Magufuli umekosea kuwapa wachina ujenzi Bagamoyo. Bandari na jeshi ni strategic, economic and security move

Hizi ni projects ccm kupiga hela na ndio maana hata wabunge wetu wanafichwa kuiona mikataba yake, huwezi kuwa na project kubwa kama hiyo halafu huyo mwanachi ambaye unasema ndio atakuwa mnufaika hajui chochote na hii uthibitisho kuwa ni mradi wa kupiga hela.
 
Tatizo lipo hivi..
Mataifa ya mafharibi yakitoa mkopo yanafuatilia matumizi na kama matumizi hayaeleweki mkopo hupati tena kulingana na sheria zao.

Mchina akitoa mkopo hana muda wa kufuatilia pia hata kama utatekelezwa na kampuni ya kichina swala la mradi kama una tija au hauna tija halimhusu.

Nchi nyingi za africa fedha fedha za mikopo toka china haziendi kwenye miradi sahihi, na mara nyingi inakuwa over priced kupitia upigaji wa viongozi.

China inachukulia huu udhaifu kama faida kwa sababu viongozi wa africa kuuza nchi zao hawaoji shida ili mradi wanaendelea kuwa madarakani.

Tumpongeze Magu kwa kupiga chini mkataba wa ujenzi wa reli waliopewa wachina.

Africa inajitaji kuitumia china katika ushirikiano kimaendeleo.. na kuwe na udhibiti wa matumizi ya mikopo.

Mikopo mingi africa haipitishwi na Bunge au na kamati za bunge.
Bunge ndo wapigaji wakubwa, wanalia kukosa ulaji huo... kwanini hatujiulizi kuwa hatusemi mikataba mikubwa ipelekwe MAHAKAMANI ama tume ya kimahakama iliyosheheni MAJAJI badala yake tunaimba BUNGENI ambako kumejaa wapigaji na wanasiasa kama akina ZITTO?????
 
Halafu kwa ubongo wako ulivyooza eti unajiona kama Malcolm X vile; ha ha ha unachekesha na kufurahisha.
Na we ulivyo kilaza unajifananisha na Abdul Nondo, yule jamaa ni kichwa, sio msukule kama wewe unaeshindia Unga wa Ndele hapo Lumumba.
 
Bunge ndo wapigaji wakubwa, wanalia kukosa ulaji huo... kwanini hatujiulizi kuwa hatusemi mikataba mikubwa ipelekwe MAHAKAMANI ama tume ya kimahakama iliyosheheni MAJAJI badala yake tunaimba BUNGENI ambako kumejaa wapigaji na wanasiasa kama akina ZITTO?????
Sasa ndio umeongea nini mkuu au just roho mbaya?

Duniani kote bunge ndio chombo pekee kinacho hakiki maamuzi ya serikali.
 
Unaweza kwenda mbali zaidi kutaafakari athari za mahusiano ya kibiashara kati ya Cina na Nchi za Afrika,
Tazama bidhaa za china zinazotumia cheap technology kama taa, viatu, nguo, mapazia,redio, mapambo nk. Hivi vitu vingeweza kuwa vinatengenezwa Afrika kwa ajili ya masoko ya ndani lakini hata tukitengeneza bei na ushindani dhidi ya bidhaa za china ni kikwazo.
Matokeo yake ni kudorara kwa teknolojia. we are always looking for cheap commodities from China. It will be difficult to grow technologically.
Urafiki gani huu watu ma- giant kama China kuja kufanya biashra reja reja Africa!
Lingine la ajabu ni kwamba wachina wanamind business zaidi kuliko chochote. Ndio maana wanawakumbatia watawala wa Afrika hata kama ni madikteta, hata kama ni wezi au wanawatesa wanachi.
Watawala wanawakimbilia wachina kwa sababu wanakubali haraka kila kitu kukidhi interests za kiuchumi. so they take it as an advantage ku sign mikataba ambayo baadaye itakuwa ni faida kwao na sio kwa faida ya hayo maataifa wanayoyasaidia au kuyakopesha.
HAINA MAANA TUWACHUKIE AU KUWAFUKUZA WACHINA BALI WE OUGHT TO TAKE ALL PRECAUTIONS!
 
Kazi ipo

Basi tuiombee nchi yetu
Kama wanataka kutenda mabaya.. washindwe.

Pia mkiandika kukataa Wachina.. andikeni je iweje.. mushauri jema litakalosaidia..
Mkuu suala si kukataa Wachina bali matokeo ya mikataba yao na kuwepo kwao Africa.
KUmbuka mahusiano ya wakploni na waafrika kipindi cha ukoloni. miongoni mwa dhulma walizotufanyia ni kusaini mikataba ya kilaghai sina haja ya kueleza! lingine lili kuwa kuua viwanada vya asili. tulijifunza kuwa wakoloni walitumia mbinu kadhaa kujenga uchumi wa kikoloni. mmojawapo ilikuwa ni Destruction methods . Mbinu hii bado inatumiwa hadi leo. Under destruction China wana undermine teknolojia na viwanda katika Africa kwa kujaza mabidhaa mengi cheap na menigine fake. hawana mipango mahususi ya ku industrialize Africa No!
Mbinu ya kutoa mikopo mikubwa na kusaini mikataba tata ina makusudi maalumu kwa hivi tunahitaji kuwa waangalifu sana.Watawala wawe makini wasi take advantage ya wachina kutohoji maswala ya demokrasia na utawala wa sheria katika Afrika na kuwakumbatia. Vizazi vijavyo vitajawahukumu watawala wa sasa kama hawako makini!
 
Eenh, unasemaje Malcom? Ni kama ulikuwa unanisubiri nimwagike?
Hapana mkuu, umenena vyema sanaa na mimi nikawa sina cha kuongezea. Maana hayo mambo ya huu mradi tumeyazungumza sana na watu wamesahau kwamba Bagamoyo hata kama Bandari itaendeshwa na Uchina, ile bado ni Special Economic Zone (SEZ) ambako nchi inaweza kunufaika sana katika mambo mengine.
 
Bandari ya bagamoyo ni pasua kichwa.
ile mikataba 21 ya wa msoga na uchina itatutesa sanaaa.
 
wachina watatumaliza, bandari na jeshi ni strategic economic and security move in their favour . Sri Lanka wameshapata matatizo hapo

Tukiweka ushabiki pembeni, nchi yetu inahitaji maendeleo, lakin tuchague aina ya njia tunazoona zinafaa kuleta maendeleo,

Hakuna hasiyejua kwamba China ni wajanja mno katika masuala ya kutafta masoko,

Mbali Zaid China hii siyo Ile ya Mao , hii China yenye Tabia zote za Ubepari na Unyonyaji,

Nchi nyingi zimeumia Kwa mpango huu WA kuwapa wachina wajenge bandari tena za Jeshi,

Tumkosea sana,

Angalia Sri Lanka na nchi kama Taiwan yamewakumba haya

Baada ya kuonekana Sri Lanka anashinikizwa kulipa haraka Deni la kujengewa miundombinu, wakakataa wakasema haiwezekani na Kwa Hali mbaya tunayopitia hii kulipa Kwa makubaliano hayo,

China wakatumia fursa hiyo kuwaambia Sri Lanka kwamba mtupatie sehem nyeti za nchi tuziendeshe sisi tujilipe ndo mzozo ukaanza,

Sri Lanka wakasema basi chukua airport mliyotujengea, China wakakataa kwamba hatutaki airport tupu na ndege zenu tunataka,

Sasa Tanzania kuweni makini Sana na wachina

China Tells Sri Lanka: We Want Our Money, Not Your Empty Airport

Nathan
00069 PGH . Sörnäisten rantatie 18 F
+38068670669*
Magufuli kakuta wachina na mikataba yao kwapani ndugu yangu. JK na Jin ximping walishasaini mikataba 17 miaka kadhaa iliyopita.
 
