Madini yetu, kazi zetu

Apr 8, 2023
26
17
Doto Mashaka Biteko, mmoja wa wanasiasa vijana kabisa na ambao tangu kuingia katika siasa na katika serikali, wameonyesha siyo tu utendaji unaokwenda na wakati, bali pia uwezo wa kuzielewa wizara zao kiasi cha kuingia kwenye lile kundi waliofahamika miaka kadhaa huko awali kama “askari wa mwavuli” kunako Baraza la Mawaziri. Kundi hili walikuwamo Mawaziri kama Mh. Jakaya Kikwete wakati wa Rais Benjamin Mkapa, Mh. Nape Nnauye na Hayati John Pombe Magufuli wakati wa Rais Kikwete na Kapten George Mkuchika wakati wa Rais Mwinyi; na sasa (walau kwa maoni yangu), na sasa Dotto Biteko anatajwa katika kundi la “Askari wa Mwavuli” kwenye baraza la Rais Samiah (likihusisha pia mawaziri kama Hussein Bashe, Mwigulu Nchemba, Juma Hamid Aweso na wengine kadhaa).

Tangu kuaminiwa kushika Wizara ya Madini, madini yamekuwa sehemu muhimu ya uchumi kwenye sekta hii ukiwa juu ya 10% kwa kipindi chote. Sehemu kubwa ya ukuaji huu, inanaisibishwa na jinsi ambavyo Wizara imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni za msingi za Diplomasia ya Uchumi inayokumbatiwa sana na Awamu ya sita ya serikali.

Wasomaji wangu wanafahamu kwamba mimi humpinga ama kumuunga mkono mtu kwa msingi wa mantiki katika hoja zake, badala ya mtizamo wa makundi maslahi na hivyo ninaposema Dotto anafanya kazi nzuri kwenye eneo hili, nazingatia jinsi ambavyo miongozo yake kwa timu yake imekuwa ikitafsiri maono ya 4R’s za Mheshimiwa Rais kwa utawala wake. Kwenye eneo la Upatanishi (Reconciliation) kwa miaka mingi tulizoea migogoro kati ya Wananchi na migodi mikubwa ya madini (na wakati huo ikiwa michache tu ikiwamo GGM Geita, Bulanhulu Kahama, Buhemba Musoma na mingine midogomidogo), jambo ambalo kwa sasa limebakia kuwa historia. Hii ni matokeo ya pamoja na mambo mengine, juhudi za kuhakikisha kwamba sababu za kukinzana kati ya wananchi wanaozunguka migodi, na wachimbaji wadogowadogo inatatuliwa. Mapatano yaliyofikiwa yamesababisha utulivu katika sekta hii ambao haukushuhudiwa kwa miaka mingi huko nyuma.

Mageuzi (Reform) siyo tu ya kimfumo, lakini pia ya kimtizamo kuhusu madini na biashara ya madini kwa ujumla katika masoko ya kimataifa, yamesaidia sana katika kulinda na kutetea siyo tu namna madini yetu yanavyouzwa huko ulimwenguni, lakini pia kulinda hadhi ya taifa na nafasi yetu kwenye namna biashara hii inavyofanywa. Moja ya mambo watanzania wengi hawakuyafahamu hapo awali, ni ukweli kwamba kwa sababu ya utulivu wetu wa kisiasa na kijamii, thamani ya madini yatokayo hapa kwetu hayakutani na vikwazo kwenye soko la kimataifa; na hivyo baadhi ya mataifa na makampuni kutoka mataifa mengine, yanajaribu kutumia jina jema la Tanzania (“our good will) kufanya biashara kwa faida kubwa.

Hii ndiyo moja ya sababu kwanini mwaka jana kulipoibuka jaribio la kampuni ya Marekani kuuza madini yaliyodaiwa kutokea Tanzania kule Uarabuni na hata kusababisha hamaki, Mheshimiwa Biteko alijitokeza mbele ya kamati ya Bunge kujibu hoja hizi na kueleza msimamo wa Tanzania kwenye hili. Jinsi alivyolishughulikia jambo hili, ilisaidia siyo tu kulitatua bila kusababisha mgogoro wa Kidplomasia, lakini kuongeza uelewa na ufikiri mpana kwenye “siasa za biashara” za kimataifa. Hii ni sehemu ndogo tu ya mageuzi, lakini tungekwenda mbali na kusema juu ya kuboreshwa mfumo wa uchimbaji mdogo na hata biashara ya madini nchini na hivyo kupunguza kwa sehemu kubwa kasi ya utoroshaji madini. Ni kweli tatizo hasa la utoroshaji wa madini halijakoma kabisa, lakini walau Wizara ya madini imeonekana mar azote kuchutama kwa kusema inapogundua mianya na kisha kuchukua hatua kuiziba.

Hata hivyo, leo nizungumze kidogo kwenye eneo la kujenga upya mifumo ama “Rebuidling” hasa kwa kutafuta kuhusianisha juhudi za kuhakikisha uwekezaji kwenye madini unaendelea kufanywa kwa namna inayosaidia uchumi moja kwa moja, kwa kuongeza fursa za ajira nchini. Baadhi yetu ambao kimsingi ni mazao ya uwekezaji kwenye madini kwa kufanya kazi na kujifunza mengi kutokea kwenye sekta ya madini katika miaka hiyo ya awali kwenye uwekezaji ndani ya sekta hii, bado tunakumbuka changamoto kubwa mbili zilizokuwa zikikabili sekta kwenye eneo la Rasilimali watu.

Kwanza ni kile kilichokuja kufahamika baadaye kama “local content” kwenye uwekezaji wote kwa ujumla wake. Hoja zilikuwa mbili kubwa hapa; kwamba migodi hii mingi ilikuwa (na bado inao) watumishi waliokuwa wakiishi kambini (camp residents) na kwamba walikuwa hawa wakitumia mahitaji ya kawaida ya vyakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu, lakini makampuni yaliyokuwa na tenda ya kutoa huduma hizo yalikuwa pia ya kigeni na hivyo faida kubwa ilikuwa ikienda nje badala ya kubaki hapa ndani, na hata watumishi wengi walikuwa wa kutoka nje na hivyo kufanya kwamba ajira nyingi kwenda nje. Kampuni ya Kifaransa ya Sodexho kwa mfano ndiyo iliyokuwa na tenda ya kulisha migodi ya Buhemba, Nyamongo, Bulhanhulu na Tulawaka, jumla ya wafanyakazi wasiopungua 15 elfu kila siku, ikifanya pia usafi na huduma zingine.

Pili ilikuwa ni ajira za moja kwa moja na maslahi ya wazawa ukilinganisha na wageni waliokuwa wakifanya kazi za aina moja. Mgodi wa Bulyanhulu kwa mfano, koplo ama sajenti mstaafu kutoka Nepal (Ghurka) akilipwa mara 100 ya Kapteni au Meja mstaafu JWTZ huku Mnepali akiitwa Security specialist na kufanya majukumu yale yale na mara nyingine chini ya yale yaliyokuwa yakifanywa na walinzi wa kitanzania. Mpishi wa kutoka India alikuwa akilipwa mshahara mara kumi hadi 20 ya mshahara wa mpishi wa kitanzania wakati kazi kubwa ikifanywa na mtanzania , ilhali Nesi kutoka Afrika Kusini akilipwa mshahara mara 30 hadi hamsini ya mshahara wa Nesi mtanzania wakati viwango vya elimu, ujuzi ni sawa na huku Nesi Mtanzania akiwa na uzeofu na hali, tabia na hata mwitikio wa wagonjwa wa kitanzani ambao nesi wa kigeni hakuwa nao.

Ni kwa msingi huu, wakati tunaposhuhudia serikali ikitiliana saini na makampuni ya Australia kuwekeza kwenye kuchimba madini kwenye mikoa ya Songwe na Morogoro na kwingineko nchini, au tunaposikia Waziri wa Madini akiahidi kuwako kwa “signing ceremonies” za mikataba ya madini na ujenzi wa viwanda vya kuchenjua madini hapa kwetu, ni rain a ombi langu kwamba juhudi zilizoelekezwa kwenye kuzielewa, kuzitengenezea mifumo na kuendelea kuisimamia kuona kwamba changamoto za “biashara ya madini” inakwenda vizuri na kukua, ziwekezwe pia kwenye kuhakikisha tunatatua changamoto za local conent kwa faida ana ya watanzania wa sasa na wajao kufaidika na rasilimali za nchi yao.

Najua mnajua kwamba sina nijualo Nanga miye, nawaza tu kibanangabananga na hizi ni salaam tu nawasalimia. Wasalaam!
 
tunaposhuhudia serikali ikitiliana saini na makampuni ya Australia kuwekeza kwenye kuchimba madini kwenye mikoa ya Songwe na Morogoro na kwingineko nchini

juhudi zilizoelekezwa kwenye kuzielewa, kuzitengenezea mifumo na kuendelea kuisimamia kuona kwamba

kuchenjua madini hapa kwetu

ziwekezwe pia kwenye kuhakikisha tunatatua changamoto za local conent

kwa faida ana ya watanzania wa sasa na wajao kufaidika na rasilimali za nchi yao.
Naona kana kwamba tunasuasua na misimamo iliyothabiti! Hata 60/40? Tumeshindwa.

Nilitarajia kusikia mikataba yote mipya, hasa baada ya misukosuko iliyopita, kwamba inatuletea faida, tija na heshima. Badala yake tumekanyagwa tena. 16%?? Kweli? Ati unprecedented yaani siyo ya kawaida barani Afrika! Kana kwamba kujisifu hata kwa kile tulichokipata kuwa ni kiduchu!

Kuna kitu hakiko sawa kabisa, kuna kitu.

Sikutarajia kusema haya, lakini, Tanzania inakosa heshima. Makubaliano haya hayakupaswa kuwa na matokeo mabaya na kuelezwa kwa namna yalivyoelezwa kupendekeza hali ya ushindi!
 
Nchi gani wanalamba 60/40 ,huo ujuha mnautoa wapi kama hamjui muulize mtu achimbe akupe 40 nonsense

USSR
 
Ni kweli tumerudi kwenye mikataba ambayo tunapata % kidogo ukilinganisha na mahala tulikuwa tumefikia, lakini ikiwa hilo litafikiwa na kazi kuanza, ni vyema tusimamie kuona kwamba tunafaidika na hiyo % badala nayo kuwa kiini macho
 
Sielewi huo "ujuha" wako umetokea wapi. Ni dhahiri nimeandika as rhetoric [hata 60/40 tumeshindwa!]ila wewe umegeuza na kutaka kuaminisha ndicho nilichokuwa nakitaka. Wacha kupotosha.
...yaani kupuuza kabisa hoja yangu kuwa tunasuasua. I find that very disrespectful. Ukome......
 
Nauliza tu, Tumeshindwa nini kupata hizo $700million tuzitumie kuwaajiri hao "Wachimbaji" ? Manake, naamini pesa nyingi zitatumika kununilia mitambo, au kutumika kutengeneza mitambo(state of art) kwa ajili ya mradi/miradi hiyo... kwanini tusinunue mitambo hiyo tuwaajiri waje kuiendesha na wakati huo huo wakiwafundisha Watanzania kufanya hivyo? Sielewi
 
...yaani kupuuza kabisa hoja yangu kuwa tunasuasua. I find that very disrespectful. Ukome....

Nauliza tu, Tumeshindwa nini kupata hizo $700million tuzitumie kuwaajiri hao "Wachimbaji" ? Manake, naamini pesa nyingi zitatumika kununilia mitambo, au kutumika kutengeneza mitambo(state of art) kwa ajili ya mradi/miradi hiyo... kwanini tusinunue mitambo hiyo tuwaajiri waje kuiendesha na wakati huo huo wakiwafundisha Watanzania kufanya hivyo? Sielewi
Tungeweza na tunaweza, lakini (kwa maoni yangu) kuna mambo mawili. Kwanza we can't be kings of all jungles na hivyo Serikali inabaki kuwa Serikali na Biashara na Uwekezaji inabaki wa wawekezaji. Kama wanaweza kuleta mitambo yao, wakajenga, na wakaanza kuzalisha na kulipa Kodi na ajira na bado kuna 16% ya gawio, let them do the work.

Pili inawezekana katika Ile tamaduni yetu ya "kuheshimu mikataba ya kimataifa" tumeamua kwenda na Serikali haifanyi Biashara, inaachia sekta binafsi.

Hapa nadhani Watanzania tunahitaji kuona fursa na kufanya tafiti kisha kutafuta wawekezaji badala ya kusubiri wale ama wanaokuja wenyewe, au wanaoletwa na "Serikali".
 
Sielewi huo "ujuha" wako umetokea wapi. Ni dhahiri nimeandika as rhetoric [hata 60/40 tumeshindwa!]ila wewe umegeuza na kutaka kuaminisha ndicho nilichokuwa nakitaka. Wacha kupotosha.
...yaani kupuuza kabisa hoja yangu kuwa tunasuasua. I find that very disrespectful. Ukome......
Well, I can only be responsible for what I say, what you understand is completely up to you
 
Yaani madini ni maumivu tu kwa waafrika...sijui lini yatakuwa baraka..
 
Nadhani tutakapoamua kwamba sisi ni watu huru tunaitaka kujenga jamii huru. Tutakapoamua hasa kujenga jamii ya watu badala ya kujijenga wenyewe na familia zetu. Tutakapoacha kuwaua waonaji wetu kwa faida ya matumbo yetu na Wana wa wakoloni wa babu zetu.
 
Doto Mashaka Biteko, mmoja wa wanasiasa vijana kabisa na ambao tangu kuingia katika siasa na katika serikali, wameonyesha siyo tu utendaji unaokwenda na wakati, bali pia uwezo wa kuzielewa wizara zao kiasi cha kuingia kwenye lile kundi waliofahamika miaka kadhaa huko awali kama “askari wa mwavuli” kunako Baraza la Mawaziri. Kundi hili walikuwamo Mawaziri kama Mh. Jakaya Kikwete wakati wa Rais Benjamin Mkapa, Mh. Nape Nnauye na Hayati John Pombe Magufuli wakati wa Rais Kikwete na Kapten George Mkuchika wakati wa Rais Mwinyi; na sasa (walau kwa maoni yangu), na sasa Dotto Biteko anatajwa katika kundi la “Askari wa Mwavuli” kwenye baraza la Rais Samiah (likihusisha pia mawaziri kama Hussein Bashe, Mwigulu Nchemba, Juma Hamid Aweso na wengine kadhaa).

Tangu kuaminiwa kushika Wizara ya Madini, madini yamekuwa sehemu muhimu ya uchumi kwenye sekta hii ukiwa juu ya 10% kwa kipindi chote. Sehemu kubwa ya ukuaji huu, inanaisibishwa na jinsi ambavyo Wizara imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni za msingi za Diplomasia ya Uchumi inayokumbatiwa sana na Awamu ya sita ya serikali.

Wasomaji wangu wanafahamu kwamba mimi humpinga ama kumuunga mkono mtu kwa msingi wa mantiki katika hoja zake, badala ya mtizamo wa makundi maslahi na hivyo ninaposema Dotto anafanya kazi nzuri kwenye eneo hili, nazingatia jinsi ambavyo miongozo yake kwa timu yake imekuwa ikitafsiri maono ya 4R’s za Mheshimiwa Rais kwa utawala wake. Kwenye eneo la Upatanishi (Reconciliation) kwa miaka mingi tulizoea migogoro kati ya Wananchi na migodi mikubwa ya madini (na wakati huo ikiwa michache tu ikiwamo GGM Geita, Bulanhulu Kahama, Buhemba Musoma na mingine midogomidogo), jambo ambalo kwa sasa limebakia kuwa historia. Hii ni matokeo ya pamoja na mambo mengine, juhudi za kuhakikisha kwamba sababu za kukinzana kati ya wananchi wanaozunguka migodi, na wachimbaji wadogowadogo inatatuliwa. Mapatano yaliyofikiwa yamesababisha utulivu katika sekta hii ambao haukushuhudiwa kwa miaka mingi huko nyuma.

Mageuzi (Reform) siyo tu ya kimfumo, lakini pia ya kimtizamo kuhusu madini na biashara ya madini kwa ujumla katika masoko ya kimataifa, yamesaidia sana katika kulinda na kutetea siyo tu namna madini yetu yanavyouzwa huko ulimwenguni, lakini pia kulinda hadhi ya taifa na nafasi yetu kwenye namna biashara hii inavyofanywa. Moja ya mambo watanzania wengi hawakuyafahamu hapo awali, ni ukweli kwamba kwa sababu ya utulivu wetu wa kisiasa na kijamii, thamani ya madini yatokayo hapa kwetu hayakutani na vikwazo kwenye soko la kimataifa; na hivyo baadhi ya mataifa na makampuni kutoka mataifa mengine, yanajaribu kutumia jina jema la Tanzania (“our good will) kufanya biashara kwa faida kubwa.

Hii ndiyo moja ya sababu kwanini mwaka jana kulipoibuka jaribio la kampuni ya Marekani kuuza madini yaliyodaiwa kutokea Tanzania kule Uarabuni na hata kusababisha hamaki, Mheshimiwa Biteko alijitokeza mbele ya kamati ya Bunge kujibu hoja hizi na kueleza msimamo wa Tanzania kwenye hili. Jinsi alivyolishughulikia jambo hili, ilisaidia siyo tu kulitatua bila kusababisha mgogoro wa Kidplomasia, lakini kuongeza uelewa na ufikiri mpana kwenye “siasa za biashara” za kimataifa. Hii ni sehemu ndogo tu ya mageuzi, lakini tungekwenda mbali na kusema juu ya kuboreshwa mfumo wa uchimbaji mdogo na hata biashara ya madini nchini na hivyo kupunguza kwa sehemu kubwa kasi ya utoroshaji madini. Ni kweli tatizo hasa la utoroshaji wa madini halijakoma kabisa, lakini walau Wizara ya madini imeonekana mar azote kuchutama kwa kusema inapogundua mianya na kisha kuchukua hatua kuiziba.

Hata hivyo, leo nizungumze kidogo kwenye eneo la kujenga upya mifumo ama “Rebuidling” hasa kwa kutafuta kuhusianisha juhudi za kuhakikisha uwekezaji kwenye madini unaendelea kufanywa kwa namna inayosaidia uchumi moja kwa moja, kwa kuongeza fursa za ajira nchini. Baadhi yetu ambao kimsingi ni mazao ya uwekezaji kwenye madini kwa kufanya kazi na kujifunza mengi kutokea kwenye sekta ya madini katika miaka hiyo ya awali kwenye uwekezaji ndani ya sekta hii, bado tunakumbuka changamoto kubwa mbili zilizokuwa zikikabili sekta kwenye eneo la Rasilimali watu.

Kwanza ni kile kilichokuja kufahamika baadaye kama “local content” kwenye uwekezaji wote kwa ujumla wake. Hoja zilikuwa mbili kubwa hapa; kwamba migodi hii mingi ilikuwa (na bado inao) watumishi waliokuwa wakiishi kambini (camp residents) na kwamba walikuwa hawa wakitumia mahitaji ya kawaida ya vyakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu, lakini makampuni yaliyokuwa na tenda ya kutoa huduma hizo yalikuwa pia ya kigeni na hivyo faida kubwa ilikuwa ikienda nje badala ya kubaki hapa ndani, na hata watumishi wengi walikuwa wa kutoka nje na hivyo kufanya kwamba ajira nyingi kwenda nje. Kampuni ya Kifaransa ya Sodexho kwa mfano ndiyo iliyokuwa na tenda ya kulisha migodi ya Buhemba, Nyamongo, Bulhanhulu na Tulawaka, jumla ya wafanyakazi wasiopungua 15 elfu kila siku, ikifanya pia usafi na huduma zingine.

