Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Magu mzee wa visasi sipati picha mitano ijayo,
kwa upinzan anaokutana nao kweny kampeni.
yy alitegemea kusifiw kwa kununua vindege na flyover zake ambazo hazijakmilik,
ingaw kwwny ahad zake hazikuwemo.
Hapiti safari hii maana 2015 hakushinda kihalali na lowassa akaamua kukaa kimya , Sasa huyu lissu sio wa kukaa kimya ..patachimbika
 
Mwanza pale kuna ziwa kuanzia kisesa Busekwa Nyansia uko maji hamna wanachota kwenye madimbwi ya mifugo

Imekaliwa na ccm
Nenda mkoa wa kagera Muleba
Wamezungukwa na ziwa
Hamna maji vijiji vyote kuanzia wilayan naomba ccm wawe wapinzan hawamu moja wajifunze na waache dharau
 
Kwa kauli hizo za kibaguzi nilitarajia TBC wakate mawasiliano na kisha tume imkemee.
 
ukifanya makosa kipindi hiki jimbo lenu mkachagua mbunge au diwani kutoka chama cha upinzani mfahamu imekula kwenu au kwa lugha rahisi mtasahau maendeleo.
hakuna kuremba mwaka huu. chagua tu ccm ili kujihakikishe maendeleo ya jimbo lako.
 
Mwanza pale kuna ziwa kuanzia kisesa Busekwa Nyansia uko maji hamna wanachota kwenye madimbwi ya mifugo

Imekaliwa na ccm
Nenda mkoa wa kagera Muleba
Wamezungukwa na ziwa
Hamna maji vijiji vyote kuanzia wilayan naomba ccm wawe wapinzan hawamu moja wajifunze na waache dharau
Hadi nansio ukerewe ni taabu tupu.
 
Umenena vyema. Kama kuwa Katibu Tarafa sio sawa na Ukurugenzi, sasa nikuulize, Makamu Mwenyekiti wa chama ambaye hajawahi kufanya kazi ya Makamu Mwenyekiti kwasababu alikuwa nje ya nchi, anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jiwe kaweza kuwa rais wa Tz,basi hata Matonya ombaomba anaweza kuwa rais wa Tz.
 
Jimbo la morogoro vijijini kuanzia ngerengere mpaka mkulazi mvua ikinyesha hakupitiki tena, mbunge na madiwani wote ni ccm tangu nchi hii ipate uhuru.
Wananchi ndio wanaoteseka na bado hawafanyi mabadiriko.🤔
Huwa wanawaahidi nini wananchi sasa hao wabunge na madiwani? Au ndio wameridhika na hiyo hali miaka yote hiyo?🤗
 
Mwanza pale kuna ziwa kuanzia kisesa Busekwa Nyansia uko maji hamna wanachota kwenye madimbwi ya mifugo

Imekaliwa na ccm
Nenda mkoa wa kagera Muleba
Wamezungukwa na ziwa
Hamna maji vijiji vyote kuanzia wilayan naomba ccm wawe wapinzan hawamu moja wajifunze na waache dharau
Na leo JPM kapita Kisesa anawalazimisha wamchague.

Sasa mbona alikuwepo mbunge wa CCM na hawana maji ya bomba.?!
 
IMG_20200906_122005.jpg
IMG_20200906_142015.jpg
 
Wananchi ndio wanaoteseka na bado hawafanyi mabadiriko.🤔
Huwa wanawaahidi nini wananchi sasa hao wabunge na madiwani? Au ndio wameridhika na hiyo hali miaka yote hiyo?🤗
Yani tuna hatari si kidogo
 
Kama kuna mtu mwenye namba ya simu ya daktari wa akili, tafadhali wapatie wasaidizi wa bwana yule, maana zimeshamruka. Aibu hii haivumiliki. Kwa muendelezo hu kuna siku atakuja kufanya kituko kitakachokumbukwa milele. Kwa Sasa wenye hekima zao na ushawishi ndani ya chama wameamua kuchutama, na huo ndiyo uungwana. Mwacheni aendelee kuswampa mwenyewe akiwa mtupu wa akili, busara na hekima.
 
Akipita, basi watu asiowapenda atawashughulikia vibaya mno.

Wengi wataumia.
 
Halafu mu MSHAURI JPM AACHE KUTISHA WAPIGA KURA kwamba hatawafanyia maendeleo kwa vile wanachagua upinzani.
Kwani ana uhakika gani kwamba atashinda?

Mbona anazungumza Kama vile mshindi wa Urais keshapatikana (ambaye ni Yeye) na sasa anafanya kampeni kwa ajili ya wabunge na madiwani?
 
Wananchi ndio wanaoteseka na bado hawafanyi mabadiriko.🤔
Huwa wanawaahidi nini wananchi sasa hao wabunge na madiwani? Au ndio wameridhika na hiyo hali miaka yote hiyo?🤗
Tena wanateseka kweli kuna watu wamezaliwa huko hawajui barabara ya lami, umeme au maji ya bomba na ccm ndio mtawala wao.
 
We bwana mdogo ni kwamba baada ya kupewa ukurugenzi ndiyo imebainika kapwaya vibaya, mkurugenzi kila siku kwenda kukagua vyoo vya shule na zahanati, Kama unaampenda ndugu yako ni vyema umshahuri afanyie kazi mapungufu.
Wivu tu!
 
