Nimeshuudia kwa macho yangu mtu akiuza gari yake aliyotumia kuchukulia vidosho wetu. Gari anauza milioni 3 ist alianza na milioni 6, na bado hajapata mteja.
Siku hizi haipiti siku bila kupigwa mzinga, tena watu wanaomba elfu kumi kumi.
Nimeshangaa masista duu ukikaa nao, story zimebadirika na wao wanawaza kutafuta mashamba ya kulima. Yale mambo ya laki si pesa siyasikii siku hizi.
Nilienda Copa cabana Tabata imefungwa.. Billcanas hakuna watu.. Pub zote bia ya ukawa ndio habari ya mjini.. TBL wamepunguza bei ya vinywaji. Mapedeshee wamepotea viwanjani.
Marafiki tuliopoteana wameanza kurudisha mawasiliano, story zao kubwa ni ugumu wa maisha na wanaomba michongo.
Nashuudia mengi awamu hii mtaani..
Vipi kuna yoyote mwenye ushuuda tushee wanajamvi?