Magufuli duniani Leo

Magufuli duniani Leo

Kwakweli alianza vizuri sana ukitilia maanani kwamba uadilifu ndio karata iliyomuibua kutoka kusikojulikana
Ila nadhani kuna watu wanamshauri vibaya kwamba anaweza tatua matatizo ya wananchi kutumia shortcuts za maneno ya kisiasa badala ya kuyatatua matatizo kama yalivyo
Kuna uwezekano vile vile hali ya kutoaminiana (wenye mikia na waliokatwa)na makundi ktk chama kumemfanya sasa ajenge usuhuba na watu ASIOFANANA NAO

Mengi yanakuja
Naomba kupinga hoja kwamba labda hana washauri wazuri. Sifa ya kwanza aliyonayo na inayomuangusha ni kwamba haamini katika ushauri wa wengine. Yeye kama alivyokuwa Idi Amini wanaamini kuwa wana akili, uwezo na uzalendo kuliko yeyote duniani. Pia pamoja na usadism aliokuwa nao , lakini kaudikteta kake kanalazimisha wote wanaomzunguka wamuambie maneno anayopenda kusikia. Sahau kuhusu ushauri
 
Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
Lipi ni jema,kuonekana huko nnje kuwa hafai au kufaa ndani kwa Watanzania?
 
Mwanzoni Rais wetu alipendwa sana na mpaka baadhi ya nchi zikatamani kumuazima akatawale kule kwa siku kadhaa au miezi kadhaa, hii ilileta picha kwamba ama Magufuli alikuwa anafanya vema mwanzoni au aliazna na vipaumbele ambavyo ni matataizo sugu ya nchi nyingi duniani mfano rushwa na uwajibikaji,

Tuwe wakweli Mpaka wapinzani wa hapo Tanzania akina mbowe na Lipumba walisema kwamba Magufuli anatekeleza ilani yao hafanyi ya kwake,

Zitto kabwe akafika hatua akasema sasa nchi ina rais kwa kweli,

Pale Kenya na nchi baadhi zilizoedesha uchaguzi baada ya Magufuli kuingia madarakani walitamani hata wale wanaenda kuwachagua wawe katika viatu vya Magufuli,

Pro Lumumba mpaka akaanzisha neno maarufu la Magufulification of Africa
Pale Autralia na Madagascar ilikuwa maandamano yakitaja kwamba tunataka kuwa na kiongozi kama Magufuli,

Ulaya walisema kuna kanchi kameibuka huko afrika kana Rais anaitwa Magufuli,

Magufuli Magufuli Magufuli aal over the world then

Je kuna jinsi alitafsiriwa vibaya mwanzoni baadae wakagundua kwamba siyo, au labda ameyafanya mazuri wakayazoea ikaonekana jambo la kawaida?
Au bado anakubalika kwa wale mnaotembea tembea huko?

BADO DUNIA INAMUONA MAGUFULI KAMA MWANZO? KAMA SIYO UNAHISI NINI KIMESHUSHA UMAARUFU HUO? NA JE ANGEFANYA NINI ILI ANEDLEEE KUAMINIKA KWA KILA MTU?
Hao wanaomuhitaji magufuri waambie tuwaazime japo mwezi mmoja waonje umaskini na kutafuta mlo wa siku moja
 
Mwanzoni na Mimi nilikuwa naye,in fact bado ana nafasi ya kuwa role model hasa kama ataruhusu Uhuru wa kujieleza na democracy kwa ujuma. Kiongozi lazima awe na ngozi ngumu,lazima akubali kukisolewa. Pale sasa ndiyo tutampa big up.
Wengi walisema hivyo hivyo kama wewe wakati Prime Minister Zedawi sasa angalia nchi yake inavyokwenda kwa kasi. Uhuru wa kujieleza wa matusi kama Mange mliyekua mnamshangilia ama wa kumtukana ndiyo demokrasia? Mnaiga wamatekani wale wenzetu wana miaka zaidi ya 300 kufika pale walipo. Mila na desturi tofauti Ulaya unaweza kumuita baba yako kwa jina lake na kumuita muongo ikawa sawa lakini hapa kwetu hiyo inaitwa ni utovu wa adabu.

Kill without mercy for the Sake of Mercy..... Huu ni msemo mzuri sana.
 
Mwanzoni Rais wetu alipendwa sana na mpaka baadhi ya nchi zikatamani kumuazima akatawale kule kwa siku kadhaa au miezi kadhaa, hii ilileta picha kwamba ama Magufuli alikuwa anafanya vema mwanzoni au aliazna na vipaumbele ambavyo ni matataizo sugu ya nchi nyingi duniani mfano rushwa na uwajibikaji,

Tuwe wakweli Mpaka wapinzani wa hapo Tanzania akina mbowe na Lipumba walisema kwamba Magufuli anatekeleza ilani yao hafanyi ya kwake,

Zitto kabwe akafika hatua akasema sasa nchi ina rais kwa kweli,

Pale Kenya na nchi baadhi zilizoedesha uchaguzi baada ya Magufuli kuingia madarakani walitamani hata wale wanaenda kuwachagua wawe katika viatu vya Magufuli,

Pro Lumumba mpaka akaanzisha neno maarufu la Magufulification of Africa
Pale Autralia na Madagascar ilikuwa maandamano yakitaja kwamba tunataka kuwa na kiongozi kama Magufuli,

Ulaya walisema kuna kanchi kameibuka huko afrika kana Rais anaitwa Magufuli,

Magufuli Magufuli Magufuli aal over the world then

Je kuna jinsi alitafsiriwa vibaya mwanzoni baadae wakagundua kwamba siyo, au labda ameyafanya mazuri wakayazoea ikaonekana jambo la kawaida?
Au bado anakubalika kwa wale mnaotembea tembea huko?

