Magufuli kuondoa 'Mawaziri vivuli' bungeni

Viva Magufuli, ondoa wote wapiga makelele, hawana jipya tofauti na kutumia vibaya raslimali zetu.
 
Atawakataza wabunge wa chama chake kuwa mawaziri vivuli?! Ndo kusema watamfuta machoz na uenyekiti wa chama!
 
You don't need to resort to English to be understood. Our national language is such a beautiful and self-sufficient language.

Sasa na wewe umefanya nini? Umeshindwaje kumshauri kwa kiswahili? Umemtumia mbu kutibu malaria.
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Asante Sana Super Brand Magufuli kwa mipango ya kuturudishia Tanzania yetu tunayoita....huku Kwetu 95% ya kura ni zako!! Kigoma unaendelea kufanya vizuri hadi sasa 85% Kura za Urais ni Zako!!

UKIWA wamepagawa nilikuwa Mwanza jana....jamaa wametaharuki wameanza michaka michaka ya usiku na kufanya uharifu barabarani...... #hapakazitu#
 
Magufuli ni moja ya marais ambao tutatamani (Tutatamani)aendelee na urais sababu ukimsikiliza ni mtu anayetaka kuweka HISTORIA Tanzania.

Big up Dr.
 
Kwangu mimi naona anataka kiifichia siri serikali imalize tembo wetu
mawaziri vivuli wanatoka upinzani na wamesaidia kufichua
madudu kwenye wizara husika ukiwaondoa ni sawa na kuondoa cctv cameras
kwenye migodi ya madini ukidhani unapunguza gharama.

Kama anataka kupunguza gharama afute wakuu wa mikoa na wilaya
pia apunguze majimbo ya ubunge yaliyoongezwa bila sababu za msingi
Na aondoe mwenge unaolitesa taifa kwa imani za kishirikina
huku tunasema tunaupinga ushirikina,wakati tunatumia fedha nyingi
kukimbiza mwenge,

Hata hivyo kama atatawala bunge litakuwa na asilimia kubwa
ya upinzani hivyo ajiandae kisaikolojia kukumbana na nguvu kubwa ya kupinga miswada
yote isiyo na mashiko.
 
Ataondoa vp na ccm ndo watakua wapinzani.!?
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Kweli uwezo wenu wa kufikiria ni Mdogo?Waziri analipwa posho gani tofauti na wabunge?Posho gani anayopewa Waziri?Waziri Kivuli analipwa posho ya nini?Tokea Lini rais akapeleka mswada bungeni?Daaa yaani ni Kazi kabisa , post very cheap
 
Maneno ya kahawa kwani magufuli si no CCM?..mfumo ni ule ule wa uongozi wa kurithishana na kubebana ....angalia ya celina kombani eti mtoto wake karithi ubunge..tabia ni ileile mwendo ni uleule..hakuna jipya kabisaaa maana hata magifuli huwa hajitambui
 
Hiyo ni sheria ya mabunge ya jumuia ya Madola
 
Sawa headgirl wa Masaki IT Centre kwa mawazo yako ya "Ki-Pre form one,usilolijuwa ni kwamba,nafasi hizo unazotamani zifutwe na Makomeo,hazikuwekwa kwa hisani ya Lumumba fc project fame,ni utaratibu wa mabunge yote ya nchi zilizo na mfumo wa vyama vingi.Lengo lake ni kuleta mawazo mbadala katika uendeshaji wa serikali.Hoja yako ni sawa na kusema Kamati za kuisimamia serikali zifutwe,jambo ambalo litalifanya bunge letu kuwa kinyume na mabunge mengine duniani hususan mabunge ya nchi za Jumuia ya Madola.

Kwavile wengine wanafanya basi nasisi tufuate. Hakika hizi ndo akili za kinyumbu za kufuata mkumbo sababu wengine wanafata...acha kukariri bwamdogo
 
Mkuu,hawezi kuondoa mawaziri vivuli. Ndio mfumo tulionao. Unafuata mfumo wa kibunge wa Uingereza. Anachoweza kufanya ni kupunguza baraza la mawaziri na kufanya mawaziri vivuli wawe wachache pia!
 
Mkuu hawa vijana hawajui kitu kabisa.
 
Magufuli ndio Rais ajae, hao wengine hawaeleweki hata sera hawana.
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Badala ya kuziba mianya ya rushwa na ufisadi ama kupunguza safari za Rais pamoja na seminar na makongamano unataka kuzuia mawazo "mbadala" bungeni.Nilikwisha sema JPM hatovumilia kupingwa ama kushauriwa.Namshangaa anataka kubadili Bagamoyo wakati Prof JMK ambapo ndio kwake ameshindwa.
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Hadithi.
 
Back
Top Bottom