carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 204
- 431
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud amewasilisha taarifa za utendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji cha Chogo, Handeni, mkoani Tanga, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU).
Akiwasilisha taarifa hizo leo jijini Dodoma, Ayoub amesema NIDA imezalisha Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) 23,718,060 na vitambulisho 21,526,594, kati ya hivyo 21,515,793 vimesambazwa kwa wananchi.
Amesema mafanikio mengine ya NIDA ni kuunganisha taasisi 152 za umma na binafsi katika kanzidata yake, kutumia teknolojia ya Laser Engraving katika uzalishaji wa vitambulisho, pamoja na kuboresha moduli 24 za mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.
Kwa upande wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji cha Chogo, tangu mwaka 2016, chuo hicho kimeendesha kozi 57 zilizonufaisha maafisa na askari 5,934.
Kamati ya NUU imepongeza juhudi za NIDA katika kuboresha huduma zake kwa wananchi, huku ikiitaka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji cha Chogo kuendelea kuboresha miundombinu yake ili kuimarisha utoaji wa mafunzo na kuongeza ufanisi katika kukabiliana na majanga.
Chanzo : Azam tv