I agree, Chinese sio wa kuwapa mradi mkubwa hivyo kama port ya Bagamoyo... Watatumaliza... I said this many many times.. China ya leo ni hatari sana na wezi sana kheri mara 10000% ubepari kuliko China ya leo... Meaning China ya leo ni mabepari na wezi wakubwa hasa katika miradi mikubwa..!!

Mh.Rais wetu alivyowanyima tenda ya SGR, nilifurahi sana sana, nikajua na Bagamoyo port atatafutwa investor mwingine ila sio China..!! Chinese are smugglers, looters..!! Mh. Rais wangu namuamini sana, i hope hili swala la Bagamoyo port ni very very sensitive, ningependelea wapewe investor mwingine ila not Chinese
Rais wa China alishasaini mikataba mingi ikiwemo huo wa bandari wakati wa Jakaya. Magufuli hana cha kufanya juu ya hilo. China watamiliki bandari kwa miaka 50 kisha watawapatia nyie. Kuweni wapole. Mpumzisheni Magufuli jamani. Kila kitu mnamtupia yeye tuuuu.
 
Mkuu Malcom Lumumba,

Yaani tuna watu wengi sana aina ya Nathan Jr! Watu hawa wakisikia jambo huwa hawafanyi jitihada za makusudi kufahamu ukweli wake! Watu hawana kabisa taarifa sahihi kuhusu Bandari ya Bagamoyo na wala hawajihangaishi kutafuta ukweli!

Kama ulivyosema, JK pamoja na madhaifu yake lakini alikuwa na maono makubwa sana! Yaani niliona plan ya ujenzi wa SGR hadi mwili ukanisisimka! Very constructive!! Ukiangalia jinsi ambavyo JK alikuwa ame-consolidate SGR na Bagamoyo Port Plans; hakika ni labda uwe mwehu tu ndo ungeweza kumpinga!!

Matokeo yake, JPM kaudaka mradi kichwa kichwa huku akionekana wazi kupelekeshwa na Kagame ambae JK hakumpa nafasi ya kumpelekesha! Hakuna Kagame anachotafuta zaidi ya kuona SGR from Dar es salaam to Kigali; na huko kwingine mtajijua wenyewe na mta-utilize vipi SGR, wala sio concern yake!!!

Halafu basi nimegundua watu hawana kabisa taarifa sahihi kuhusu kinachosemwa Uchina na kutaifisha miradi ya nchi mbalimbali kama Sri Lanka! Hawa wasio na taarifa wala hawafahamu staili ya Magufuli ndiyo iliyoiponza Sri Lanka na wala sio staili ya JK!

Halafu umegusia jambo lingine ambalo wengi hawafahamu! Majority wanadhani Uchina wakishajenga Bandari ya Bagamoyo, ndo basi serikali haitapata chochote hadi bandari hiyo itakaporudi mikononi mwetu! Hawa hawafahamu kwamba ALWAYS kodi ni mali ya serikali na kwamba, hata kama bandari itakuwa under Chinese operations bado kodi yetu tutakusanya!
 
wachina watatumaliza, bandari na jeshi ni strategic economic and security move in their favour . Sri Lanka wameshapata matatizo hapo

Tukiweka ushabiki pembeni, nchi yetu inahitaji maendeleo, lakin tuchague aina ya njia tunazoona zinafaa kuleta maendeleo,

Hakuna hasiyejua kwamba China ni wajanja mno katika masuala ya kutafta masoko,

Mbali Zaid China hii siyo Ile ya Mao , hii China yenye Tabia zote za Ubepari na Unyonyaji,

Nchi nyingi zimeumia Kwa mpango huu WA kuwapa wachina wajenge bandari tena za Jeshi,

