Magufuli effects: Ushuhuda wa hali iliyopo mtaani

Magufuli effects: Ushuhuda wa hali iliyopo mtaani

Kuna sistaduu mkali hapa kitaa mwanzoni alikuwa matawi ya juu saana ila kwa sasa yeye anazuga na happy bezidei yake kupata mkwanja...anasisitiza mchango kila baada ya dakika kadhaa anatuma sms mpaka unakereka.

Mbaya zaidi hata mkionana barabarani anakumbushia kwa mdomo...ni hatari!
 
Nimeshuudia kwa macho yangu mtu akiuza gari yake aliyotumia kuchukulia vidosho wetu. Gari anauza milioni 3 ist alianza na milioni 6, na bado hajapata mteja.

Siku hizi haipiti siku bila kupigwa mzinga, tena watu wanaomba elfu kumi kumi.

Nimeshangaa masista duu ukikaa nao, story zimebadirika na wao wanawaza kutafuta mashamba ya kulima. Yale mambo ya laki si pesa siyasikii siku hizi.

Nilienda Copa cabana Tabata imefungwa.. Billcanas hakuna watu.. Pub zote bia ya ukawa ndio habari ya mjini.. TBL wamepunguza bei ya vinywaji. Mapedeshee wamepotea viwanjani.

Marafiki tuliopoteana wameanza kurudisha mawasiliano, story zao kubwa ni ugumu wa maisha na wanaomba michongo.

Nashuudia mengi awamu hii mtaani..

Vipi kuna yoyote mwenye ushuuda tushee wanajamvi?
Copa Cabana imefungwa ila imefunguliwa pun nyingine matata mitaa hiyo hiyo, na watu wa tabata kama kawa wanakula bata.
 
Wakati wa campaign alisema serikalini kulikua kumejaa majizi na mafisadi,ina watu hao walikua wakitumia pesa ya umma km yao.Hata wagombea nyadhifa mbalimbali walikua wakitumia fedha kupata nyadhifa hizo kwakua walijua wakishazipata hela yao ingerudi manake enzi hizo serikalini ilikua ni kupiga hela tu.
 
Mhh,yaani sasa watu mmeanza kuona JF imekuwa na watoto
IST kwa 3m?weka picha hapa au ni Pm nimtume mtu akaiangalie nitampa 3.5m.Leo leo

Hapo chumvi kibaooo
Huu uzi ungeungwanishwa maana zipo kibao kama hizi,na kila mmoja kaja kwa style yake.
Subirini watu watoke bush waje mjini wapige hela huku nyie mnakariri maisha magum.

Huu ni ugonjwa ambao watu tumeishajitengenezea,na hali hii itatuathiri saana vijana,na hapo hapo wapo watu wanapiga hela na ukikaa nao wanakuambia maisha magum.

Kwangu mie naona kawaida tu,maana nimekulia kwenye kuhangika,nimeishaibiwa sana,tekwa,dhulumiwa
Sasa hii mipito ni ya kawaida sana tena sana tu,atahri kubwa inaonekana imekariri Dar,ila cha kushangaza sasa bado watu wa mkoani wanakuja wanapiga hela kwenye biashara na kurudi mkoa.

Na wengi wanakimbia kulipa madeni ya watu eti kisa Ukata,aisee watu wameishapata kichaka.
 
inawezekana kweli hali imekaba maana ata idadi ya wahudhuriaji kwenye mikutano ya Injili kwa sasa imezidi ku
panda chati
 
Jamani yani,,,,,tatizo sijui ni nini? lile nnalojua au ni mengine?
 
Kurasin watoto waliozoea upigaji wa bandarin wanatia huruma sijawahi kuona
 
Hatari sana ofisini kwangu kwa kuwa wanajua sijaoa (sina majukumu) basi hawaishi kunikopa leo tuu kuna mmoja kanitoa buku tano.Tatizo watu tukisema hali tete nchini wanaleta siasa.
Unafikiri tatizo ni nini? Hawapati mishahara hao wafanyakazi wenzio ama nini
 
Jamani nyie acheni, Kuna bar jirani hapa kubwa Tu, imekuwa Ni sehemu ya kuchezea watoto,mtaani pamepoa utafikiri tupo kijiji
 
Dah...mnarudia yaleyale tuu...karibuni kwenye ufalme wa HAKI......Ndiyo mjue kama mlikuwa mnaishi kwa HAKI au WIZI 😎
 
Mm nauza dawa ya kupunguza nguvu za kiume sikuizi wateja wanazidi kuwa wengi mana ya kuonge
 
Hali ni ngumu kwa kweli, tunaofanya kazi na kupokea mshahara tunalalamika sipati picha ambao hata ajira hawana hali zao zikoje

Subiri tarehe 1 octoba 2016 kuna mechi ya simba na yanga uone uwanja utakavyofurika ndio utajua usiyekuwa na hela ni wewe.Watu wanazo za kula hadi za kwenda kuangalia mechi na wengi wala sio wafanyakazi walioajiriwa wanatoka mitaani tena uswahilini
 
Mm nauza dawa ya kupunguza nguvu za kiume wateja wake wameongezeka tofauti na zakuongeza nguvu vp uongeze nguvu wakati hela ya kuonga madem una kwa anaye hitaji akiitumia hela zitajaa mifukoni mwake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom