Ndugu
Pasco, nashukuru kwa mchango wako, natambua umeshafanya maamuzi yako ya kumchagua Lowasa na Chadema, hongera kwa kufanya maamuzi. Binafsi sijafanya maamuzi sababu sikurupuki, sina chama, naendelea kuwapima wagombea wote kutokana na vigezo ambavyo nitavianisha hapo chini baadaye:
Sitegemei uanze na mihemko ya CCM out bila kupata vigezo nitakavyojirizisha navyo kwamba ninayemchagua anatosha kuniongoza kwa miaka mitano ijayo.
Lengo la kuanisha muda wa uanachama wangu humu JF ni kuonesha kutoyumbayumba na ushabiki maandazi wa vyama na misimamo kama wewe na wengineo mnavyofanya humu.
Vipimo vyangu;
- Usikivu ( Ntamchagua kiongozi anayesikiliza shida za watanzania, ushauri wa wataalamu na wanasheria)
- Maono(Vision)- Kiongozi anayeitazama Tanzania ya kimaendeleo kwa mikakati inayotekelezeka na ufahamu kwamba maendeleo ni hatua(steps) not an event.
- Afanyaje maamuzi inapobidi(decisiveness).
- Mtatua matatizo( problem solver)- sifa hii inashabihiiana na ya juu hapo.
-Mwaminifu(honesty)- Kiongozi ambaye nikimtazama najiridhisha na uaminifu wake bila shaka yeyote.
-Mbunifu( Creative)
-Mwenye ari na uchu wa kuwainua waTanzania, asiyependa uonevu.
Pamoja na sifa nyingine, hizi kwangu ni muhimu kwa kiongozi nitakayemchagua.
Nilitegemea wewe mwanaUkawa unielimishe kwanini nimchague mgombea wako kwa kutanabaisha mifano na hatua za mgombea wako na sio kunishambulia as if mimi ni mwanaCCM.
Yapo mengi yaliyonivutia Ukawa ilipoanzishwa( Umuhimu wa Katiba mpya), sasa imekuwa ya kina Sumaye, watu ambao mimi binafsi siwaamini; Nina haki ya kuhoji uhalali wake kwenye haya so called Mabadiliko.
Tatizo wana Ukawa hamshauriki kama mgombea wenu; sifa yangu ya kwanza hapo juu ni USIKIVU
Wiki njema ndugu