Tumkosea sana,

Angalia Sri Lanka na nchi kama Taiwan yamewakumba haya

Baada ya kuonekana Sri Lanka anashinikizwa kulipa haraka Deni la kujengewa miundombinu, wakakataa wakasema haiwezekani na Kwa Hali mbaya tunayopitia hii kulipa Kwa makubaliano hayo,

China wakatumia fursa hiyo kuwaambia Sri Lanka kwamba mtupatie sehem nyeti za nchi tuziendeshe sisi tujilipe ndo mzozo ukaanza,

Sri Lanka wakasema basi chukua airport mliyotujengea, China wakakataa kwamba hatutaki airport tupu na ndege zenu tunataka,

Sasa Tanzania kuweni makini Sana na wachina

China Tells Sri Lanka: We Want Our Money, Not Your Empty Airport

Nathan
00069 PGH . Sörnäisten rantatie 18 F
+38068670669*
Dr Magufuli aliwakatalia, pia hata sgr alikataa, sasa wewe hizi habari umetoa wapi? Au ni habari za zamani haupo updated? Jk ndiyo aliingia makubaliano ila sema kulikuwa na rushwa kubwa mno na gharama zilikuwa inflated, alivyokuja mzalendo akapiga chini zote na kuanza upya, hivyo hata hiyo bagamoyo ikijengwa itakuwa kwa makubaliano mapya. Kuhusu Sri Lanka nimefika huko, kilichowatokea na poor cashflow kwenye miradi, mfano road toll wa sri lank wengi hawakupenda hivyo high way za mchina hazikuwa zinatumika maana waliacha alternative ya bara bara
 
Mkuu Malcom Lumumba,
Halafu umegusia jambo lingine ambalo wengi hawafahamu! Majority wanadhani Uchina wakishajenga Bandari ya Bagamoyo, ndo basi serikali haitapata chochote hadi bandari hiyo itakaporudi mikononi mwetu! Hawa hawafahamu kwamba ALWAYS kodi ni mali ya serikali na kwamba, hata kama bandari itakuwa under Chinese operations bado kodi yetu tutakusanya!
Mkuu Chige kitu ambacho mimi nimejaribu kuwaambia ni kwamba Bagamoyo Mega Port haitageuka kuwa ghost town kama wanavyotaka kutuaminisha. Kwanza hata kama Uchina akiendesha ile bandari kwa miaka 99, kama ulivyosema bado kodi itakuwa ni mali ya watanzania na serikali yake. Makontena zaidi ya laki moja kwa mwaka siyo kitoto eti.

Pili, swala jingine ambalo watu wengi hatujalijua ni kwamba Bagamoyo ni moja kati ya sehemu 14 ambazo ndani ya nchi ambazo zilichaguliwa kuwa maeneo maalumu kwa maendeleo ya uchumi na viwanda al maarfu kama Special Economic Zone (SEZ). Ambako kimkakati ni kwamba sheriaza biashara zitakazokuwa zinafanya kazi eneo hilo ni tofauti kabisa na sehemu nyingine ndani ya nchi. Sheria za uwekezaji Bagamoyo zitakuwa ni tofauti kabisa na sheria nyingine za nchi. Pia ili kukuza kasi ya viwanda hata sheria za uhamiaji na makazi katika eneo hili ni lazima zitakuwa za tofauti kabisa na hizi nyingine.

Kikubwa ambacho watu wengi hawakijui kuhusu Bagamoyo ni kwamba huu mpango haukuanza na Jakaya Mrisho Kikwete. Wakoloni wa Kijerumani waliona Bagamoyo kama sehemu ya kimkakati sana: Mzee Mwinyi alijaribu kutengeneza Special Economic Zones lakini mpango wake haukuzaa matunda. Raisi Jakaya mwaka 2006 ndiyo akatengeneza Sheria iitwayo SPECIAL ECONOMIC ZONES ACT 2006, ambayo ilipitishwa na bunge la Tanzania. Sasa haya majungu dhidi ya yule mzee wa watu sijui yanatoka wapi...

Tatu, hivi mkuu Chige unajua huu mpango wa kufungua Special Economic Zones nchini Tanzania wakina Mzee Mwinyi waliiga huko Uchina ?? Mwaka 1984 Uchina alifungua na yeye Special Economic Zones 14 kama ambavyos serikali ya Tanzania imefanya. Sasa ukienda kule Guangzhou na Shanghai hutakuta bandari peke yake. Kuna uwekezaji mwingi kutoka nje ya nchi, viwanda ndiyo vimejaa kabisa. Sasa haingii akilini unaposema kwamba eneo ambalo litahudumia wakazi wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati litageuka kuwa Ghost Town. Ukisoma ule mpango wa Bagamoyo kuna sehemi walipanga kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya watu 75,000. Hivi utasemaje kwamba huu ni mpango wa hovyo ??

Hebu angalia hiki kielelezo:
Bagamoyo.jpg


Chato Airport ndiyo itageuka kuwa Ghost Town na hili ndilo ilimpasa Raisi ashauriwe vizuri sana. Kama ningekuwa mimi, ningepeleka hizo hela zote kwenye Uwanja wa ndege wa Mwanza ambao najua ungehudumia maelfu ya watanzania kwa kukuza Uchumi wa viwanda na Utalii. Halafu kuna wataalamu walishawahi kuandika mapendekezo kuhusu hili, lakini bahati mbaya sana viongozi wa tanzania ni hawana utamaduni wa kupende kusikiliza ushauri wa kitaalamu nje ya mambo ya siasa.

Tutafika tu lakini....
 
Mkuu Malcom Lumumba,

Upo sahihi kabisa kuhusu sheria zitakazotawala ile special economic zone. Na wakati ule, watu walitembelea Shenzhen na ndoto ilikuwa kuibadili Bagamoyo kuwa Shenzhen ya Afrika. Ingawaje kabla ya SEC Shenzhen ilikuwa ni mji wa kawaida tu lakini hivi sasa ni miongoni mwa majiji 5 kwa uchumi mkubwa nchini China huku ikiwa na GDP takribani mara 6 ya GDP feki ya Tanzania!

Na hilo la idadi ya miaka... hapa JF miaka michache iliyopita wapinzani wa huu mradi waliibua hoja ya kwamba hadi miaka 30 inaisha, na bandari itakuwa imekufa! Nilipohoji kwanini Bandari ya Bagamoyo ndo ife ndani ya miaka 30 na isife bandari ya Dar es salaam yenye umri wa miaka zaidi ya 100, sikupata jibu!
 
Nchi nyingi za Afrika zitakuja jutia sana huu uwekezaji wa Mchina. Maana yeye kutoa pesa kwa ajili ya kujipenyeza haoni shida na hujificha kwenye kichaka cha masharti nafuu. Kwa vile viongozi wetu wanataka mteremko na hawataki Nchi inayotoa pesa kwa masharti mengi na baadaye inataka ifanye ukaguzi wa hizo pesa walizotoa,basi wanaona kimbilio ni China. Tunaambiwa kwa mfano Ethiopia,ile Reli yake hadi Djibouti imegharimu pesa nyingi sana mara kumi ya GDP ya taifa hilo. Sasa ukijiuliza watalipaje,unapata jibu tu kuwa Nchi itawekwa rehani. Morocco nao kwa sasa wana mvutano na China, Ghana ndo usiseme,wao hadi wanaanza wafukuza kutoka Nchini Mwao. Hivi majuzi tumesikia ya Kenya na China. Vp kuhusu ule umoja wa China,Brazil,S. Afrika,India....una manufaa yapi?
Hapa tujipange kwa kweli.
Hivi ubaya wa nchi za magharibi hamuujui? Utafute mlingamishe. Hapa nchi za magharibi zinatutumia kuwasaidia kupigana vita yao na China! Wote ni wale wale!
 
Back
Top Bottom