Simpendi Lowassa. Ila kwa sababu anasaidia kuibomowa CCM sawa tu.
Kama Rais hata mie ningelitamani awe Magufuli ill Bunge liwe la Chadema....au Ukawa.
Mkuu Sikonge mimi huwa nafatilia uzi zako, wewe ni mwelewa wa mambo mengi - ni kweli CCM kuna sehemu walikuwa wamejisahau sana, tatizo si CHAMA bali ni watu wachache tu ndani ya CHAMA na wanajulikana fika na sina shaka Mh.Magufuli anawajua sana na actually baadhi yao walikuwa wanampiga vita openly in other words bila aibu - ulevi wa madaraka na kutoambilika kwao ndio kunazua tafarani yote tunayo ishuhudia hivi sasa.
Mkuu Sikonge pamoja na mapungufu tajwa hapo juu yanayo husu chama tawala bado Mh.Magufuli anaweza kutumia ufagio wa chuma kuwaodoa/stafisha Miungu watu ndani ya CCM, wale ambao watapona zahama za Tingatinga wa come 2 their senses wajione wao ni binadamu kama wewe na mimi kazi yao ni kutumikia wananchi na sio kutangaza Ufalme wa kujali familia zao na ndugu zao - kila mtanzania mwenye kujituma aweze kusonga mbele bila ya kutegemea a right connection ngazi za juu, mambo haya yakujali vices hizo ndio yalichangia kwa kiasi kikubwa kuharibu ethics za Taifa letu na kuwafanya wananchi kukata tamaa.
Mkuu Sikonge na wenzako tafadhali mpe chance Mh.Magufuli uone atakavyo badirisha CHAMA na Serikali yake kwa ustawi wa Taifa letu, jamaa huyu ni moto wa kuotea mbali hana utani na mtu linapo kuja suala la uwajibikaji ulio tukuka, atawatia kashikashi kweli kweli, cha muhimu tumuombe Mungu amsaidie katika harakati zake za kusafisha Taifa letu, hawe tayari kufanya a U-TURN akae mbali na viongozi walio fanya CCM na Serikali yake kulalamikiwa na wapiga kura, akiendelea kuwakumbatia wapambe wanaojifanya wana uzoefu wa siku nyingi ndani ya CHAMA na Serikali basi akae akijua harakati zake zitawekewa spana, hasi underrate kikundi hicho wako highly organized kumu-contain kwa kasi ya ajabu.
Mkuu, Taifa la CHINA limepiga hatua kubwa in less than three decades kutokana na Viongozi wao kujirudi na kusafisha CHAMA na Serikali yake bila kujali wasifu,Cheo na connection ya waharifu ndani ya CHAMA na Serikali, walichukuliwa hatua kali wengine kunyongwa ndio maana wananchi walikubali kufanya kazi kwa bidiii na kuwajibika baada ya kushuhudia Serikali na CHAMA tawala kinawachukulia hatua kali Miungu watu ndani ya Serikali na CHAMA matokeo yake Taifa lao liko karibu neck 2 neck na UCHUMI wa Merikani, na sisi kama Taifa tuna wajibu wa ku-emulate Serikali ya Uchina.
Mkuu Sikonge sina shaka utakuwa unashangaa kwa nini nakazania kuipigia debe CCM pamoja na mapungu yake ya hapa na pale, jibu ni rahisi - sina Imani yoyote na UKAWA tangu wamvurumishe Mh.Slaa kwa kisingizio eti cha ku-speedup mabadiliko, hakuna anaye jiuliza mabadiliko kwa gharama gani? Mtu mnaye muweka kuongoza harakati zenu kuna waswali mengi kumuhusu kuliko majibu - kaingia pale kama a
mercenary kamanda aliye ongoza coup d'état hana interest ya kweli kwa CHADEMA na wanachama wake au UKAWA in general - hakuhusika na lolote katika kukuza CHADEMA wala kuleta demokrasia ya kweli katika Taifa letu - yeye yuko interested na kitu kimoja tu nacho ni:KITI cha Urais come rain or shine, kinacho nisikitisha Watanzania wenzangu hawataki kujiuliza maswali magumu kuhusu Mh.Lowassa ambaye alikuwa anahusaka Urais tangu miaka ya tisini mpaka leo bila mafanikio, je alikuwa anaonewa au ana matatizo ya kweli lakini baadhi ya Watanzania wamekwisha kata shauri kupuuzia matatizo ambayo yako wazi kabisa na hajawahi kuyakanusha kwenye majukwaa ya kampein, sana sana uyakwepa kuyajibu - WHY, one may ask? Sasa Mkuu Sikonge unafikiri vuguvungu hili la baadhi ya Watanzania kutaka madadiliko kwa gharama yoyote mradi CCM iondoke madarakani bila kujali wasifu wa kinara anayeongoza harakati hizo unafikiri kuna heri ndani YAKE?