Magufuli duniani Leo

Magufuli duniani Leo

#No one like JPM,

Kwa wote mnaojaribu kutuaminisha ujinga kaeni mkijua magufuli anapendwa sana na wanyonge wote Afrika.

juzi tu hapa tumetoka kushuhudia wazambia wakipagawa juu ya uwepo na kumshuhudia pale zambia.mpaka waziri mmoja akichanganyikiwa na kumpigia magoti.

Na kule kenya mpaka hata rais uhuru ameanza magufulification.

mambo ni hivyo dunia na afrika kwa ujumla wanamtambua kama rais mzalendo kwa bara la afrika.

mfano ni nchi za SADEC nk!

Wazungu hasa wamarekani na hao wa EU wanamuona mwiba,
wanamuona kama mtu anayetaka kuwashitua viongozi wengi barani afrika kuukataa unyonyaji wa raslimali za nchi zao.

Ukiongeza na jinsi alivyokataa kujipendekeza kwao tangu aingie madarakani,ni lazima wamtazame kwa jicho la tatu.
kwa hiyo nyinyi wapinzani wake wa ndani ya nchi,tunawajua ni kwa nini mnamchukia.

tuachieni bulldozer lifagie nchi.

viva JPM 2025
 
Visingizio. Uchafu wake unaonekana wazi.
Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
 
Dikteta mzalendo? Hata kwa makaburu SA, ubaguzi ulipakwa lipstick na kuitwa 'separate development' policy.
Mkuu The Retired, kwanza naomba kukiri ushallow kwenye reasoning. Nchi zote zilizopata maendeleo makubwa, maendeleo hayo yameletwa na viongozi madikiteta, angalia Tiger nations, no gain without pain.

Madikiteta wako wa aina nyingi, na Magufuli kweli ni dikiteta, hilo halina mjadala, ila huyu ni dikiteta mzalendo, anafanya udikiteta kwa nia njema na dhamira safi ya kulisaidia taifa.

Tanzania tulipofika, tulihitaji mtu kama Magufuli ili tuweze kusonga mbele.

P
 
Chakushangaza sasa kipindi chote hicho anasifiwa hukuleta uzi tujue
 
Mwanzoni Rais wetu alipendwa sana na mpaka baadhi ya nchi zikatamani kumuazima akatawale kule kwa siku kadhaa au miezi kadhaa, hii ilileta picha kwamba ama Magufuli alikuwa anafanya vema mwanzoni au aliazna na vipaumbele ambavyo ni matataizo sugu ya nchi nyingi duniani mfano rushwa na uwajibikaji,

Tuwe wakweli Mpaka wapinzani wa hapo Tanzania akina mbowe na Lipumba walisema kwamba Magufuli anatekeleza ilani yao hafanyi ya kwake,

Zitto kabwe akafika hatua akasema sasa nchi ina rais kwa kweli,

Pale Kenya na nchi baadhi zilizoedesha uchaguzi baada ya Magufuli kuingia madarakani walitamani hata wale wanaenda kuwachagua wawe katika viatu vya Magufuli,

Pro Lumumba mpaka akaanzisha neno maarufu la Magufulification of Africa
Pale Autralia na Madagascar ilikuwa maandamano yakitaja kwamba tunataka kuwa na kiongozi kama Magufuli,

Ulaya walisema kuna kanchi kameibuka huko afrika kana Rais anaitwa Magufuli,

Magufuli Magufuli Magufuli aal over the world then

Je kuna jinsi alitafsiriwa vibaya mwanzoni baadae wakagundua kwamba siyo, au labda ameyafanya mazuri wakayazoea ikaonekana jambo la kawaida?
Au bado anakubalika kwa wale mnaotembea tembea huko?

BADO DUNIA INAMUONA MAGUFULI KAMA MWANZO? KAMA SIYO UNAHISI NINI KIMESHUSHA UMAARUFU HUO? NA JE ANGEFANYA NINI ILI ANEDLEEE KUAMINIKA KWA KILA MTU?
Unategemea kabisa nchi za Ulaya na US zitoe sifa kwa rais mzuri wa Afrika? Rais mzuri ni kama akina Mobutu, wale wanaoruhusu makampuni kupitisha makinikia. Ukiona rais wa Afrika anapewa sifa, ujue hakuna rais hapo!
 
Hiyo ilikuwa "initial euphoria".

Kiswahili tynasema "nguvu ya soda".

Mtuhani wa uongozi ni kuweza kuwa na "strategic staying power".

Magufuli si strategic na hana staying power.

Ndiyo maana ukiacha the low hangubg fruit kujenga infrastructure, hakyna la maana analofanya consistently and strategically.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi walianza kushtuka baada ya Acacia kudaiwa kodi ya shilingi trilioni190! Isitoshe mambo yaliyowasisimua baadhi ya watu ni mambo mepesi tu kama kufagia barabara, kufuta sherehe za kitaifa, kufukuza watumishi kazi hadharani, kuzuia safari nje ya nchi, kuzuia mikutano, warsha, semina, nk.
 
Baada ya Matukio ya watu kutekwa na kupotea, Lissu kushambuliwa mchana kweupe, na watu kukatazwa hata kukamatwa kwa kumuombea dua Lissu Dunia sasa imepata picha halisi ya huyo unaye mtaja.
Urembo wa kuchonga haudumu
Hakika
 
Back
Top Bottom