Magufuli duniani Leo

hili laweza kuwa jibu pia
 
Amechemka kwenye 'angle' ya demokrasia na utawala bora. Angefaulu hapo,believe me Tanzania na Africa ingemuimba Magufuri forever
 
Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
Cyo kweli,ni utawala usio wa sheria ndiyo unamwangusha. Hayo mengine ni kutafuta pakujifichia tu.
 
Fatilia kipindi cha Dr Mumbi anavyotembelea miradi mikubwa kwenye youtube channel yake na angalia comments za watu wa mataifa mbalimbali wanavyo iongelea Tanzania na Rais Magufuli in a positive way
 
Shallow reasoning Mr. P, (nisamehe rafiki mwema, nimekosa neno rahisi la kuweka) huyu ni dictator, madictator huwa hawapoi! Tafuta historia ya dictators wote, huwa ni ukatili mwanzo mwisho mpaka anapinduliwa au anakufa madarakani! Kwenye demokrasia and therefore no dictatorship, sheria , katiba vitakupunguza kasi ya kutaka kufanya anayoyafanya ya kuvunja sheria na Katiba!
 
Mkuu The Retired, kwanza naomba kukiri ushallow kwenye reasoning. Nchi zote zilizopata maendeleo makubwa, maendeleo hayo yameletwa na viongozi madikiteta, angalia Tiger nations, no gain without pain.

Madikiteta wako wa aina nyingi, na Magufuli kweli ni dikiteta, hilo halina mjadala, ila huyu ni dikiteta mzalendo, anafanya udikiteta kwa nia njema na dhamira safi ya kulisaidia taifa.

Tanzania tulipofika, tulihitaji mtu kama Magufuli ili tuweze kusonga mbele.

P
 
Wewe jamaa sometimes ni boya hasa, maneno ya vijiwe vya kahawa unaamisha watu, yaani mataifa yaache kuwatamani kina Obama, Clinton na Angalau Kenyatta ,Rais mwingi wa hekima, wamtamani mtu katili asiye hata na hekima eti awaongoze, akaue uchumi wao kama alivyoua uchumi wetu.
 
Siyo maneno yangu, Alafu uboya unajua kuutambua?
 
Ni kweli nakumbuka hili bandiko
 
Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
Magufuli amefifia baada ya kuunda kundi lake la wasio julikana linalo teka, ua, poteza, piga risasi,............pia amefifia baada ya kuzuia wapinzani wasifanye siasa, kauli zake juu ya uzazi wa mpango, wanafunzi wanao pata mimba,.......
 
Tena baada ya kumaliza muda wake kikatiba aje mwingine wa mfano wake.

Nafikiri miaka 20 baada ya 2015 Tanzania itaendelea sana kiuchumi sababu ya udikteta wa Magufuli na misimamo yake dhidi ya rasilimali za taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…