Magufuli umekosea kuwapa wachina ujenzi Bagamoyo. Bandari na jeshi ni strategic, economic and security move

wachina watatumaliza, bandari na jeshi ni strategic economic and security move in their favour . Sri Lanka wameshapata matatizo hapo

Tukiweka ushabiki pembeni, nchi yetu inahitaji maendeleo, lakin tuchague aina ya njia tunazoona zinafaa kuleta maendeleo,

Hakuna hasiyejua kwamba China ni wajanja mno katika masuala ya kutafta masoko,

Mbali Zaid China hii siyo Ile ya Mao , hii China yenye Tabia zote za Ubepari na Unyonyaji,

Nchi nyingi zimeumia Kwa mpango huu WA kuwapa wachina wajenge bandari tena za Jeshi,

Tumkosea sana,

Angalia Sri Lanka na nchi kama Taiwan yamewakumba haya

Baada ya kuonekana Sri Lanka anashinikizwa kulipa haraka Deni la kujengewa miundombinu, wakakataa wakasema haiwezekani na Kwa Hali mbaya tunayopitia hii kulipa Kwa makubaliano hayo,

China wakatumia fursa hiyo kuwaambia Sri Lanka kwamba mtupatie sehem nyeti za nchi tuziendeshe sisi tujilipe ndo mzozo ukaanza,

Sri Lanka wakasema basi chukua airport mliyotujengea, China wakakataa kwamba hatutaki airport tupu na ndege zenu tunataka,

Sasa Tanzania kuweni makini Sana na wachina

China Tells Sri Lanka: We Want Our Money, Not Your Empty Airport

Nathan
00069 PGH . Sörnäisten rantatie 18 F
+38068670669*

Elezea basi vizuri lini jpm aliwapa na itaanza lini nk
 
Sri Lanka’s debt situation is severe. The country is currently in $58.3 billion deep to foreign financiers, and 95.4% of all government revenueis currently going towards paying back its loans. This means that out of every hundred dollars the government brings in only $4.60 is going towards essentials like education and public services.

Sisi kwa sasa nusu ya makusanyo tunalipa madeni

Hii hali mbaya sana kwa Sri Lanka. Hili tayari ni kama koloni, viongozi wao wanakusanya kodi kwa niaba ya wadeni wao.

Ila wanaweza kusema hatuwezi kulipa, (defaulting) na China wasiambulie kitu kwa miaka mingi sana.

Ila kama kweli China inajali inaweza kubadili hii mikopo ya muda mfupi ilipwe kwa muda mrefu badala ya 95% kwenda kulipa madeni labd iwe 50% kwa miaka mingi zaidi kama ilikuwa miaka 10 walipe hilo deni wanaweza kuwapa miaka 20, 30 lakini wasichukue vitu vyao kama bandari.

Pesa nyingine ziende kwenye mishahara, elimu, afya, barabara miundombinu, kuendesha nchi.
 
I agree, Chinese sio wa kuwapa mradi mkubwa hivyo kama port ya Bagamoyo... Watatumaliza... I said this many many times.. China ya leo ni hatari sana na wezi sana kheri mara 10000% ubepari kuliko China ya leo... Meaning China ya leo ni mabepari na wezi wakubwa hasa katika miradi mikubwa..!!

Mh.Rais wetu alivyowanyima tenda ya SGR, nilifurahi sana sana, nikajua na Bagamoyo port atatafutwa investor mwingine ila sio China..!! Chinese are smugglers, looters..!! Mh. Rais wangu namuamini sana, i hope hili swala la Bagamoyo port ni very very sensitive, ningependelea wapewe investor mwingine ila not Chinese

Kitu muhimu ni usimamizi thabiti wa kila kitu, kuweka watu wasiopenda rushwa.

Mbona hawafanyi mambo ya kijinga USA na Ulaya ambapo wamewekeza sana. Hata Singapore, Dubai wamewekeza hizi nchi ndogo sana lakini wana misimamo, wanasimamia rasilimali zao, wahakikisha hawachezewi.

Hii mikataba pia iwe inawekwa wazi kwa wananchi wote.
 
