Mikakati ya hao wanaopanga kuandamana ili hatimaye wamuondoe ikulu rais Magufuli ni mibovu sana.
Huwezi kumlinganisha rais Magufuli na hao akina Mubarak au sijui Gadaffi. Majitu yaliyokaa kwenye madaraka miongo na miongo.
Rais Magufuli kachaguliwa kidemokrasia [hata kama wengine hawakukubaliana na matokeo].
Tena kachaguliwa kihalali.
Rais Magufuli hata miaka mitatu madarakani hajafukisha.
Sasa unapoandaa maandamano yenye lengo la kumpindua, jua hakuna kundi, taasisi, au yeyote yule mwenye akili timamu atakayekuunga mkono.
2020 siyo mbali kivile. Kwa nini usisubiri hadi wakati huo ili umtoe kupitia nguvu ya kura?
Okay, utasema kuwa labda CCM wataiba kura.
Sawa, kama wataiba kura kweli hapo ndipo itakuwa muda muafaka kabisa wa kuitisha maandamano nchi nzima na kupinga yaliyotokea kwenye uchaguzi.
Hapo hata jumuiya ya kimataifa itakuwa na nafasi nzuri ya kukuunga mkono.
Lakini hii ya kupiga makelele mtandaoni na kushindana kumtukana mtu aliyechaguliwa kihalali haitofanikiwa kamwe.
Itaanzania na kuishia mtandaoni tu.
Hivyo shime wote msiompenda Magufuli. Pangeni mikakati mizuri. Acheni kupayuka na kulialia mitandaoni na mjipange ili 2020 ikifika mnamrudisha Chato huyo msiyempenda.