Magufuli atamba CCM haina mbadala

Magufuli atamba CCM haina mbadala

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,292
Rais John Magufuli amezindua Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere na kubainisha kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kutawala milele kwa kuwa hakina mbadala.

Akizungumza leo Jumatatu Julai 16, 2018 katika uzinduzi wa ujenzi wa chuo hicho Kibaha mkoani Pwani, kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema chuo hicho ni moja ya sababu ya CCM kuimarika kwa kuwa kitazalisha viongozi wazuri.

“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele, wanaohangaika watapata tabu siku zote. Chama hiki kipo na kitaendelea kuwepo na kitaendelea kuleta maendeleo kwa ajili ya Watanzania. Hakuna mbadala ni CCM hadi milele,” amesema.

“Wanachama wa CCM tembeeni kifua mbele tumeamua kuleta Tanzania mpya inayowapigania wananchi hasa wanyonge ili waweze kushiriki katika maendeleo.”
Rais Magufuli ameviomba vyama sita vya ukombozi kusini mwa Afrika vinavyoshirikiana kujenga chuo hicho, kufikiria kupanua wigo wa kuweka masomo mengine ya masuala ya maendeleo, badala ya kufundisha itikadi pekee.
Pia amevitaka kuwakaribisha wanachama wa vyama vingine wenye mrengo unaofanana na vyama hivyo, kujiunga na kujifunza kozi mbalimbali zitakazotolewa katika chuo hicho.
“Makatibu wa vyama hivi sita wahahakikishe wanakamilisha taratibu zote mapema ili majengo yakikamilika, mafunzo hayo yaweze kuanza mapema, pia mkandarasi akamilishe mapema na awashirikishe wananchi katika ujenzi huo ili nao waweze kunufaika,” amesema
Amebainisha kuwa chuo hicho kitasaidia kuzalisha viongozi wenye sifa wanaotambua itikadi, kwamba vyama vina misingi ya kiitikadi inayofanana.
Amesema uanzishwaji wa chuo hicho ni mwelekeo mwingine wa kushirikiana kwenye masuala ya kiuchumi na kisiasa, kwamba kitatoa mchango mkubwa katika mwelekeo huo.
Vyama vinavyomiliki chuo hicho ambavyo baadhi ya viongozi wake wamehudhuria uzinduzi huo ni ZANU-PF cha Zimbabwe, MPLA cha Angola, Frelimo (Msumbiji), MPLA (Angola), ANC (Afrika Kusini) na Swapo (Namibia).
 
Hahahaaaa hapo lazima waoM wakamtafute babu wa loliondo
 
Sasa ni wakati wa kutangaza Tanzania sio nchi ya vyama vingi bali ni nchi ya chama kimoja baaaaaasi. Hilo neno nchi ya kidemokrasia ifanyiwe amendimenti
 
Magu ni mwanasiasa na anaonhea kisiasa. Hivi kweli mlitarajia aseme ni siku gani ccm itaachia ngazi?!!!! Si angeonekana hamnazo
 
ukitaka kujua kwanini "U milele" angalia background ya "podium" neno "CER...…..I"
 
sasa huo mbadala utatoka wapi kwa aina hii ya upinzani isiyojielewa wala kuwa na hoja.
Kama wapinzani hawajielewi mbona CCM kinondoni mliwanyima mawakala wa ukawa viapo vyao kitendo kilichosababisha mkamuua Akwelina kwa risasi????
 
Back
Top Bottom