Magufuli, nishati na madini ingekuaje?

Mamushka

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
1,595
99
Habari zenu wadau, Sijui kwanini natamani sana kuona wizara ya Nishati na Madini, angepewa John Magufuli hata kwa muda mchache tu.

Najiuliza sana sijui ingekuaje au angefanya nini, au ndo angeanza kwa kutimua maelfu ya watu,
au mpaka sasa umeume ungekua umesharudi ndani ya wiki moja, natamani kuona.

Kuna mtu mwenye wazo kama langu? sorry kama nimewakwaza.
 
Wakuu wanaogopa kumuweka hapo maana yule hana simile, atawaanika wooote! Na hapa ndio dhamira ya serikali inakuwa na mashaka maana haiingii akilini hata kidogo wizara nyeti kama ya Nishati na Madini inaongozwa na huyu joker Ngeleja na fresher Malima. Wawili hawa wana utaalam gani au creativity gani kwenye nishati na madini?

On the other hand wakimtoa Magufuli kwenye barabara bei ya ujenzi zita-shoot kama wakati wa Shukuru Kawambwa. Sasa hivi angalia samaki na ufugaji alikokuwa Magufuli, Dr Mathayo ni kama hayupo, makokoro yamerudi, shamba la bibi limechanua tena.

Nionavyo mimi siri ya mafinikio ya Magufuli sio tu kusimamia sheria bali pia kutuoogopa kuwambua 'wakubwa' hata kama ni CCM yenyewe na hapa ndio wanapata kigugumizi maana wengi wao wamewekeza kwenye nishati na madini.
 
Weeeeeeee!!!
usinichekeshe,
hawezi kupewa, hata mkiomba miungu yoteeeee!
We hio aibu watajificha wapi?

hizo zinaitwa ndoto za alinacha.
Fanya kazi
 
Habari zenu wadau, Sijui kwanini natamani sana kuona wizara ya Nishati na Madini, angepewa John Magufuli hata kwa muda mchache tu.

Najiuliza sana sijui ingekuaje au angefanya nini, au ndo angeanza kwa kutimua maelfu ya watu,
au mpaka sasa umeume ungekua umesharudi ndani ya wiki moja, natamani kuona.

Kuna mtu mwenye wazo kama langu? sorry kama nimewakwaza.
hawezi pekee, matatizo ya umeme yamenzia ikulu, unless makuguli awe rais
 
Wakuu wanaogopa kumuweka hapo maana yule hana simile, atawaanika wooote! Na hapa ndio dhamira ya serikali inakuwa na mashaka maana haiingii akilini hata kidogo wizara nyeti kama ya Nishati na Madini inaongozwa na huyu joker Ngeleja na fresher Malima. Wawili hawa wana utaalam gani au creativity gani kwenye nishati na madini?

On the other hand wakimtoa Magufuli kwenye barabara bei ya ujenzi zita-shoot kama wakati wa Shukuru Kawambwa. Sasa hivi angalia samaki na ufugaji alikokuwa Magufuli, Dr Mathayo ni kama hayupo, makokoro yamerudi, shamba la bibi limechanua tena.

Nionavyo mimi siri ya mafinikio ya Magufuli sio tu kusimamia sheria bali pia kutuoogopa kuwambua 'wakubwa' hata kama ni CCM yenyewe na hapa ndio wanapata kigugumizi maana wengi wao wamewekeza kwenye nishati na madini.

Mkuu ulichosema ni kweli tupu, kwasababu haiingii kichwani, kabisa wizara nyeti kama hiyo ipewe watu ambao bado hawaiwezi na bado lifumbiwe macho.
 
kwani huko aliko kishafanya nini hadi sasa? zaidi ya kumulikwa tu na kamera za wanahabari? alikopitia je, alifaya nini, mmesahau alichoifanyia tanzania na nyumba za serikali? kweli watanzania tunasahu kirahisi sana, hata haya ya ngereja na jairo tutasahau pia.

mi nionavyo huyo naye ni walewale, kama alishindwa kuzilinda nyumba za serikali na leo taifa litapata gharama za kutisha kuwaweka maafisa wa serikali mahotelini kwa ajili yake, hata huko naye atatafuta madili mapya na kutengeneza pesa tu kama wenzake, mi kwa kweli sioni utofauti wake na waheshimiwa wengine! samahani kwa nitakaowakwaza
 
Wanasema Maghufuli angalau anafanya maamuzi na kuyasimamia hata kama ni mabaya kama hili la nyumba za serikali! Lakini mbele ya JK Maghufuli hatafurukuta tena baada ya sakata lile la bomoabomoa.
 
kwani huko aliko kishafanya nini hadi sasa? zaidi ya kumulikwa tu na kamera za wanahabari? alikopitia je, alifaya nini, mmesahau alichoifanyia tanzania na nyumba za serikali? kweli watanzania tunasahu kirahisi sana, hata haya ya ngereja na jairo tutasahau pia.

mi nionavyo huyo naye ni walewale, kama alishindwa kuzilinda nyumba za serikali na leo taifa litapata gharama za kutisha kuwaweka maafisa wa serikali mahotelini kwa ajili yake, hata huko naye atatafuta madili mapya na kutengeneza pesa tu kama wenzake, mi kwa kweli sioni utofauti wake na waheshimiwa wengine! samahani kwa nitakaowakwaza

Kwa uelewa wangu, uuzwaji wa nyumba za serikali ilikuwa ni mpango mzima wa serikali na ulipitishwa na baraza la mawaziri. So whether Maguli alikuwepo au hakuwepo kwenye cabinet isingebadilisha chochote maana waziri anatakiwa asimamie yale yanayopitishwa na baraza la mawaziri. On the other hand ingekuwa vizuri kupata taarifa za bunge (hansard) ili kujua kama hili jambo la kuuza nyumba za serikali lilijadiliwa bungeni na nani alisema nini. Ni vizuri sasa tu-establish all the facts leading up kwa uuzwaji wa nyumba za serikali.
 
Naungana na mtoa hoja magufuri ni mtu pekee asie na woga katika kutekeleza maamuzi magumu na wizara hiyo ndio inamfaa kwa sasa
 
Angeongea kwenye TV na Radio kwa msisitizo akinukuu hata vifungu vya sheria kuhusu kuvunja mikataba kwa wawekezaji wanaokiuka taratibu zilizokubaliwa, tena angetoa takwimu za uzalishaji wao nk.

Lakini utekelezaji ungesubiri Rais aamue, na kama kawaida Rais angekaa kimnya au kuja na misemo ya Pwani kulizungumzia hili, au angeunda
tume na majibu ya tume yasingejulikana kamwe.
 
Tatizo la Wizara ya Nishati ni kutopewa kimbaumbele na Wizara ya Fedha. Mimi naona tatizo ni Mustafa Mkullo, wakimwondoa Mkullo na kumweka mtu mwenye upeo wa kuangalia matatizo ya taifa na kupanga vipaumbele sahihi nchi itaenda mbele kimaendeleo
 
Mkullo ni 'ultimate Security' ya Magogoni. Sioni akiondoka hapo langoni kabla ya 2015. Kwa umachinoo wake kamaliza akiba yote hazina na sasa wanakopa kwenye bank za ndani. Sasa hivi serikali ndio mkopaji mkuu kwenye mabenki yetu!
 
Huyu jamaa tungempa urais awachane live wazembe wasiokkuwa na aibu wala fikra za kufanya kazi kwa bidii.
 
Mkullo ni 'ultimate Security' ya Magogoni. Sioni akiondoka hapo langoni kabla ya 2015. Kwa umachinoo wake kamaliza akiba yote hazina na sasa wanakopa kwenye bank za ndani. Sasa hivi serikali ndio mkopaji mkuu kwenye mabenki yetu!

wakuu naomba anayeijua background ya mkullo aniambie manake hata hiyo bajet yake aliyosema ni ya kisomi zaidi nina uhakika kuna madudu aliyofanyaamdayo enzi zile nikiwa form five nisinge yafanya
 
Magufuli hana nguvu ya kubadili system nakubali, ila ni mfukunyuzi,
anafukua mambo yanakaa hadharani, ndio shida yake,
analeta aibu, watu wanakula kimya yeye anaweka hadharani,
sio kuwa atasafisha wakubwa ila ataweka hadharani ndio sababu hawamtaki.

Wote ndio hao hao tu, tofauti ni kuwa yeye hana rafiki wa kula nae,
pia akianza tu, waandishi wako nyuma yake hivyo hakuna siri
 
Back
Top Bottom