ASIKATE RUFAAA ANAPOTEZA HELA ZAKE
CHADEMA WAPELEKE TIMUYA KULINDA KURA NA WAHAKIKISHIA

CCM KULE WATAPATA MWENYEKITI WA SERK ZA MITAA NAKUSHUKA CHINI

KUNA SEHEMU ZA KUPAMBANA NA CCM SIO HUKOO..HATAWAO WANAJUA HILOO
 
Jukwaa limejileta lenyewe..
Ukizingatia ccm haina ubavu katika aneo hilo..
Watu wana hasira ya kukosa kuona bunge lao moja kwa moja..
Watu sukari ya shida..

Mikutano ya kampeni inaweza ikaanza asubuhi kabisa!
 
Back
Top Bottom