Magufuli & CCM angalieni hapa, kisha mjilinganishe!

Magufuli & CCM angalieni hapa, kisha mjilinganishe!

Wakuu nilishasema magufuli ni longolongo nilitukanwa humu jamvin mpaka nikala ban sasa Nashukuru Mungu wenzangu mmefunguka
 
ninapo ona haya naikumbuka sana kauli ya THOMASI NYIMBO " hakuna chama kilicho leta uhuru kikaleta maendeleo pia, kazi ya TANU/ CCM ilikuwa kuleta uhuru tu baada ya hapo inapaswa chama kingine kilete maendeleo ya kweli "
 
tanzania hatuna malengo ya kuendeleza nchi kwa njia yeyote ile ila tuko kuendeleza vyama, familia na mambo yale ya kijinga jinga. maana hatuna malengo tunaongea sana bila vitendo, sisi tuambie majungu ndio utaamini tuko juu na starehe za ajabu ajabu
 
Mi sichangii kitu,nina hasira sana,naogopa ban,Mods kutunyima jukwaa huru la kujiachia na mitusi yetu mmetunyonga sana,Watu tuna hoja nzito ambazo uwasilishwaji wake haukamiliki bila kupachika mitusi angalau miwili mitatu ili ujumbe uwafikie walengwa ipasavyo. I'm passing with my grudges against those #j😉w¡! green & yellow
 
Hivi tulipopata uhuru tulikuwa maaikoni wa ngapi duniani. Maana sasa tumo katika masikini tatu bora duniani.
 
March. 30 2011
chaneasefastrain.jpg

India and China will help build a railway network across Ethiopia that would significantly improve the east African nation's transport system.
India has pledged $300 million for the national rail network construction while China's Export and Import ( EXIM )) Bank has inked a deal to finance 85 percent of the cost of a light rail network in the capital city of Addis Ababa at $490 million.
The cost of the rail network across the country has been estimated at $6 billion, according to an initial estimation.
"India has pledged to provide us with $300 million for the project as part of its assistance to the infrastructure development of African countries," Ethiopian Transport Minister Diriba **** told the Capital newspaper.
"We have asked India for another $300 million for the project," he said.
The rail network is part of the country's Growth and Transformation Plan that sets a target of construction of a 2,395-km national rail track.
The Addis Ababa track would be 36.5 km long.
Diriba told parliament every kilometre of the national track would cost $2-3 million. Based on this calculation, the average cost for a prioritised 1,808-km network would amount to around $4.5 billion.
The Addis Ababa rail network, supplemented by buses and taxis, would help in solving the ever-increasing transportation problems the city was facing, officials said.
China has also given four buses, whose manufacturing would be emulated locally as part of the government's plan to deploy 500 new buses in the capital.

Haya unaona sasa!? Wenzetu wanafanya kweli, sisi Watz akija mwekezaji au mfadhili akina Omar Chambo wanaanza kudai 10% kwanza hata kabla ya kuanza mradi wenyewe....nani anataka upuuzi huo? Wachina wamekuja wakatujengea jengo zuri la VIP kama starting point huku wakitaka kuendelea na viwanja vya ndege, wakapata disappointment kubwa toka kwa akina Chambo na wakaondoka mkuku bila hata ya kuaga!Sijuwi tumelogwa na nani?
 
ccm, hakuna cha mwakyembe wala magufuli, yaani walipokuwa wanaongea pale jangwani, nilikuwa natamani kupasua tv jinsi wanavyojisifia kutengeneza barabara ili chadema waandamane kwenye lami....

foleni kwa wale wanaotoka kimara wanaelewa jinsi mateso yalivyo, hadi imefikia wafanyakazi wanatamani kuhama dsm wakafanye mkoani ili kupunguza garama ya maisha na msongo wa akili kutokana na kuchoka kwanza na safari, foleni, kazi ofisini n.k....toka posta hadi ufike home hata hamu ya kukumbatia watoto wako huna..

hata ukiwa na gari wese linaishia kwenye foleni.....afu mtu anakuja kubwabwata tu hapo jangwani....hii ya ethiopia iko under construction, meres zenawi haongei sana kama ccm, yeye ananyamaza tu pamoja na kumtukana kwingi, anafanya kwa vitendo....zote hizo hapo juu wanajenga na karibia watamaliza....
Nadhani hawa viongozi wetu wazee (Magufuli na wengineo) uwezo wao kufikiri na kutenda umepungua sana, na wanaogopa challenge hivyo wanazugazuga wakisubiri muda wao wa kustaafu ufike.
 
