Tofauti ya CCM ya Magufuli na wapinzani kwenye dhana za uhuru na haki

Oct 6, 2020
27
50
Kampeini kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 zimeanza rasmi tarehe 26 Agosti, 2020. Vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi vimeanza kunadi ilani, sera na wagombea wao. Katika kampeini hizi. Wakati kauli mbiu ya CHADEMA ni “Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu”, ya ACT ni “Kazi na Bata”, ikiwa na maana kwamba sawa watu wafanye lakini pia wapate uhuru na furaha (kula bata).

Hivyo, wagombea hawa, kama zilivyo ilani zao husisitiza kuwa nchini Tanzania hakuna uhuru wala haki, kwa hiyo hujinadi kuwa lengo lao ni kuwa wachaguliwe kuongoza nchi ili walete uhuru na haki. Hata hivyo, ilani zao na hotuba zao kwenye mikutano ya kampeini, zinaacha sintofahamu kubwa kubwa juu ya tafsiri za dhana za uhuru na haki. Kwa mfano, utamsikia Mh. Tundu Lissu, Mgombea Urais kupitia CHADEMA akisema ataka watanzania wawe huru na wapate haki lakini hataki serilali ishiriki katika kudhibiti njia kuuza uzalishaji mali na utoaji huduma ili kuzifanya ziwe za manufaa kwa taifa zima.

Badala yake, anataka uzalishaji na utoaji huduma vifanywe na watu binafsi kupitia kile kinaitwa nguvu ya soko huria (lisilodhibitiwa na yeyote). Hata hivyo, historia iko wazi kuwa, ubinyaji mkubwa wa uhuru na ukiukaji haki za watu uliopindukia, uliowahi kutokea duniani ulitokana na mifumo ya uzalishaji na utoaji huduma kumilikiwa na watu wachache kwa kisingizio cha lile linaloitwa soko huria. Soko huria limekuwa likiwasaidia watu wachache kujilimbikizia ukwasi mkubwa kwa kumasikinisha kwa kiasi kikubwa watu waliokuwa wengi.

Sasa ukisikia mgombea anaomba achaguliwe ili alete uhuru na haki kwa watanzania kwa kuchagiza mfumo wa soko lisilodhibitiwa na serikali, unajiuliza kama uelewa wake wa hizi dhana uko sawa sawa. Kwa kuzingatia muktadha huu, lengo la makala haya ni matatu. Kwanza ni kufafanua dhana za uhuru na haki; pili ni kunonesha namna zinavyozingatiwa nan a Seriakaili ya Awamu ya Tano (SAT) chini ya Rais John Magufuli; kuonesha namna zinavyopotoshwa na wagombea wa vyama vyama vya upinzani. Mwisho makala yatatoa wito kwa wananchi kuchakata sera za wagombea ili wasiingizwe mkenge na siasa za kitapeli.

Uhuru na Haki

Kuna tafsiri kuu mbili kuhusu dhana za uhuru na haki. Ya kwanza huongelea uhuru wa mtu binafsi, kwa mfano uhuru wa kumiliki mali, kuongea au mtu kwenda kule atakako kwenda. Uhuru binafsi uambatana pia na haki binafsi. Hii ndio tafsiri kuu inayotawala kwenye hizo dhana mbili. Hata haki za binadamu, toka zilizoasisiwa mwaka 1948, hulenga kulinda uhuru na haki za mtu binafsi, (mmoja mmoja). Si lengo la Makala haya kueleza kuwa haki za mtu binafsi si za muhimu, isipokuwa inalenga kueleza kwamba tafsiri ya uhuru na haki haiishii na mtu binafsi. Kuna tafsiri pana Zaidi ya hii.

Kwa mfano hata miaka ile ya utumwa, si kwamba kila mtu kwenye jamii walizotoka watumwa alikuwa anaathirika moja kwa moja na utumwa. Kimsingi walikuwepo maajenti wa biashara hii ambao pia walikuwa wananufaika na biashara hii haramu. Hata katika harakati za kudai uhuru kutoka kwa wakoloni, wapo waafrika ambao hawakupenda ukoloni uondoshwe maana walikuwa ‘wananufaika’ nao. Mtakumbuka kuwa Hayati Baba wa taifa, wakati wa harakati zake za kudai uhuru, ilibidi authibitishie umoja wa mataifa kuwa wale waafrika ambao walikuwa hawaafiki harakati za kudai uhuru, mwishowe waliunga mkono adhima ya kuadai uhuru, vinginevyo usingepatikana.