Msaada kwa anayejua tafadhali, Huu Mradi umefikia wapi na una masharti gani.?
Kwanza ninachojua Hii contract mzee Magu alikuta ishasainiwa tayari japo kwasasa kumekuwa na suasua kwa ujenzi! lakini ujenzi ulianza kipindi cha JK
 
wachina watatumaliza, bandari na jeshi ni strategic economic and security move in their favour . Sri Lanka wameshapata matatizo hapo

Tukiweka ushabiki pembeni, nchi yetu inahitaji maendeleo, lakin tuchague aina ya njia tunazoona zinafaa kuleta maendeleo,

Hakuna hasiyejua kwamba China ni wajanja mno katika masuala ya kutafta masoko,

Mbali Zaid China hii siyo Ile ya Mao , hii China yenye Tabia zote za Ubepari na Unyonyaji,

Nchi nyingi zimeumia Kwa mpango huu WA kuwapa wachina wajenge bandari tena za Jeshi,

Tumkosea sana,

Angalia Sri Lanka na nchi kama Taiwan yamewakumba haya

Baada ya kuonekana Sri Lanka anashinikizwa kulipa haraka Deni la kujengewa miundombinu, wakakataa wakasema haiwezekani na Kwa Hali mbaya tunayopitia hii kulipa Kwa makubaliano hayo,

China wakatumia fursa hiyo kuwaambia Sri Lanka kwamba mtupatie sehem nyeti za nchi tuziendeshe sisi tujilipe ndo mzozo ukaanza,

Sri Lanka wakasema basi chukua airport mliyotujengea, China wakakataa kwamba hatutaki airport tupu na ndege zenu tunataka,

Sasa Tanzania kuweni makini Sana na wachina

China Tells Sri Lanka: We Want Our Money, Not Your Empty Airport

Nathan
00069 PGH . Sörnäisten rantatie 18 F
+38068670669*

alternatively nani apewe........ ujenzi huo
 
chige kuna mwingine huku anasema Wachina watanyang'anya bandari kama Sri Lanka wakati mkataba wa bandari ya Bagamoyo uko chini ya BOT-Build Operate Transfer: Kwamba Uchina wataijenga bandari ya Bagamoyo kwa miaka 30 na wataiacha.

Unajua bwana Nathan Jr hizi propaganda za kitoto ambazo huwa nawaonya kila siku ifike mahali tuziache. Sasa nikikuuliza Uchina watanyang'anyaje bandari wakati wanaijenga kwa pesa yao na kuitumia kwa miaka 30 halafu wanatuachia najua huwezi kunipa jawabu hapa.

Sasa kama ulikuwa haufahamu, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni muumini wa uwekezaji kwa njia ya BOT (Build Operate Transfer): Moja ya kitu alichowahi kumshauri Mzee Mkapa ni kwamba unapowakaribisha wawekezaji basi hakikisha wanajenge wenyewe hiyo miradi na kuiendehsa ili muda ukipita wawaachie na mpate faida na siyo kubinafsisha viwanda na mashirika ambayo mlitengeneza kwa gharama zenu wenyewe. Sasa hapa ambacho unapinga wewe ni kipi ??

Kitu kingine ni kwamba, ulitaka Uchina akijengee bandari bure au ulitaka uchukue mikopo ya bure?
Ukinitajia nchi ambayo inatoa mikopo ya bure hapa duniani basi hoja yako itakuwa na mashiko sana na bila kufanya hivyo hoja yako nzima itakuwa ni Propaganga Mufilisi inayolenga kuwatishia watanzania wasipige hatua za kimaendeleo (Preaching the politics of fear and the gospel of envy)

Kingine ambacho hujakifahamu ni kwamba hata Serikali ya Mao Zedong ilivyokuwa inajenga reli ya TAZARA kuna maslahi ilikuwa inayapata sana hapa Tanzania: Its Quid Pro Quo. Kama yalikuwa siyo ya kiuchumi basi yalikuwa ni ya kimkakati ndiyo maana ukifuatilia ule ujenzi wa ile reli, mainjia wale waliotembea kwa miguu miezi tisa wakifanya tafiti walishawahi kufanyiwa fujo na wamarekani hadi kupigana kabisa kipindi cha ujenzi hapa Tanzania. Tafuta nakala za ule ujenzi utaelewa nachosema!

Hoja yako ya mwisho kabisa ya jeshi na Ulinzi bado inanitia sana Ukakasi kwasababu sioni uhatari wowote ule kwasababu kama ni Uchina jeshi letu wanalifahamu kuanzia kwenye ngozi hadi mfupa (From skin to skeleton). Kipindi cha miaka ya 70's inasemekana JWTZ ilikuwa na Military Advisors kutoka Uchina kama 700 hivi, ambao wamewafundisha na kuwapa vifaa vya kijeshi wakati wote ule.
Mzee Nyerere alijisifu siku moja kwamba "The Chinese are my friends, and if i want weapons i just say hey i want weapons and they give me" AU unahisi ile vita ya Kagera mlipigana wenyewe eeh ??

Pakistani wamekubali kumpa Uchina Bandari ya Gwadar ambayo ataitanua under BOT (Build Operate Transfer) na kuitumia kwa miaka 40 halafu atawaachia. Kwanini usema Magufuli amekosea kuwapa wachina ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ?? Au mwenzangu ulihisi kwamba tumekopa hela ili kujenga ile Bandari ??

Raisi Jakaya na madhaifu yake yote aliekuwa ni mtu mwenye akili sana na maono ya mbali na ndiyo maana alitaka hadi kuwaacha Wachina wajenge SGR na kutanua TAZARA ili ziunganishe Malawi, Zambia, Congo DRC, Burundi na Rwanda kutokea Bagamoyo. Raisi Magufuli mwanzoni alikuja kama wewe kutaka kuzuia ujenzi wa Bagamoyo Port kisa iko nyumbani kwa wakina Jakaya, lakini unahisi kwainini baadaye alilegea ?? GO FIGURE.........

RAI YANGU KWAKO:
Ungekuwa muungwana sana kama ungemshauri Raisi Magufuli kwamba amekosea kuchukua mkopo ili kujenga SGR na kuipeleka Kigali baada ya kuacha hawa wachina waitanua wenyewe kama walivyopanga mwanzoni na awamu iliyopita. Zaidi ya hapa hizi ni propaganda za kitoto mno zisizo na mashiko tena ambazo hazijajikita katika utafiti wowote ule.

Ungesoma nyaraka za mradi wa Bandari ya Bagamoyo na faida zake kwa Uchumi wa Tanzania, nakuhakikishia asilimia 100% usingediriki hata kupiga hizi propaganda zako.
 
wachina watatumaliza, bandari na jeshi ni strategic economic and security move in their favour . Sri Lanka wameshapata matatizo hapo

Tukiweka ushabiki pembeni, nchi yetu inahitaji maendeleo, lakin tuchague aina ya njia tunazoona zinafaa kuleta maendeleo,

Hakuna hasiyejua kwamba China ni wajanja mno katika masuala ya kutafta masoko,

Mbali Zaid China hii siyo Ile ya Mao , hii China yenye Tabia zote za Ubepari na Unyonyaji,

Nchi nyingi zimeumia Kwa mpango huu WA kuwapa wachina wajenge bandari tena za Jeshi,

Tumkosea sana,

Angalia Sri Lanka na nchi kama Taiwan yamewakumba haya

Baada ya kuonekana Sri Lanka anashinikizwa kulipa haraka Deni la kujengewa miundombinu, wakakataa wakasema haiwezekani na Kwa Hali mbaya tunayopitia hii kulipa Kwa makubaliano hayo,

China wakatumia fursa hiyo kuwaambia Sri Lanka kwamba mtupatie sehem nyeti za nchi tuziendeshe sisi tujilipe ndo mzozo ukaanza,

Sri Lanka wakasema basi chukua airport mliyotujengea, China wakakataa kwamba hatutaki airport tupu na ndege zenu tunataka,

Sasa Tanzania kuweni makini Sana na wachina

China Tells Sri Lanka: We Want Our Money, Not Your Empty Airport

Nathan
00069 PGH . Sörnäisten rantatie 18 F
+38068670669*

Jielimishe zaidi kuhusu mambo haya Nathan Jr, usiyaelewe juu juu tu ukadhani umeyajua.

Hilo la Sri Lanka unalifahamu vizuri? Na Taiwan je? Unajua wana tatizo gani?

Zote ulizotaja hapa unajua vizuri yanayowahusu katika mahusiano yao na China? Ngoja nikuongezee mfano mwingine, Djibouti.

Sijaona ukielezea chochote hapa kinachoeleweka ili nasi tukifahamu vizuri. Umesikia tu habari juu juu, nawe unaamua kuwa mjuzi wa kuyaelezea hayo mambo kwetu ili nasi tuyajue kama unavyoyajua wewe!

Hakuna anayekataa tusiwe waangalifu na taifa lolote wanaokuja hapa kutaka tufanye mambo nasi, kwani inaeleweka kila taifa hufanya mambo yake kwa manufaa ya taifa lao.

Lakini hatuwezi kukataa kutafuta manufaa yetu kwa kuogopa tu kwa kututolea mifano unayoielezea hapo juu, na mingi yake ukiwa unaonyesha huna ufahamu mzuri juu yake.
 
H
chige kuna mwingine huku anasema Wachina watanyang'anya bandari kama Sri Lanka wakati mkataba wa bandari ya Bagamoyo uko chini ya BOT-Build Operate Transfer: Kwamba Uchina wataijenga bandari ya Bagamoyo kwa miaka 30 na wataiacha.

Unajua bwana Nathan Jr hizi propaganda za kitoto ambazo huwa nawaonya kila siku ifike mahali tuziache. Sasa nikikuuliza Uchina watanyang'anyaje bandari wakati wanaijenga kwa pesa yao na kuitumia kwa miaka 30 halafu wanatuachia najua huwezi kunipa jawabu hapa.

Sasa kama ulikuwa haufahamu, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni muumini wa uwekezaji kwa njia ya BOT (Build Order Transfer): Moja ya kitu alichowahi kumshauri Mzee Mkapa ni kwamba unapowakaribisha wawekezaji basi hakikisha wanajenge wenyewe hiyo miradi na kuiendehsa ili muda ukipita wawaachie na mpate faida na siyo kubinafsisha viwanda na mashirika ambayo mlitengeneza kwa gharama zenu wenyewe. Sasa hapa ambacho unapinga wewe ni kipi ??

Kitu kingine ni kwamba, ulitaka Uchina akijengee bandari bure au ulitaka uchukue mikopo ya bure?
Ukinitajia nchi ambayo inatoa mikopo ya bure hapa duniani basi hoja yako itakuwa na mashiko sana na bila kufanya hivyo hoja yako nzima itakuwa ni Propaganga Mufilisi inayolenga kuwatishia watanzania wasipige hatua za kimaendeleo (Preaching the politics of fear and the gospel of envy)

Kingine ambacho hujakifahamu ni kwamba hata Serikali ya Mao Zedong ilivyokuwa inajenga reli ya TAZARA kuna maslahi ilikuwa inayapata sana hapa Tanzania: Its Quid Pro Quo. Kama yalikuwa siyo ya kiuchumi basi yalikuwa ni ya kimkakati ndiyo maana ukifuatilia ule ujenzi wa ile reli, mainjia wale waliotembea kwa miguu miezi tisa wakifanya tafiti walishawahi kufanyiwa fujo na wamarekani hadi kupigana kabisa kipindi cha ujenzi hapa Tanzania. Tafuta nakala za ule ujenzi utaelewa nachosema!

Hoja yako ya mwisho kabisa ya jeshi na Ulinzi bado inanitia sana Ukakasi kwasababu sioni uhatari wowote ule kwasababu kama ni Uchina jeshi letu wanalifahamu kuanzia kwenye ngozi hadi mfupa (From skin to skeleton). Kipindi cha miaka ya 70's inasemekana JWTZ ilikuwa na Military Advisors kutoka Uchina kama 700 hivi, ambao wamewafundisha na kuwapa vifaa vya kijeshi wakati wote ule.
Mzee Nyerere alijisifu siku moja kwamba "The Chinese are my friends, and if i want weapons i just say hey i want weapons and they give me" AU unahisi ile vita ya Kagera mlipigana wenyewe eeh ??

Pakistani wamekubali kumpa Uchina Bandari ya Gwadar ambayo ataitanua under BOT (Build Order Transfer) na kuitumia kwa miaka 40 halafu atawaachia. Kwanini usema Magufuli amekosea kuwapa wachina ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ?? Au mwenzangu ulihisi kwamba tumekopa hela ili kujenga ile Bandari ??

Raisi Jakaya na madhaifu yake yote aliekuwa ni mtu mwenye akili sana na maono ya mbali na ndiyo maana alitaka hadi kuwaacha Wachina wajenge SGR na kutanua TAZARA ili ziunganishe Malawi, Zambia, Congo DRC, Burundi na Rwanda kutokea Bagamoyo. Raisi Magufuli mwanzoni alikuja kama wewe kutaka kuzuia ujenzi wa Bagamoyo Port kisa iko nyumbani kwa wakina Jakaya, lakini unahisi kwainini baadaye alilegea ?? GO FIGURE.........

RAI YANGU KWAKO:
Ungekuwa muungwana sana kama ungemshauri Raisi Magufuli kwamba amekosea kuchukua mkopo ili kujenga SGR na kuipeleka Kigali baada ya kuacha hawa wachina waitanua wenyewe kama walivyopanga mwanzoni na awamu iliyopita. Zaidi ya hapa hizi ni propaganda za kitoto mno zisizo na mashiko tena ambazo hazijajikita katika utafiti wowote ule.

Ungesoma nyaraka za mradi wa Bandari ya Bagamoyo na faida zake kwa Uchumi wa Tanzania, nakuhakikishia asilimia 100% usingediriki hata kupiga hizi propaganda zako.

Hapo kwenye uendeshaji kwa miaka 30, katika pitapita zangu mitaa fulani ya kitaa nikasikia mtu mmoja anadai kuwa Mkuu katoa miaka 99 badala ya 30. Kwavile mimi siko na uhakika na hili ikabidi nikae kimya. Je kuna ukweli wowote kwa hili la kuendesha kwa miaka 99 badala ya 30. Na kama ni kweli kuna tofauti gani kati ya mkataba wa awali na huu wa sasa kimalengo hadi kupelekea kuwa miaka hiyo?

Kingine wakati wa utumiaji wa Bandari hii kwa miaka 30 au hiyo 99 Serikali/ nchi ya Tanzania tutakuwa tunafaidika na nini kutokana na uwekezaji huu wa Chinese?
 
Duuuh mbona mnamuandama sana Uncle Magu. Kwa taarifa yenu miradi uliyotaja yote amekuta imeshasainiwa. Na vyombo vya habari vyooote vilitangaza. Angeikataa mngesema ana chuki na uongozi uliopita. Sasa uncle afanye nini ili mridhike nyie binadamu?????? mnanikera saaaaaaana!!!!!!!!
Kama ni hivyo mbona hujisifia yeye kama ndo muasisi wa hayo maendeleo?
 
Kingine wakati wa utumiaji wa Bandari hii kwa miaka 30 au hiyo 99 Serikali/ nchi ya Tanzania tutakuwa tunafaidika na nini kutokana na uwekezaji huu wa Chinese?
Wewe umeuliza maswali ya msingi kabisa ambayo ningetegemea walio na taarifa za huo mradi wangekupa majibu.

Kwa maoni yangu, siamini kuwa Magufuli angeweza kukubali mkataba huo wa miaka 99 (pamoja na kwamba sikubaliani naye kwa mambo mengi ya msingi zaidi ya hili). Ninavyomwona, hawezi kuiuza nchi kwa mkataba wa namna hiyo; hata kama ungekuwa na manufaa mengi kwa nchi yetu kwa sasa.
Kujenga na kuendesha mradi kama huo kwa miaka 30, ili mwekezaji arudishe gharama na kupata faida yake ni muda mzuri kwake na kwa taifa letu, hapo bandari itakaporudishwa muda ukiisha ili iwe chini ya umiliki wa moja kwa moja kwa taifa letu.

