Magufuli must go: Salamu za mwaka mpya

Mithali:12.13, 17
Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.

Kila amtukanaye mkuu wa nchi hasira za Mwenyezi Mungu ziko juu ya anaye mtukana kwani Yeye ndio aliye mweka madarakani na mtukanaji au anaye jifanya msema ukweli kuliko Mungu hakika amelaaniwa na laana ya milele yeye na ukoo wake
 
I mean don't get me wrong, I like the guy.
He doesn't mince words, and everything is by the book.
But we are not happy, most of us normal citizens in general aren't happy.
Shouldn't the economy include us as well?
I don't care about the political harshness, all I want is to be happy.
We only live once, why should my 10 years under Magufuli be miserable?
10 years is a pretty long time.
In developed countries, the economy situation is shared with everyone because they know only people can improve or sustain it.
Watu wanasema watanzania ni wavivu lakini sio kweli.
Maeneo ya pwani na sehemu zenye shughuli za uvuvi watu huamka saa 9 mpaka saa 10 asubuhi kwenda kuvua samaki.
Hali kadhalika sehemu za kilimo watu huamka saa 10 asubuhi kwenda vibaruani.
Watu wavivu hawawezi kuamka mapema kiasi hiko.
Kuna tatizo la mfumo ambalo Magufuli hawezi kulitatua.
Kuna shughuli wanafanya watanzania wanalipwa chini ya sh 2000 kwa siku, mfano wasaidizi wa mama ntilie ( lakini waziri mhagama yupo tu wizarani na Magu hasemi kitu ). Hawa wanaolipwa chini ya elfu mbili wanafanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 3 usiku, hili Raisi halisemi na miaka mitatu imepita ( hawezi kulitatua). Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali watu.
Lakini pia kuna walioajiriwa sekta rasmi, kuna watu wanalipwa chini ya dollar za kimarekani 200 kwa mwezi ( tena wengi wakiwa ni watumishi wa umma). Huu ni mfumo mbaya wa uajiri na unadumaza uchumi wa watu.
Wenzetu walioendelea, watu wanaolipwa kidogo pia hufanya kazi kwa muda mfupi ili wapate nafasi ya kufanya vibarua vingine. Magufuli na waziri wako Mhagama hamjaliona hili na hamuwezi kulitatua ( walau mngeligusa ndani ya miaka mitatu iliopita ).
Tatizo ni mfumo na watendaji wa serikali, wanachama wote wa CCM ni victims wa mfumo hakuna haja ya kuwachukia. Magufuli huna uwezo wa kiakili kubadilisha mfumo. Watu wanasema hakuna ajira, akili za watu ni kwamba ajira rasmi zipo serikalini tu. Lakini mfumo ungekua mzuri, mashirika makubwa yangeipa changamoto dhana hii kwa kuajiri watu na kuwapa vyote ambavyo
waajiriwa wa serikali wanapata ( bima, mafao, job security n.k) huu nao ni mzigo ambao serikali ingetoa muongozo lakini utashi wa Magufuli sio mkubwa kiasi hiki. Fikiria kahawa inavyonyweka mida ya jioni kwenye vigenge, mtu mmoja anaweza kutengeneza brand yake akatengeza vigenge sehemu tofauti tofauti na kuajiri wasomi katika ofisi wapige hesabu, wagawe mishahara, waitangaze bidhaa nk . Lakini hili ndani ya mfumo huu haliwezekani, serikali inakusanya fedha nyingi na haizirudishi kwenye mzunguko kwa wakati.
Wakati wachina na nchi nyingine zinafanya ujenzi mkubwa ziliwaahidi wafanyakazi kazi wao milo mitatu kwa siku na fedha kidogo. Waliijenga wenyewe bila mtu hata mmoja kutoka nje. Na kipindi hicho ni zaidi ya miaka 60 iliopita ambapo kwao wasomi walikua wachache kuliko wajuvi. Sisi tuna wataalamu wengi wanahitimu masuala ya ujenzi lakini mradi tumewapa watu wa nje kwa kisingizio cha waje kutufundisha namna ya kufanya. Tungeweza kufanya
sisi wenyewe kwa wingi wetu na akili zetu, lakini mfumo tulionao hauamini wananchi wakawaida na Magufuli hawezi kuubadilisha. Jambo la ajabu ni kwamba mpaka barabara za ndani za tunatengenezewa na watu wa nje. Hatuwezi kukuza uchumi kwa mfumo huu, na Magufuli hawezi kuubadilisha. Magufuli, umejitahidi sana kusimamia huu mfumo lakini huu mfumo unatuumiza zaidi ya kutusaidia. Ununuaji wa ndege ungeendana na wananchi kuwa na furaha lakini hatuna furaha. Ndege ni jambo zuri na tulilichelewa. Kwanini tusiwe na furaha sasa? Kwanini tupoteze miaka mingine mitano ambayo ni mingi kwa umri wa binadamu wa sasa bila furaha kwa ajili yako? Tuachie tu nchi tutafute mwingine atakae nunua ndege na kutufanya tufurahi. Hakuna haja ya kulazimisha kufanya unavyojua wewe wakati maamuzi yako yana athiri watu wengi sana. Mfumo ni mbaya, wote sisi ni waathiriwa wa mfumo na Magufuli hana utashi wa kuubadilisha.
Kinachotia hofu ni kwamba, ukigombea tena kama binadamu tutakua tumeishi miaka zaidi ya 7 bila furaha.
Huna uwezo wa kiakili wa kubadili mfumo, tuachie nchi.

Heri ya Mwaka Mpya,
Hofu haijengi amani ya kudumu,
Nina haki ya kuishi kwa furaha,
Citizen Four.
Inaelekea huna taarifa rasmi, unachukua maneno mnayodanganyana huko mitandaoni ukidhani ndio uhalisia wa wananchi.. Labda ungesema ni wewe peke yako ndio huna furaha..

Kwa taarifa yako, ukitembea mitaani kwenye mikoa yote ukakutana na wamachinga watakwambia wanafuraha na wamefaidika na Magufuki.. Wapo wanachi waliofaidika na kwa kupatiwa haki za kwenye migogoro ya ardhi (Mh.Lukuvi anajitahidi), kwenye sekta ya afya, hata elimu. Unaongelea furaha ya wananchi kwenye eneo lipi?

Unapoongelea swala la miradi mikubwa kupewa wakandarasi wa nje, we ulitakaje? yupo mkandarasi Tanzania mwenye uzoefu wa kujenga barababra inayopita baharini? au ulitaka tuwape wakandarasi wajifunze kwenye miradi hii mikubwa? ingekua unatoa pesa mfukoni mwako ungefanya maamuzi kama hayo?

Hebu tuambie( kwa akili yako) nini suruhisho ya hizo changamoto ulizo ziainisha hapo kwenye andiko lako.
 
Mkuu;
Tatizo lako hujui hata mantiki ya ulichokiandika!

Nani alikuambia mpango wa maendeleo niwa Rais au unatolewa na Rais?

Kwa kukusaidia, Mpango wa Maendeleo unatolewa na serikali kwa kusomwa na Waziri wa Fedha na Mipango baada ya kujadiliwa kwenye vikao serikalini.
Si kweli thus kila rais aingie uja na ya kwake Kwa kuyaponda ya waliopita
 
No one but you is responsible for your happiness! Endeleza ujinga.
 
Huu Unaongea sasa ni uwendawazimu...
Kila amtukanaye mkuu wa nchi hasira za Mwenyezi Mungu ziko juu ya anaye mtukana kwani Yeye ndio aliye mweka madarakani na mtukanaji au anaye jifanya msema ukweli kuliko Mungu hakika amelaaniwa na laana ya milele yeye na ukoo wake
 
Andiko refu lakini pumba nyingi!

Kama unaona miaka 10 ni mingi kwako unaweza kuhamia katika nchi mojawapo kwenye EAC.

Hujui kama dunia kwa sasa ni kama kijiji? Hamia kijiji kingine.

Rais Magufuli is here to stay and also doing wonders.

And, right now Magufuli is the man.
Umeshindwa kuonyesha pumba kwenye andishi la mshikaji, badala yake umeleta vitisho [stali ya awamu ya 5]. Zipi pumba sasa?
 
Mkuu;
Tatizo lako hujui hata mantiki ya ulichokiandika!

Nani alikuambia mpango wa maendeleo niwa Rais au unatolewa na Rais?

Kwa kukusaidia, Mpango wa Maendeleo unatolewa na serikali kwa kusomwa na Waziri wa Fedha na Mipango baada ya kujadiliwa kwenye vikao serikalini.

...na haujadiliwi bungeni
 
Andiko refu maneno mengi, lakini mwisho ni kulalamika tu.
Ni nchi gani ambayo unaichukulia mfano Us au EU?
Kama magufuli alimtumbua mwanafanili mliyemtegemea sema wazi tukuelewe.
Halafu unasema wananchi, badala ya kujisemea wewe na wanaokutumia.

Sisi tulio wengi,.

MAGUTULI MUST STAY 2025,

Kadri mnavyomnanga ndiyo mnavyompaisha.
Amen.

Sasa mbona umerudia makosa ya mwandishi huyo?
Usiseme “sisi”
Sema “mimi”
 
Kila amtukanaye mkuu wa nchi hasira za Mwenyezi Mungu ziko juu ya anaye mtukana kwani Yeye ndio aliye mweka madarakani na mtukanaji au anaye jifanya msema ukweli kuliko Mungu hakika amelaaniwa na laana ya milele yeye na ukoo wake
Lubuva na Kikwete ndio Miungu yako?
 
Kila amtukanaye mkuu wa nchi hasira za Mwenyezi Mungu ziko juu ya anaye mtukana kwani Yeye ndio aliye mweka madarakani na mtukanaji au anaye jifanya msema ukweli kuliko Mungu hakika amelaaniwa na laana ya milele yeye na ukoo wake

Hizo laana za bei rahisi na mimi nazitaka jamani. Mnaposema ni chaguo la Mungu kwani Mungu alipigia kura kituo kipi? Au mnamaanisha Lubuva?
 
Eti doing wonders! Kipi cha ajabu anachokifanya? Kutoongeza mishahara? Matumizi ya fedha bila bunge kuridhia? Au kukwapua fedha za wafanyakazi na wastaafu? Akili za kuku
 
Inaelekea huna taarifa rasmi, unachukua maneno mnayodanganyana huko mitandaoni ukidhani ndio uhalisia wa wananchi.. Labda ungesema ni wewe peke yako ndio huna furaha..

Kwa taarifa yako, ukitembea mitaani kwenye mikoa yote ukakutana na wamachinga watakwambia wanafuraha na wamefaidika na Magufuki.. Wapo wanachi waliofaidika na kwa kupatiwa haki za kwenye migogoro ya ardhi (Mh.Lukuvi anajitahidi), kwenye sekta ya afya, hata elimu. Unaongelea furaha ya wananchi kwenye eneo lipi?

Unapoongelea swala la miradi mikubwa kupewa wakandarasi wa nje, we ulitakaje? yupo mkandarasi Tanzania mwenye uzoefu wa kujenga barababra inayopita baharini? au ulitaka tuwape wakandarasi wajifunze kwenye miradi hii mikubwa? ingekua unatoa pesa mfukoni mwako ungefanya maamuzi kama hayo?

Hebu tuambie( kwa akili yako) nini suruhisho ya hizo changamoto ulizo ziainisha hapo kwenye andiko lako.
= Suluhisho
 
Andiko refu lakini pumba nyingi!

Kama unaona miaka 10 ni mingi kwako unaweza kuhamia katika nchi mojawapo kwenye EAC.

Hujui kama dunia kwa sasa ni kama kijiji? Hamia kijiji kingine.

Rais Magufuli is here to stay and also doing wonders.

And, right now Magufuli is the man.
umesema dunia kijiji sawa. kila kijiji kina mjini kwake pale kwenye viduka .hujasema tanzania ipo sehemu gani ya hicho kijiji? mjini mwakijj au poein?
 
Wewe waweza kuwa na furaha Kwa sababu umo mulemule,, lakkini una furaha kuona Shangazi na mjomba hana furaha?
Maana hata PM Majaliwa hana furaha kuona Shangazi yake hana furaha Kwa kuogopa kipigo.
Mugabe alikuwa anashangiliwa hivi hivi na wanasema 95% lakini alipo ondolewa 95% walishangilia.
Hata sisi tuna unafiki huo. Jamaa must go
Hama nchi ndgu yangu wewe unaonekana ni mvivu wa kufanya kazi na umezoea vya kuletewa endelea wabunifu na wachapa kazi wanaona kawaida.
 
Kila amtukanaye mkuu wa nchi hasira za Mwenyezi Mungu ziko juu ya anaye mtukana kwani Yeye ndio aliye mweka madarakani na mtukanaji au anaye jifanya msema ukweli kuliko Mungu hakika amelaaniwa na laana ya milele yeye na ukoo wake
Yours isa wrong notion, huyu amewekwa na UWT, Polisi, na wana CCM wachache, usimsingizie Mungu. Hata
angekuwa Ni Mungu kamweka kwa sasa atakuwa Hana furaha naye kama alivyomchukia mfalme Sauli.
 
Back
Top Bottom