CCM wako busy na mikutano ya kuishambulia CDM
Kweli kabisa. CCM walitakiwa wawajibu CHADEMA kwa vitendo kwa kuwapa huduma madhubuti wananchi, na sio kwenda kushambuliana kwa maneno kwenye majukwaa.
 
Ccm ya ukweli iliondoka na Nyerere hii iliypo ni magamba,wanafiki,wazandiki na mafisadi tu ya rasilimali zetu,waache tu waendelee na upuuzi wao wa kushindana na Cdm halafu cha kushangaza hv ma doctor na maprof walipanda pale jukwaaan jangwani akili zao waliziacha nyumbani au?Nape hata akiwaambia kateni viuno watafuata!!!!Someni alama za nyakati hakuna mtz mpumbavu tena maisha yametunyuka tuna hasira kinoma.
 
Mkuu wangu naona unacompare machungwa na maapple.

Nafikili si sahihi kufananisha nchi masikini na tajiri.

For your information:
According to World bank statistics,
1. Per capita income of Tanzania for 2011 was US$ 553, and the figure for Ethiopia for the same year was $ 360.
2. The per capita income for Tanzania for year 2010 was US$ 524, for Ethiopia was $358

GDP ya Ethiopia (Nominal) ni US $ 31.26 Billion kwa mwaka 2011, wakati ina wakazi 83 million, Tanzania GDP ya 2011 (nominal) ni US $ 23.33 Billion, wakati ina watu 42 million.

Who is richer and should be doing better?
 
MODS please tuanzishie jukwaa la matusi wengine tunataka kuondoa misongo ya mawazo maana hapa kuchangia kwangu ningeporomoka na matusi tu
 
Ahahahahaa! tunamtwisha kalai la zege mzee ccm apeleke ghorofa ya saba, na zege huwa hailali!
 
Tunaweza kufika pale Ethiopia ilipofika tutakapoamua kuachana na unafiki na tukafanyakazi tukiwa tunajilinganisha na best out there lakini sio kila tuliposhindwa tunatafuta mchawi. Ruksa aliposhindwa alianza kujitetea kuwa alikuta watu wanavaa magunia na kandambili na uchumi ukiwa sifuri. Hivi kweli kwa kiongozi makini na ambaye ulikuwa kwenye system unaweza kudiriki kusema hivi. Hivi uliangalia bench marking before pursuing any economic policy? Wewe unaondoa mising yote ya kiuchumi na kisiasa na ushindwa kuleta mbadala unafungulia pandora box, kodi hukusanyi, viwanda umegawa na waliogawiwa wanavigeuza kuwa warehouses halafu unajitetea kuwa ulikuta uchumi umeshuka. Na wananchi wakakubali kuwa brainswashed kwa fanciful goods zilizoanza kuruhusiwa. Na hiyo kasumba aliyoiacha ndio hii unatutafuna maana Watanzania ukiwauliza maendeleo nini watakwambia si unaona vitu vingi madukani? Zamani hatuna TVs sasa si unaona kila kona TV, Bia kila sehemu na mifano mingimingi midogo. Hakuna anayweza kukutajia miundo mbinu kama hiyo ya barabara, reli, mabwawa ya umume, vyuo vya teknolojia na mengine. Ndio ,maana hatujali hata raslimali zetu zinazoporwa kama madini, ardhi, mbuga za wanyama, mistu, fukwe za bahari na kadhalika maana hatuoni kuwa hizo zinatakiwa zitumiwe barabara kwa manufaa ya vizazi vya leo na kesho. Tunahitaji kubadilika ili tulinde mali zetu na tuhakikikshe zinatumiwa kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho. Tuache defence mechanism kama hiyo ya Ruksa ambaye alirithi nchi ina assets za hazina ya madini, wanyama, mistu, viwanda ahalafu anasema nilirithi uchumi zero.
 
Upembuzi yakinifu unaendelea!majibu rahisi rahisi
BONGOLALA nini kuendelea kwa upembuzi yakinifu, wakiulizwa wanadai "tumejipanga, tumeandaa mpango mkakati, tumetue tume kushughulikia suala hilo, tumejidhatiti..." na vijimajibu viiiiiiiiiiingi ili mradi kila kukicha wana msemo mpya wa kiswahili kuonyesha kuwa ni watendaji kumbe hakuna lolote porojo tupu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom