Serikali imekuumbuaJamani mwenye buku tano anisaidie
Kuna Salon niliingiaa baada ya watu kupotea wanadai wamama wamesafiri .Sikukuu ya Idd ya kuchinja Mabucha yamejaa nyama mpaka Usiku haijawai tokea...nilikaa sehemu ya Pub moja wkend..meza nyingi maji na Soda.Nikikaa mahali ni Malalamiko si njiani kazi kwenye Bajaji kwenye mwendo kasi daladala ukienda sheli kujaza mafuta Dukani Sokoni majumbani. Nimeongea mpaka na Wauza Karanga za kutembeza wanadai Zamani ilikuwa Dharau.'We kijana toka hapa na Karanga zako Chafu Eti leo vp una za Kuonjaa.(Hali Inatishaaa)
Sasa na ww mfanyakazi mwenye mshahara kimebadilika nini, mshahara umeshushwa au kuna mwezi hujalipwa?Hatari sana ofisini kwangu kwa kuwa wanajua sijaoa (sina majukumu) basi hawaishi kunikopa leo tuu kuna mmoja kanitoa buku tano.Tatizo watu tukisema hali tete nchini wanaleta siasa.
Na huko mtaani kwenu makabwela tu msisingizie serikali. Yaani mtu mwenye "ist" anasumbua mtaa nyie wengine mkoje?Nimeshuudia kwa macho yangu mtu akiuza gari yake aliyotumia kuchukulia vidosho wetu. Gari anauza milioni 3 ist alianza na milioni 6, na bado hajapata mteja.
Siku hizi haipiti siku bila kupigwa mzinga, tena watu wanaomba elfu kumi kumi.
Nimeshangaa masista duu ukikaa nao, story zimebadirika na wao wanawaza kutafuta mashamba ya kulima. Yale mambo ya laki si pesa siyasikii siku hizi.
Nilienda Copa cabana Tabata imefungwa.. Billcanas hakuna watu.. Pub zote bia ya ukawa ndio habari ya mjini.. TBL wamepunguza bei ya vinywaji. Mapedeshee wamepotea viwanjani.
Marafiki tuliopoteana wameanza kurudisha mawasiliano, story zao kubwa ni ugumu wa maisha na wanaomba michongo.
Nashuudia mengi awamu hii mtaani..
Vipi kuna yoyote mwenye ushuuda tushee wanajamvi?
sasa unajisifu kwa kuzoea shida?! Unajiona upo salamaCye masikini hali hii tumezoea tangu kitamboooo karibuni xnaa [HASHTAG]#thanks[/HASHTAG] again Magufuli
Amesema ofisini kwake.Sasa inabidi utafakari kwanza au urudie kusoma alichokiandika.Sasa na ww mfanyakazi mwenye mshahara kimebadilika nini, mshahara umeshushwa au kuna mwezi hujalipwa?
hahahahahaha....hatari ila watu hawatembei na hela nyingi siku hizi.ndo ukweli wenyewe leo kwenyewe nimesikia kwenye habari Prof Muhongo kapiga harambee kwa maafisa waliokuwepo naye huko Kagera na donation iliyopatikana ni elfu 40 tu