Tanzania itafaidika vipi?

1. Jibu la haraka na moja kwa moja ni AJIRA mbalimbali zitakazozalishwa na mradi huo. Hapa itakuwa ni maelfu ya waajiriwa, na bila shaka sheria zetu zitafanya kazi ili iwe hivyo katika ngazi zote za ajira zitakazo zalishwa. Tukishindwa kusimamia hilo tusiwalaumu wawekezaji.

2. Hizi ajira, ni lazima taifa liwe na utaratibu wa kuhakikisha zinaleta tija zaidi ya mishahara wanazopata waajiriwa. Ni lazima ziwe ajira za kukuza ujuzi wa waTanzania katika kila nyanja za ajira hizo. Hili serikali haijalipa uzito unaostahili mpaka sasa. Pamekuwa na maneno mengi tu ya "skills development na Technology transfer," lakini hapajawekwa mikakati ya kuhakikisha hili linafanyika kwa ufanisi unaotakiwa katika miradi yooote inayoendelea humu nchini.
Hatutaweza kuendelea kama tutaendelea kulifumbia macho hili jambo.
Kama Taifa ni lazima tutilie mkazo zaidi sasa katika kupanua uwezo wetu kupitia kwenye miradi kama hii ili nasi tuweze kabisa kujitegemea katika hiyo miaka 30 ambayo watakuwa wanaendesha mradi huo. Itakuwa upuuzi mkubwa, wakati mkataba unakwisha tunaanza kutazamana tena na kujiuliza nani mwenye uwezo wa kuuendesha. Matokeo yake inalazimu tuwapigie magoti tena waendelee kuwepo katika mradi huo.
Miaka 30, sio mingi. Unaikumbuka TAZARA? Si walijenga wao waChina? Sisi hatukubaki na kitu chochote isipokuwa hiyo reli tu, na hata ujuzi wa kuiendesha kwa faida hatukuwa nao hadi sasa!

3. MAPATO - Wanapojenga na kuendesha mradi kama huo usisahau kuwa watakuwa pia wanalipa kodi mbalimbali kuendena na masharti ya mkataba. Bagamoyo itakuwa bandari kubwa sana na muhimu kwa eneo lote hili la Afrika Mashariki. Lakini kumbuka, mradi huo, sio ujenzi wa bandari pekee. Kuna serikali ya Oman pia na ujenzi wa"Special Economic Zones" na miradi mbali mbali za uzalishaji - viwanda n.k.

4. Binafsi, kinachonivutia zaidi katika mradi huo, hasa 'ujenzi' wa bandari kunahusikana sana na hili: tafuta ramani ya Africa. Tazama ilipo Tanzania. Peleka macho yako toka Mashariki mwa ramani hiyo, yaelekeze yaende Magharibi mwa ramani hiyo. Yavushe Ziwa Tanganyika, na tazama Kaskazini na Kusini katika eneo lote hilo.
Utanisamehe sana kama bado hunielewi ninachokizungumzia hapa.

Let your imaginations take over on the possibilities that are open to be had! Kama uwezo wa kuzitumia fursa bwelele kama hizo tunashindwa kuzitumia, sisi tutakuwa taifa la watu wa ajabu sana.

Nisikuchoshe.
 
Cha muhimu ni kuwa na strategy za kujifunza from the roots ya huo mradi yaani kuanzia ujenzi hadi operations baada ya mradi kukamilika tungekua nchi makini tungeshajifunza kitu from Tazara, SGR tungejenga wenyewe lakini kama tutaendelea hivi hivi na pata potea ioo bandari baada ya miaka 40 itakua ghost town tu.

Lazima kuwe na mkakati wa kielimu turuhusu technology transfer vyuo vyetu vifundishe mambo kama haya tutengeneze professional za kuhandle project kama hizi na kuinnovate mpya za kisasa zaidi.
 
Back
Top Bottom