/.
Mkuu , labda niongelee kwa nafsi yangu kuwa nipo na nafuatilia mjadala kila nikipata fursa
Levictus alitaka kujua kama niliyoandika 2011 bado nasimama nayo. Nimemjibu bandiko 237 nikimujumuisha mpwa wangu
Judi wa Kishua
Nilisema hivi, tunahitaji nidhamu nchini na kwamba nidhamu inaanzia kwa mtu kwanza kabla ya kusambaa.
Nidhamu ni utartaibu unaofuatwa kwa kuzingatia taratibu.
Kuna tofauti ya nidhamu na woga. Ninasimama katika nidhamu kwani ndicho tunahitaji
Nikasema sote tunataka mapambano dhidi ya uovu na waouvu wanaoifasidi nchi
Nimerejea kwa hili kwasababu kuu moja.
Wapo wenzetu wanaoamini wale wanaosimamia nidhamu na mapambano ya ufisadi n.k.
Halafu wapo (nikiwemo) tunaoamini katika nidhamu na mapambano ya ufisadi kwa udhati, kwa nidhamu bila kupepesa macho, bila mahaba, bila kuonea au kuhurumia.
Nitoe mifano. Jana Rais alikuwa Unguja katika ziara inayosemwa ya kiserikali.
Wasoma risala walizungumzuia habari za CCM. Shughuli ilikuwa ya CCM kwa kila mantiki.
Sasa kama mikutano ya siasa imepigwa marufuku mbona huu wa ''ccm' umeruhusiwa?
Je, hapo kuna nidhamu ya kutekeleza yale yanayosemwa?
Wapo wapi wanaokemea maandamano na mikutano ya siasa?
Je, huo si uoga? Tofauti ya nidhamu na uoga ipo wapi?
La pili, tumesikia Rais akisema kitendo cha mtu fulani kukataa kutoa mkono kwa Rais wa Zanzibar asingeweza kusaini makaratasi ya mtu huyo kwenda kutibiwa.
Kwamba mzozo wa mambo yao binafsi unaingiaje katika haki zao kisheria
Aliyekataa kutoa mkono ana haki ya kufanya hivyo kama binadamu
Hakuna sheria ya nchi inayolazimisha wawili hao kupeana mikono kwa namna yoyote
Haki ya kutibiwa nje ni ya kisheria , si favor wala hisani.
Kama ni ku sign karatasi Rais wa ZNZ hana chaguo, ni wajibu wake kisheria na kikatiba
Ndivyo nidhamu inavyotaka, kwamba kuheshimu taratibu
Katika hali kama hii inawezekanaje kuwaambia wananchi kuhusu nidhamu ya kazi?
Hivi kuna karani gani atakayepeleka faili bila kuogopa kumuudhi Rais?
Je,atakuwa ametendewa haki? Je, karani atakuwa ametimiza wajibu wake kwa nidhamu?
Tunaposema kiongozi asimamie nidhamu tuna maana hiyo kuwa nidhamu kila eneo bila chuki , husda au upendeleo.
Ukiangalia Taifa kwanza, utaona sote tunazungumzia umuhimu wa nidhamu na mapambano ya ufisadi, ufujaji na wizi.
Ukiangalia kwa jicho la 'uchama' mahaba n.k. utaiona nidhamu kwa mtu, utaona mapambano ya ufisadi kwa mtu.
Utaweza ku trade nidhamu kwa woga. Utaufumbia macho ufisadi kwa kuuita ujasiriamali.
Nasimama na bandiko langu la 2011 kwa asilimia zote.