Mahakama kuu Arusha yamvua ubunge Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), yaamuru uchaguzi urudiwe

Sio udokta mkuu, ila huyu wa kwetu hakubaliki kihivyo, ningefurahia sana Chadema wangemsimamisha mwingine
Kwa mf.kama nani labda? pia cdhani kama sheria inaweza kuruhusu akasimamishwa mtu mwingine...kama uchaguzi utarudiwa
 
Al-hamdulillah, hapo ndipo Magufuli atajua kwamba serikali yake watu hawaitaki. Ni kushusha NONDO tu kwenye mikutano ya kampeni hata watanzania wayajue maovu ya serikali yake. Na kwa jinsi ulivyo mkoa wa Arusha sasa, CCM hawana chao hapo.
 
Nilishawahi andika hii kitu.Kuwa Arusha na Kilimanjaro kulikuwa na wapiga kura toka Kenya.OFFCOURSE MODERATOR hakunikawiza akafuta huo uzi mara moja.nA KULE MKOA wa Mara walikoshinda CHADEMA kwa kuangalia jicho la pili kama wakenya hawakupiga kura.
Basi kama wakenya walipiga kura ni udhaifu wa serikali, maana ndo ilivyokuwa inatoa vitambulisho vya mpiga kura, inakuwaje wakenya wapewe vitambulisho ili hali si watanzania
 
Aiseee tusubiri tuone huu mtifuano ingawa upepo wa kisiasa unampa nguvu mgombea wa CCM kushinda ukizingatia matokeo ya uchaguzi uliopita jimbo hilo upishano wa kura haukua mkubwa na pia kasi iliyopo sasa ya rais huenda CCM wakaibuka washindi.
Siasa kuibashiri ni kazi kwelikweli
 
Agizo liliishatoka kuwa mahakimu na Majaji wahakikishe Serikali na CCM haishindwi kesi yeyote hivyo huo ni utekelezaji wa Agizo la kauli ya yule.
 
Basi kama wakenya walipiga kura ni udhaifu wa serikali, maana ndo ilivyokuwa inatoa vitambulisho vya mpiga kura, inakuwaje wakenya wapewe vitambulisho ili hali si watanzania

Hujuma za mtandao wa Lowasa uliokuwa ndani ya serikali lakini Mungu si Athumani yanaelekea mwisho
 
Back
Top Bottom