Nachojaribu kusema hapa ni kuwa, hawa wanufaika wa hii mifumo haramu ya utumwa na ukoloni, kila mmoja kwa namna yake, wangeweza kusema wana uhuru na haki ya kunufaika na kutetea mifumo hiyo ambayo walio wengi waliiona haramu. Kumbe sasa tunagundua kuwa hizi dhana ni kubwa kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja. Bahati mbaya sana, wagombea Urais wa vyama vya upinzani wanaamini kuwa uhuru na haki ni vya watu binafsi; tafsiri yao ya hizi dhana kuna namna zinahalalisha mifumo kandamizi ambayo huwapendelea wachache kwa kisingizio cha haki za mtu binafsi na kuwakandamiza walio wengi.

Tafsiri ya pili ya uhuru na haki ni ile inayolenga jamii kwa upana wake. Ni ile inayolenga kuondoa mifumo ya unyonyaji na ukandamizaji katika nyanja mbalimbali za uchumi, siasa, utamadamuni na fikra. Tafsiri hii haimlengi mtu mmoja mmoja (au mtu binafsi), bali jamii nzima. Hapa jamii huchukuliwa kama kitu kimoja kisichogawanyika. Sio kundi la watu ambalo kila mtu ana haki zake binafsi, bali kitu kimoja ambacho hutokana na watu kushirikiana katika shughuli wanazofanya, pamoja na pamoja na fikra zao. Tafsiri hii huleta dhana ya uhuru na haki ya jamii na kwa maana hiyo, uhuru na haki za watu wote kwa umoja wao kama wanajamii moja.

Tafsiri hii ya uhuru na haki ndio ilitumika kudai uhuru, kupambana na ukoloni mambo-leo, na ndio inaendelea kutumika kupambana na uliberali-mambo leo unaoendelea (ambao wengine huuita utandawazi). Katika kutekeleza/kuishi tafsiri hii, kuna baadhi ya watu hasa wale wanaodai uhuru na haki binafsi ambazo zinamumiza jamii, huumia. Basi hawa wakiumia huanza kupiga kelele, kudai uhuru na haki zao, huku wakijua/kutokujua kuwa katika kudai za kwao, huumiza uhuru na haki za jamii zima.

Kwa hiyo viongozi wa vyama vya upinzani, kina Mh. Tundu Lissu, na Bernard Membe, na waandamizi wao kina Mh. Freeman Mbowe na Zitto Zuberi Kabwe, wamejitoa kutetea uhuru na haki za watu binafsi huku wakilenga kukandamiza uhuru na haki za jamii nzima. Serikali ya Awamu ya Tano (SAT), chini ya Rais John Magufuli, tofauti na hawa wapinzani, yenyewe imejikita kwenye hii tafsiri ya pili ya dhana za uhuru na haki. Mambo ambayo SAT imefanya kwa miaka 5 iliyopita na inayopendekeza kufanya miaka 5 ijayo (kama inakavyoonesha baadae) ni Ushahidi kuntu kuwa inalenga kujenga jamii huru nay a haki.

Kupamabania uhuru na haki

Kupamabania uhuru na haki za jamii hakujaanza leo. Mapambano dhidi ya ukoloni yaliyoongozwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere kwa upande wa Bara, na Hayati Sheikh Abeid Karume kwa upande wa Zanzibar yalikuwa mapambano ya kuondoa dhuluma, unyonyaji wa kikioloni na kuleta uhuru na haki za kijamii za tu/watu binafsi. Haya mapambano yaliendelea baada ya uhuru wa bendera mwaka 1961 Bara, na 1963 Zanzibar, hata baada ya kuzaliwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mwaka 1964. Mwaka 1967 kwa mfano, chini ya uongozi madhubuti ya Baba wa Taifa, iliasisiwa Sera ya Ujamaa na Kujitegemea, chini ya Azimio la Arusha.

Lengo kuu la sera hii, pamoja na mambo mengine, lilkuwa ni kujenga jamii yenye kujitegemea katika nyanja zote, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kifikra. Hii sera haikulenga kuwatukuza mtu mmoja mmoja kwa kuwapa uhuru na haki kama wanavyopendekeza wapinzani. Badala yake ililenga kuleta uhuru na haki za jamii nzima. Labda hii ndio sababu Mh. Lissu amesikika akimshambulia Rais Magufuli hasa katika mkutano wake wa kampeini pale Kawe eti anairudisha nchi nyuma kwa kufanya baadhi ya mambo kwa mrengo wa ujamaa. Mh. Lissu alisikika akisema ujamaa ulishakufa.

Ni bahati mbaya sana kuwa Mh. Lissu hana taarifa/hawezi kung’amua mkanganyiko unaoendelea katika mfumo wa ubepari kuanzia katika kutengeneza matabaka makubwa na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotishia uhai wa binadamu wote lakini kuanzia na watu wan nchi zinazoendelea kama Tanzania. Lissu yeye anapigia upatu soko huria litawale katika uzalishaji mali na utoaji huduma, huku serikali ikiwa inatazama tu. Hili suala limekuwa likuhubiriwa na wanazi wa uliberali lakini utekelezekaji wake umepelekea majanga makubwa kama nilivyotaja awali.