Pili ilikuwa ni ajira za moja kwa moja na maslahi ya wazawa ukilinganisha na wageni waliokuwa wakifanya kazi za aina moja. Mgodi wa Bulyanhulu kwa mfano, koplo ama sajenti mstaafu kutoka Nepal (Ghurka) akilipwa mara 100 ya Kapteni au Meja mstaafu JWTZ huku Mnepali akiitwa Security specialist na kufanya majukumu yale yale na mara nyingine chini ya yale yaliyokuwa yakifanywa na walinzi wa kitanzania. Mpishi wa kutoka India alikuwa akilipwa mshahara mara kumi hadi 20 ya mshahara wa mpishi wa kitanzania wakati kazi kubwa ikifanywa na mtanzania , ilhali Nesi kutoka Afrika Kusini akilipwa mshahara mara 30 hadi hamsini ya mshahara wa Nesi mtanzania wakati viwango vya elimu, ujuzi ni sawa na huku Nesi Mtanzania akiwa na uzeofu na hali, tabia na hata mwitikio wa wagonjwa wa kitanzani ambao nesi wa kigeni hakuwa nao.

Ni kwa msingi huu, wakati tunaposhuhudia serikali ikitiliana saini na makampuni ya Australia kuwekeza kwenye kuchimba madini kwenye mikoa ya Songwe na Morogoro na kwingineko nchini, au tunaposikia Waziri wa Madini akiahidi kuwako kwa “signing ceremonies” za mikataba ya madini na ujenzi wa viwanda vya kuchenjua madini hapa kwetu, ni rain a ombi langu kwamba juhudi zilizoelekezwa kwenye kuzielewa, kuzitengenezea mifumo na kuendelea kuisimamia kuona kwamba changamoto za “biashara ya madini” inakwenda vizuri na kukua, ziwekezwe pia kwenye kuhakikisha tunatatua changamoto za local conent kwa faida ana ya watanzania wa sasa na wajao kufaidika na rasilimali za nchi yao.

Najua mnajua kwamba sina nijualo Nanga miye, nawaza tu kibanangabananga na hizi ni salaam tu nawasalimia. Wasalaam!

sasa ndugu doto ndo umeamua kujiandikiela sifa kiasi hiki
 
Waziri wetu but hayo yote yanafanywa na wa chini yake ila sifa zinakwenda kwake big up
Na kwa Waziri/Kiongozi mzuri, anawajibika kuzipokea sifa hizi kwa niaba ya timu nzima na kuwatambua wote wanaosaidia na kuwasaidia pia wao kufikia maono yao. To pay it forward
 
Nchi gani wanalamba 60/40 ,huo ujuha mnautoa wapi kama hamjui muulize mtu achimbe akupe 40 nonsense

USSR
Educate him don't supress him kaka!Inatakiwa na sisi tuweze fedha zetu angalau iende 35%!

Hiyo 16% ya kupewa haina maslahi mapana kwa Taifa na uchumi wetu!
Tuweke fedha )mtaji na sisi!

All in all,Dotto amefanya vzr sana katika sekta hii,kaitoa mbali sana sana!

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
My sentiments exactly! Moja ya changamoto tunazo hapa kwetu, siyo kwamba hatuwezi kupata fedha within ourselves na kujenga refineries na kuchimba Madini yetu kwa faida, we are egocentric and selfish kiasi hatuwezi kuja pamoja tukaweka mitaji bila kutafuta kudhurumiana ama kutapeliana. We are too short sited lakini tunaweza sana kulalamika na hatutaki kuona those who do the best with the worst we hand them.
 
Mkuu haya material unayafahamu?
IMG_20230521_154444.jpg

IMG_20230521_154440.jpg
 
Back
Top Bottom