Salaam wana JF...

Jana tarehe 04.09.2020 nikiwa nimetulia sehemu nilibahatika kufungulia TBC1 na kukuta kampeni za Dkt. Magufuli akiwa mkoani Mara.

Muda wa alasiri, alikuwa Bunda, badae akapita na kusimama Kiabakari, ni eneo la mnada wilayani Butiama.
Leo najua atakuwa na mkutano Musoma mjini.

Mambo niliyoshangaa kwa Dkt. Magufuli:-

1. Aliwaambia wananchi wa Bunda kwamba hakuwafanyia maendeleo yoyote, kwa sababu wao walichagua upinzani.

-Akawauliza "nyinyi hamjiulizi mko karibu na Ziwa lakini hamna maji?"
-Akawauliza "hamuoni wenzenu Lamadi (mpakani mwa Bunda, jimbo Busega) wana taa za barabarani, nyie hamna?!"
- Akawaambia, hata barabara nimeendeleza zinazowazunguka hapa nikawaruka.

Mwisho akaishia kuwaambia mnichagulie mbunge wa CCM, na madiwani wa CCM.

Nilishangaa hakueleza zaidi atawafanyia nn, ila aliwaahidi kuwa mkinichagulia mbunge wa CCM nitakuja kuwashukuru, na siku hiyo ndio ntakuja na mipango yote kuibadilisha Bunda.

Akawasisitiza wasichague maupinzani tena.

ETI HAWEZI KUACHA MTOTO WAKE, AKAMHUDUMIA WA JIRANI.

Nampa pole Dkt. Magufuli kwa haya na timu yake ya kampeni.

Inaelekea hajui vizuri watu wa Mara (hasa eneo la Bunda).

-Moja, sio watu wa kutishiwa vitu kabisa. Pole Dkt. Magufuli

Kwa hili, Bunda umepoteza.
Wale wamezoea kuishi na upinzani tangu Nyerere akiwa hai.

Unamtishia mwana Bunda (Mwikizu, Msizaki, Mzanaki, Mkurya, n.k) vitu?!!!! Eti ndio akuchague?

UME FAIL....

Hawakuchagui, watasema baki na taa zako za barabarani.

Wale ni kina LadyJaydee hawatishwi na hawapigi magoti.

Sijui huko usukumani labda wanapiga magoti.

- Mbili,
Ni uongo mkubwa kwamba Bunda haina maendeleo kisa kuwa upinzani.

Nikuulize leo upo Musoma mjini, ambayo ipo CCM awamu hii yako ya kwanza;

Mbona Musoma mjini imefubaa kuliko Bunda?, mji umepotea na biashara haziendi mpaka watu wameukimbia?! Mbona huko yupo mbunge wa CCM?

Haya BUTIAMA je?

Mbona siku zote wapo CCM. Tena wanapitaga bila kupingwa. Mbona BUTIAMA imechoka sana.

- BUTIAMA haina maji, lakini ipo CCM.
Mbunge CCM, Madiwani CCM.

- BUTIAMA kampuni yako ya Mayanga imeshindwa kujenga Barabara ya Butiama - Serengeti, na hela walilipwa, Mradi wa kumalizika 2015, mpaka leo umekufa.

Mbunge CCM, Madiwani CCM.

- BUTIAMA haina hospital ya maana, Haina sekondari ya maana, Haina soko la maana.

Mbunge CCM, Madiwani CCM.

ACHA HADAA, HAKUNA CHA CCM.

-HALAFU UNAJIITA KABISA RAIS WA MAENEO YA CCM TU.!!

2. AKIWA KIABAKARI.
Akiwa hapa alisema tatizo kubwa la Jimbo la BUTIAMA, ni ukabila.

Aisee you're very WRONG.

Butiama haina ukabila kabisa.
Ndio maana hata ulivyosema hivyo niliona kila mtu ananyamaza.

Sijui ulimaanishi nini. Ila umedanganywa pakubwa, matatizo ya BUTIAMA ni mengine kabisa.

Nakuhurumia sana.

Halafu mu MSHAURI JPM AACHE KUTISHA WAPIGA KURA kwamba hatawafanyia maendeleo kwa vile wanachagua upinzani.

Ni uongo mkubwa...

Haya ni majimbo ambayo yapo CCM, lakini ni maskini vibaya sana..

1. BUTIAMA
2. BUKOMBE
3. BUSEGA
4. MANYONI
5. MUSOMA VIJIJINI
6. KIBITI
7. RUFIJI
8. MKURANGA
9. MVOMERO
10. UKONGA
11. KAKONKO
12. MAGU
13. IRAMBA
14. MAKETE
15. NEWALA
16. MTAMA
17. KIVUU
18. SUMBAWANGA
19. NZEGA KASKAZINI
20. NZEGA KUSINI
21. SENGEREMA
22. CHATO
23. LONGIDO
24...........

Mwana JF...

Taja MAJIMBO mengine yaliyopo CCM lakini ni maskini vibaya mno...

Comment hapa Chini.....
Kilosa
 
Back
Top Bottom