Ndio maana hata kwa nchi zinazoitwa zilizoendelea, zenye ubora mkubwa wa maisha (quality of life) ni zile zilizozingatia sehemu ya falsafa ya usoshalisti ambao kwa Tanzania ulichukua mwelekeo wa ujamaa na kujitegemea. Hivyo ujamaa si fikra ya kubeza hata kidogo kama anavyofanya Mh. Lissu. ACT Wazalendo hao hujiita wajamaa lakini nadhani hulitumia hilo kama kificho cha ajenda zao za uliberali mambo-Leo. Mfano kwa kauli mbiu yao ya kazi na bata, hutetea hata watu wanaotuhumiwa kwa uhujumu uchumi kwa kisingizio kwamba wamenyimwa nafasi ya kufurahi/kula bata na wapendwa wao. Ajenda yao ya kula bata huwasahaulisha kuwa wachache wanapodai haki na uhuru wa kula bata kwa kuhujumu mali za jamii, hufifisha uhuru na haki za jamii pana.

Jitihada za kujenga jamii huru na ya haki zimekuwa muda wote zikikinzana na jitihada za zinazotetea uhuru na haki za watu binafsi kama wanavyofanya wagombea wa upinzani. Kuanzia miaka ya 1980, watetezi wa uhuru na haki binafsi walipata nguvu na msukumo mkubwa sana kutoka mataifa na taasisi za kibepari za kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Katika kipindi kila mtu na familia yake waliambiwa wanawajibika na maisha yao peke yao. Ilibidi kila mtu au familia yake wagharamie elimu, matibabu, wanunue pembejeo za kilimo na zana nyingine za uzalishaji.

Mali nyingi zilzokuwa zinamilikiwa kwa pamoja ziliuzwa kwa watu binafsi ili kujenga sekta binafsi. Madhara yake yamekuwa ni kushuka kwa kiwango cha elimu. Mfumo wa elimu ambao CHADEMA na ACT wanasema unafundisha vijana kujibu mitihani si kupata ujuzi wa kukabiliana na mazingira yao, umerasmishwa na kuchagizwa na ubidhaishaji wa elimu. Wenye shule hukazania vijana wafaulu kwa wingi ili mwaka unaofuata wapate wengi zaidi na hivyo wapate faida zaidi.

Vijana wanaotoka kwenye familia za hali ya chini ndio wameathirika zaidi maana uwekezaji kwenye shule za umma wanakosoma hawa wasiokuwa na uwezo wa kwenda shule binafsi ilikuwa mdogo. Miradi ya kitaifa kama reli, bandari, n.k. nayo ilianza kuendeshwa na sekta binafsi. Sekta zinazokua kwa kasi kama mawasiliano na benki serikali hakuonekani kuwekeza badala yake sekta binafsi ikiongozwa na raia wa kigeni ndio iliongoza, ikitengeneza faida na kuiamishia kwenye nchi zao huku wakila na wenzetu wachache, ilihali watanzania kwa wingi wao wakiendelea kutaabika.

Rais Magufuli kwa miaka mitano iliyopita amejitahidi sana kurekebisha huu mfumo wa soko holela kwa kuongeza udhibiti wa serikali na pengine kushiriki moja kwa moja. Kwa mfano, amedhibiti utoroshaji madini kwa kujenga masoko ya madini kwenye mikoa yote ili minada ifanyike nchini na serikali ipate kodi yake. Imeanzishwa kampuni ya madini ya Twiga ambayo inamilikiwa na serikali pamoja Kampuni ya Barrick ili kuhakikisha madini yanayochimbwa, serikali inapata stahiki zake.

Kwenye elimu imefanya marekebisho makubwa kwenye shule za sekondari kongwe. Labda hii pia imechagiza ufaulu wa kidato cha sita mwaka huu, 2020 ambapo kati ya shule 10 bora kitaifa, 8 ni za serikali. Pia mpango wa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi kidogo cha nne umewezesha watoto wengi kupata fursa ya elimu. Kwenye afya, serikali imejenga zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na mikoa nchi nzima. Dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa 100%. Rais Magufuli anapambana kuondosha uongo kuwa shughuli za kiuchumi na kijamii zinaweza kuendeshwa na nguvu ya soko huria bila serikali kuingilia. Mkwamo uliotokana ushauri huu wa uongo kama nilivyoonesha hapo juu ni ushahidi tosha kabisa. Hivyo tushikamane naye tusonge mbele. Tuachane na laghai laghai za wapinzani.

