Magufuli: Wanaopita kwenye barabara za mwendokasi chomoeni tairi za magari yao muuze

nimecheka kweli alipo sema kuwa wale wanaojisaidia kwenye daraja kule juu kwanini wasikamatwe na kupelekwa na kwenye vyoo vya jela
 
Rais John Pombe Magufuli achukizwa na uharibifu na matumizi mabaya ya miundombinu ya mabasi ya mwendo kasi na kuagiza mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kwa wasiofuata sheria.

Amewataka wachukue magari yao na wapeleke kituoni kisha wachomoe matairi ya watuhumiwa wauze na watakuwa wamepata biashara


Mnacheka lakini kwa mwenye busara hapa kuna shida /tatizo kubwa! Na matrafiki watafanya hivyo. Kesho atasema mtu anakuwa mkaidi polisi una bunduki, piga risasi! Na watatekeleza
 
Alikuwa rais hapa watu wakalalamika anakalia mambo kimya sasa amekuja anayejibu naye anaonekana sio mzuri,Jaman nani mwingine mnamtaka?
 
Haya mambo ya sheria na ujinga ujinga ndo yaliotufikisha hapa, undava undava tu kama alivyosema rais ndo nchi hii itanyooka,.. Akienda kituoni anakuta hamna matairi YES next time hawezi rudia tena.. Kumpeleka sijui kwa sheria ni kupoteza muda tuu. Watz wako sugu sana.. Hapa kazi tu.
Yani uwizi utumike kukomesha makosa ya barabarani?
 
Ndiyo akili za kushikiwa hizo kwamba mtu akiandika hapa kupinga hizi sera za kukurupuka basi ana stress, wewe ndio wale wale akili fupi. Huyu fisadi kawekwa madarakani na akina Mkapa na Kikwete ili aendelee kuwalinda na maovu yao. Kama CCM ingetaka kiongozi safi basi Augustino Ramadhani alikuwa hana doa lakini Kikwete na Mkapa wakamhofa kwamba yule anaweza kuikubali rasimu ya Warioba na hivyo kuwaondolea kinga Marais waliotenda maovu madarakani.

Iko siku labda hii akili yako iliyofunga itafunguka na kuona Majanga ya huyu dikteta na sera zake za kukurupuka katika miezi saba tu kishaanza kuweweseka mara anataka kwenda chunga ndege, mara anajuta kuchukua form ya Urais na kauli nyingine chungu nzima ambazo zinawaacha midomo wazi Watanzania wengi.

Katiba hamna time nayo maana mnajua ni kiama cha CCM na itapotea rasmi na kubaki history tu.

Utakufa na hasira towards ccm, relax, the country is safer
 
Nimecheka sana....'kisela' au 'kisera'??????najua unamananisha 'kisela' lakini hawezi kutoa kauli ya aina hiyo...Inaonyesha tu namna Rais anavyochukizwa na tabia ya baadhi yetu watanzania...Ukienda pale kwenye kituo cha DART Ubungo na Kimara, utaona vijana kwenye ngazi zile za kupandia na kushukia wameweka bidhaa zao...kahawa, soda, kashata, bodaboda, baiskeli..na wengine wamelala chini...mpaka abiria wakati mwingine baadhi wanapita kwa wasiwasi mkubwa kwa kuhofia usalama ...vijana wamevaa kapelo wako pale, wanaleta wasiwasi, wengine wanajadili mambo ya Real Madrid, wengine Arsenal, wengine Yanga, wengine 'chura' yaani kelele, mtindo mmoja....Watanzania tuna safari ndefu mno...Yaani vituo vya DART tayari vimegeuzwa vijiwe....
Yote haya hayatoshi kuwa justification ya ofisi kuu ya taifa kutoa maagizo kwa polisi waibe tairi za watuhumiwa ili kukomesha uzembe barabarani.
 
Nilikuwa nasubiri wanafunzi wa UDOM nao wagome, wangeondoka wote- Rais Magufuli

Tumeleta mradi wa mabasi ya mwendo kasi lakini watu wanajisaidia humo. Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Polisi wapo. Wapelekeni wakajisaidie gerezani-Rsis Magufuli

Badala fedha ziende kujenga maabara, madarasa na madawati, zinaenda kuwalipia vilaza.- Rais Magufuli

"Trafiki wakamate magari yanayopita barabara ya magari yaendayo kasi na kutoa matairi na wakihojiwa wajibu, lilikuja bila matairi."-Rais Magufuli
your prezdaa
 
Yote haya hayatoshi kuwa justification ya ofisi kuu ya taifa kutoa maagizo kwa polisi waibe tairi za watuhumiwa ili kukomesha uzembe barabarani.


Duh, nadhani leo nitacheka kweli kwelina kuvunjika mbavu...hii SPEECH ya JPM imewakwaza wengi...hata mimi nilimsikia JPM akisema hivyo lakini mimi nilichukulia vingine, to me, and I am sure to many others, maneno yale yalikuwa with light touch...siamini kuwa kuna polisi atakamata gari na kulipeleka kituo cha polisi na kuchomoa matairi eti kwa kuwa Rais alisema hivyo kwenye hotuba...
 
Back
Top Bottom