Uchaguzi 2020 Magufuli ukija Tanga, haya ndiyo yataweza kukupa kura za kishindo

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,350
2,000
Ndugu Magufuli, mkoa wa Tanga uliwahi kuwa mkoa tajiri no.1 East Africa kwa sababu ulikuwa ndio sehemu iliyo ongoza ulimwenguni kwa zao la katani, likifuatiwa na yucatan ya Mexico.

Tokea miaka ya 1970, zao la katani limekufa baada ya nylon kugunduliwa na kuweza kutengenezwa kwa bei nafuu zaidi ya katani. Mashamba mengi yamekufa na yaliyobaki wajaja wameyachukua bila ya kuyaendeleza na kuyachukulia madeni.

Iwapo chama changu itakuja na agenda ya kuhakikisha kuwa mashamba haya yaturudishwa serekalini, pamoja na yale ambayo yapo serekalini, yakafanyiwa utafiti mzuri na yale yasiyo na manufaa kwa muendelezo wa zao la katani, wakagaiwa wananchi wanaishi pembeni ya mashamba hayo na sio watu wa kutokea mbali, wananchi wa Tanga watafurahiya sana jambo hilo, na litabadilisha maisha ya wengi.

Tutaweza ongeza ajira kwenye kilimo kwa zaidi ya asilimia 80%, zao la katani linawanufaisha watu wachache sana.

Tafadhali liangalie hili kwa umakini. 98% ya mashamba ya katani hakuna yanayoendelea, hakuna kilimo wala kazi inayofanyika, yamekuwa mapori tu.
 

dikteta2020

JF-Expert Member
Aug 14, 2018
585
1,000
Katani ya Tanga aliyeua hilo zao ndiye huyo huyo unayemuita aje kulikuza! Kazuia katani kuuzwa nje imebidi yale mashamba katani yote ichimbuliwe labda wanataka kuotesha mazao mengine.
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,350
2,000
Katani ya Tanga aliyeua hilo zao ndiye huyo huyo unayemuita aje kulikuza! Kazuia katani kuuzwa nje imebidi yale mashamba katani yote ichimbuliwe labda wanataka kuotesha mazao mengine.

Itakuwa kheri sana kama kutaoteshwa zao lingine, lakini mashamba yagawiwe, ekari 10 kila mtu, aliyeuwa zao la katani ni nyerere. Nimekulia muheza, na miaka ya 70 nilikuwa nasoma primary school , so I know what really happened
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,350
2,000
Takataka ambayo imeua mbaazi na korosho kwa mkono wake ndio ije ifufue Katani ?!!

Wabongo kwa kuishi kwa matumaini koko hamjambo aiseeee.

Miaka 5 yote kashindwa kufufua hata Kahawa tu ndio ataweza katani
Mkaruka wacha kukurupuka, soma mada vizuri, hatutaki ufufuaji wa zao la katani, bala twataka ardhi igawiwe, tutalima maharagwe, mahindi, nyanya, mboga na mazao ya kuwauzia Watanzania na nchi jirani ya Kenya.
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,154
2,000
Tanga hata asipofanya lolote anashinda. Tanga ni wateja wa CCM kwa miaka halafu hakuna cha maana kinachofanyika. Shamba la bibi
 

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,333
2,000
Walishagawana mashamba na kuuza viwanja-mfano Pongwe City ni shamba lililokua Amboni Estate, leo hii majumba yanamea!!

Hati za mashamba kama yale huwa hazifutwi na maafisa ardhi mkoa ama makamishina,nani aliruhusu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom