Kwema Wakuu?
Nilikua naomba usaidizi wenu wa msaada wa mawazo. Ninamdai mtu kama TZS 18mil hivi na nikamfungulia kesi ya madai kwenye Mahakama moja ya mwanzo hapa Dar es Salaam.
Bwana yule alikiri kudaiwa na mimi na akahidi kua atakua analipa kidogo kidogo na pesa atakua anakuja kuzilipia mahakamani, nazipokelea hapo tunasainishana. Hii ilikua mwaka 2018 kesi ilipoisha.
Sasa baada ya kulipa mara moja tu hakutokea tena. Nikimpigia simu anazungusha tu, anatoa ahadi ambazo hatekelezi. Niliandika barua mahakamani kuelezea hali ile nikaomba kukazia Hukumu lakini hakuna lililofanyika.
Nikaandika barua ya pili kukumbushia kuhusu barua ya kwanza ya kukazia hukumu lakini kimya. Katika barua zote nilieleza kua niko tayari kutoa ushirikiano kuonyesha mahali mali za mdaiwa wangu zilipo lakini mahakama imekaa kimya.
Barua zote mbili nilikua natoa nakala kisha nabaki na "copy" ambayo imegongwa muhuri wa mahakama kua wamepokea "original" yake.
Nachoomba kufahamu katika hali kama hii natakiwa kufanyaje wakuu? Mdaiwa bado anazungusha lakini mali zake zipo, tena hazizidi kilometer moja kutokea hapo mahakamani.