BADO DUNIA INAMUONA MAGUFULI KAMA MWANZO? KAMA SIYO UNAHISI NINI KIMESHUSHA UMAARUFU HUO? NA JE ANGEFANYA NINI ILI ANEDLEEE KUAMINIKA KWA KILA MTU?

Afrika bado wanamuona kama Mwanzo ila Ulaya na Marekani wanamuona mbaya kwani kawakazia.
 
Binafsi naamini Magufuli ni kiongozi mzuri sana tu ukilinganisha na waliomtangulia kuanzia Mwinyi

Tatizo lake kubwa ni kutotaka kukosolewa kunakopelekea ubabe na uonevu kwa wanaomkosoa

Angerekebisha hapo naamini angekuwa vizuri zaidi
 
Afrika bado wanamuona kama Mwanzo ila Ulaya na Marekani wanamuona mbaya kwani kawakazia.
Shida ya wenzetu hao maslahi yao kwanza
Na kwa Magufuli kawabania hawezi kuwa mzuri kwao hata siku moja
 
Kwenye demokrasia JPM ni ziro
unachekesha..hivi ni nani mfano wa kuigwa basi hapa.Tanzania ..kwa demokrasia..kwa sabab hata chama chenyewe kinachojiita cha demokrasia hakina demokrasia hata hiyo zero huipati..utapata demokrasia negative..
 
Naona kuna maccm yanakifananisha Chama Tawala cha ANC cha Afrika kusini na CCM. ANC wanauwezo wa kumng'oa Rais aliyeko madarakan endapo kama atakua ameshindwa kuongoza nchi vizuri, sasa maCCM yanaweza kufanya hivyo? Yani kama CCM ingekuwa kama ANC, leo JPM asingekuwa madarakan.
 
Kuna watu walidhani ni nguvu ya soda, hii ngoma iko vile vile hadi 2025, Magufuli ni yule yule juzi, jana, leo na hata...

Mimi nimeshauri hivi
P
P, ni kweli anabaki kuwa yeye kwani hakuna mwingine kwa wajihi na tabia zake Bali yeye!
Ila kwenye kazi has a za kiuongozi kuna mahali unatakiwa flexible na siyo rigid kama alivyo sasa!
Nikuulize, kwanini unaipenda hali take ya kuwa rigid na conservative? Kuna linalokunufaisha wewe zaidi au walio wengi? Kama lipo ni vyema ukashare nasi ili tumsalute! Na kama halipo LA kulinufaisha taifa basi mshauri awe anabadilika kulingana na mahitaji ya wakati!
 
Huko ulaya wala huitaji kufika si wanatoa taarifa zao tunasoma, Danmark na USA wamekata misaada sababu Magufuli ni Rais bora kabisa kabisa.
Hao tulikataa masharti yao ya ushoga na usagaji. Wengi Sasa wametuelewa na pia hatutembezi bakuli. Pesa ziko hapa hapa kwetu. Tunataka ushirikiano wa usawa siyo wa ubwana na utwana.
 
Ukiskiliza maneno ya mtandaoni unaweza kudhan watu wanamchukia Magufuli ila kumbe wananchi wanamkubali balaa.
Bahati mbaya wapiga kura wengi hawana muda wala account jamiiforums ila wanamkubali JPM.
Muwe na wakati mwema.
hao wengi ni akina nani kama si mm na ww tuliomo humu twitter, IG na kwingine... ndiyo hawahawa waTZ, usidanganyike ni aghalabu kukuta kijana wa sasa hatumii mitandao ya kijamii....
 
Wazungu ndio mafisadi wakuu waliotufukarisha kwa karne nyingi.
Kiongozi yeyote anayekwenda kinyume na matakwa yao hawatampenda tu.
Kwani lazima wampende Maghufuli?
Acheni maneno,chapeni kazi.
 
Binafsi naamini Magufuli ni kiongozi mzuri sana tu ukilinganisha na waliomtangulia kuanzia Mwinyi

Tatizo lake kubwa ni kutotaka kukosolewa kunakopelekea ubabe na uonevu kwa wanaomkosoa

Angerekebisha hapo naamini angekuwa vizuri zaidi
Kama hataki kukosolewa kama ulivyosema basi ni kiongozi mbaya sana kuwahi kutokea. Hawezi kuwa kiongozi mzuri kama hataki kukosolewa. Hii kwamba ni kiongozi mzuri kulinganisha na waliomtangulia mara nyingi hujengwa na fikra za udini na ukanda na ukabila tu uliojificha kwa ndani mbali sana huko.
 
Back
Top Bottom