Magufuli kuondoa 'Mawaziri vivuli' bungeni

Magufuli kuondoa 'Mawaziri vivuli' bungeni

Enzi za chama kimoja zimeshapitwa na wakati...
Huyo mzeee si ajabu akaondoa na sheria ya vyama vingi...!!
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Ndo maana tunasema mgombea wenu hana ufahamu wa mambo na ndo maana akilini mwake Saddam alikuwa Rais wa Libya na baadaye akawa Rais wa Kuwait(na hafahamu kuwa Libya na Kuwait hazijapata kuwa na Marais - Libya ilikuwa na 'Kiongozi' kama yule wa ACT hapa kwetu na Kuwait wana Mfalme)

Sasa ninachotaka kusema ni hiki - utaratibu wa kuwa na Shadow Ministers ni utaratibu wa mabunge yote yanayofuata taratibu za Westminster,sasa mgombea wacha awajaze huo ujinga mnaoushangilia halafu mtachekesha!
 
Hilo linawezekana kufuta waziri vivuli lakini haina maana ya wapinzani kutokuwa na wawakilishi wao wa wizara tofauti. Shadow ministers wapo nchi karibu zote ila kwa mfano ujerumani wao hawana waziri vivuli ila wana teams of experts ambao wanaikosoa na kusimamia masuala yote.

Nafikiri itakuwa ngumu au haitawezekana kabisa, nafikiri labda akate matumizi mengine kwa njia zingine.
 
Ndo maana tunasema mgombea wenu hana ufahamu wa mambo na ndo maana akilini mwake Saddam alikuwa Rais wa Libya na baadaye akawa Rais wa Kuwait(na hafahamu kuwa Libya na Kuwait hazijapata kuwa na Marais - Libya ilikuwa na 'Kiongozi' kama yule wa ACT hapa kwetu na Kuwait wana Mfalme)

Sasa ninachotaka kusema ni hiki - utaratibu wa kuwa na Shadow Ministers ni utaratibu wa mabunge yote yanayofuata taratibu za Westminster,sasa mgombea wacha awajaze huo ujinga mnaoushangilia halafu mtachekesha!

ndugu uko sawa kabisa kuna vitu vingine ni kuweka ushabiki pembeni kila kitu unachokiona chanzo ni katiba na katiba ina halalisha uwepo wa mawazili kivuli sasa najiuliza kwa katiba ipi atafuta mawazir vivuli uku rasimu ya warioba ilipigwa chini ambayo ilikuwa inalezea vizuri maswala hayo na kwa jinsi gani tutapunguza matumizi ya serikali ebu jiulize unatoa mawazili vivuli afu una wabunge zaid ya mia mbili ambao wanalipwa posho isipongua laki mbili kila siku pindi bunge linapokaa bado
 
Sawa headgirl wa Masaki IT Centre kwa mawazo yako ya "Ki-Pre form one,usilolijuwa ni kwamba,nafasi hizo unazotamani zifutwe na Makomeo,hazikuwekwa kwa hisani ya Lumumba fc project fame,ni utaratibu wa mabunge yote ya nchi zilizo na mfumo wa vyama vingi.Lengo lake ni kuleta mawazo mbadala katika uendeshaji wa serikali.Hoja yako ni sawa na kusema Kamati za kuisimamia serikali zifutwe,jambo ambalo litalifanya bunge letu kuwa kinyume na mabunge mengine duniani hususan mabunge ya nchi za Jumuia ya Madola.

usijisumbue, miaka hiyo jf was a of great thinkers, these are modern day great thinkers na bahati mbaya wengi wako ccm

kwa upande mmoja japo kiduchu twaweza walikuwa sahihi, the top cleam of ccm! the likes of Lusinde, hawa ndio gt wa ccm
 
Hivi hawa mleta mada na wanaosupport walienda shule juu ya elimu ya uraia au wanaigiza !
 
Hivi mnajua maana ya mawaziri vivuli nyie? Wanaigharimu nini serikali? Ama kweli Magufuli hajui siasa
 
Kama hii no kweli, nina wasiwasi na ufahamu na uwezo wa Magufuli kama Rais!!!!
 
Dr Magufuli katika mpango wake wa kupunguza matumizi ya Serikali yasiyokuwa ya Lazima, anatarajia kupunguza baraza la mawaziri, watakaokuwa wachache na wenye viwango stahiki.

Aidha pia anatarajia kupeleka mswada bungeni wa kuondoa mawaziri vivuli ili pia kupunguza gharama zisizo za lazima. Misamaha ya kodi kwa Wabunge nayo ni miongoni mwa marekebisho atakayoanza nayo Dr Magufuli.

Mimi sioni tatizo kwani nani hajui Makufuli ndiye katiba, sera na ilani?
 
Back
Top Bottom