Ni bahati mbaya sana kwa mfano kuwa Mh. Lissu anawaaminisha watanzania kuwa nchi inaweza kuendelea kwa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi. Katika mkutano wake wa kampeini pale Kawe alisikika akisema kuwa akichaguliwa kuwa Rais atapunguza kodi za uingizaji bidhaa ili wafanyabiashara wengi waweze kuingiza bidhaa nyingi nchini, akiamini kuwa akipunguza kodi wafanyabiashara wataacha kukwepa kodi. Wakati Rais Magufuli anaongelea ujenzi wa viwanda nchini ili kuguza ajira, ujuzi na mapato ya ndani, Lissu anaongelea uingizaji wa bidhaa kwa kodi ndogo sana ili Tanzania izidi kuwa dampo la bidhaa kutoka nje.

Labda ndio anafanya maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa Economic Partnership Agreement (EPA) kati ya nchi za Afrika Umoja wa Ulaya, ambao unalenga kuondoa ushuru wa bidhaa kutoka Ulaya na makamuni ya ulaya kuja Afrika kushindaniaunalengzote, ndo na kubwa, hata za kufagia barabara. Kutapa tapa kwake hakuishi. Amesikika pia akilaani utekelezaji wa sheria kwa kuwabomolea nyumba wavamizi wa barabara ya Dar es Salaam-Morogoro, hasa eneo la Kimara hadi Kibamba, jijini Dar es Salaam. Huyu mtu anayetetea uvunjifu wa sheria si wa kuchagua kuwa Rais. Ni mlaghai. Sasa je, hakutaka barabara ijengwe ili kupunguza msongamano?

Au alitaka wavamizi wapewe fidia kinyume na sheria? Ajabu sana akiwa mkutano wa Segerea amesikika akilalamikia msongamano wa magari jijini. Sasa anataka uondolewe vipi bila kupanua barabara? Pia akasikika anasema daraja linalojengwa Ocean Road — Oysterbay halitasaidia wananchi maana Oyesterbay wanakaa mabalozi na viongozi. Sasa sijui haoni kama wale wakipita darajani watayaachia magari ya abiria/wananchi barabara ya Ali Hassan Mwinyi ili wananchi wapite kwa urahisi? Anatapa tapa. Tumpuuze!

Huyo Mh. Membe amesikika Lindi huko akiwadanganya wananchi kuwa mikoa ya kusini imesahaulika maana haijajengewa barabara za kuunganisha wilaya na wilaya kwa lami. Ni uongo. Ndio shida ya viongozi wenye kushikilia dhana uhuru na haki za kibinafsi. Hii inaweza pia kupelekea chuki miongoni mwa watu wa kusini kudhani wao wanachukiwa na serikali kumbe ni uongo na uatapeli wa wanasiasa. Kazi kubwa iliyofanyika kwenye sekta ya barabara ni kuunganisha mikoa na mikoa kwa lami. Sasa ndio inaelekea ya kuunganisha wilaya na wilaya. Huwezi ongelea mafanikio haya makubwa bila kumtaja Rais Magufuli toka enzi za Serikali ya Awamu ya Tatu ya Hayati Mzee Mkapa hadi sasa.

Image for post

Kwa kuhitimisha, tafsiri za uhuru na haki zipo za aina mbili. Ya kwanza hutetea uhuru na haki za watu binafsi/mmoja mmoja na kukwamisha uhuru na haki za kijamii (za pamoja). Lissu na Membe na waandamizi wao wamechagua hii ili wakifanikiwa wapate kula na wenzao wachache kwa madai kuwa ni uhuru na haki yao kula na kufurahi/ kula bata, huku wakipokonya Mali za kijamii na kuwamasikinisha walio wengi. Ya pili hutetea uhuru na haki za jamii nzima/pana.

Katika kufanya hivyo hukinzana na uhuru na haki za mtu mmoja mmoja ili kuilinda jamii isiparaganyike. Rais Magufuli amaechagua hii ya pili. Nawasihi watanzania umuunge mkono kwa kumpa kura za ndio. Kina Lisu na Membe na waandamizi wao tuwapuuze. Watatukwamisha.
 
Mnalipwa na ccm kuandika hizi topolo zenu ndefu.
 
..soko huria lisilo na udhibiti ni lile waliloanzisha ccm wakati wa azimio la Zanzibar.

..lakini soko huria mahali kwingine kokote ktk mataifa yaliyoendelea kuna mamlaka za udhibiti.

..kwa mfano kuna mamlaka za kuthibiti ushindani na ubora wa bidhaa; mamlaka za kutetea haki za walaji; pamoja na sheria, taratibu, na miongozo, inayothibiti shughuli za kiuchumi na kibiashara.

..soko huria maana yake pia ni soko lenye ushindani wa haki.
 
Back
Top Bottom