Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,299
2,000
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais? Si tumwache tu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tu?

2. Je, hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources? Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa; je kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?

5. Kwani katiba ni nini? Si ni kipande tuu cha karatasi? Ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tu? Nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?

6. Na Katiba ni ya nani? Ni yetu? Na iko kwa manufaa ya nani? Si ipo kwa manufaa yetu? Hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli? Kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tu? Au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?

Hayo ni maswali tu nimeanza kujiuliza aloud.

Je, wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?

Paskali
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,085
2,000
Labda makada wa ccm ndio watakaolilia uchaguzi ili wamkomeshe Magufuli

Sisi tulioitaji uwajibikaji tunafurahishwa sana na JPM yaan kinachotokea ndicho tulichokipigia kilele siku nyingi.

Mungu mwongezee Magufuli ukali mara dufu.

Dili za makada zinabanwa. Hahah hah hah yaan ni raha sana

HUWA NASEMAHATA RWANDA HAWAJAKOSEA KUMWONGEZA KAGAME THIRD TERM think of kila primary skuli pupil anatumia komputa kujifundishia wakati hata UDSM komputa moja kwa wanafuzi 100
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,675
2,000
Safi sana naona umejisalimisha CCM nilidhani bado unazungusha mikono ukisubiri mabadiliko ya Lowassa.
Kuzungusha mkono wakati uswahili umeshaondolewa ikulu itakuwa ni ujinga! Wengi wanasema Kikwete kuondoka ikulu basi ni ushindi kwa watanzania wote
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
Pasco you are way over yourself my friend,
hilo haliwezekani na kwanza ni mapema mno kuona muelekeo wa utawala wa magufuli wazungu wanasema dont put all your eggs in one basket that it is way too much of bet to place on your fellow human being. kuna majipu ya mikataba ya madini, mafuta na gas hakiyaanza kuyatumbua hayo tutaanza kupata picha ya mueleko wake
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,678
2,000
Tulikuwa na Mr Clean kwa miaka 5 ya kwanza. Miaka 5 iliyofuata hata hatujui tusema alikuwa Mr nani
Tukawa na Ari mpya miaka 5 ya mwanzo, mwisho wa siku ndiyo haya ya makontena

Kama tunaweza kufanya analysis kwa kutumia siku 25 na ku project kwa miaka 5 tutakuwa na takwimu zetu duniani

Ngoja kamati kuu na NEC zikae kitako kuangalia jinsi anavyogusa 'maeneo' muhimu ya shughuli za watu

By the way, Nyani Ngabu kauliza intriguing question, tunahitaji uchaguzi kwa mwendo ulioonekana?
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom