Nimeshuudia kwa macho yangu mtu akiuza gari yake aliyotumia kuchukulia vidosho wetu. Gari anauza milioni 3 ist alianza na milioni 6, na bado hajapata mteja.
Siku hizi haipiti siku bila kupigwa mzinga, tena watu wanaomba elfu kumi kumi.
Nimeshangaa masista duu ukikaa nao, story zimebadirika na wao wanawaza kutafuta mashamba ya kulima. Yale mambo ya laki si pesa siyasikii siku hizi.
Nilienda Copa cabana Tabata imefungwa.. Billcanas hakuna watu.. Pub zote bia ya ukawa ndio habari ya mjini.. TBL wamepunguza bei ya vinywaji. Mapedeshee wamepotea viwanjani.
Marafiki tuliopoteana wameanza kurudisha mawasiliano, story zao kubwa ni ugumu wa maisha na wanaomba michongo.
Nashuudia mengi awamu hii mtaani..
Vipi kuna yoyote mwenye ushuuda tushee wanajamvi?
mmh hiyo copa cabana mbona imeshafunguliwa sema tu haina watu kama zamani manake sikuhizi tabata imekuwa kama sinza pub zinafunguliwa kila siku na zinajaa balaa, kuna moja imefungiliwa pale kilimani baada ya kituo cha balakuda inatwa sijui the great inajaa balaa, ukija pale tabata sanene toroka uje pub ndo usiseme wkend hamna hata pakupaki gari, kuna nyingine pale bima sikumbuki jina lake usiseme, kweli maisha magumu ila watu bado wana stareheka kama kawa nazani bado wako kwenye denial