Magufuli apigilia msumari kwa mafisadi

Magufuli anakubalika na watu wote, hata wale waliokuwa wanaichukia CCM hivi sasa wanaikubali baada ya kufanya maamuzi magumu ya kumkataa fisadi nguli nchini na kumuweka mtu muadilifu na mchapakazi. Dr Magufuli amekuwa kivutio kwa watu wote na amebeba matumaini makubwa ya Watanzania

nyie ndio mnao muharibia..mwenzeni anamatangazo kibao anaomba kura mpaka kwa push up na unyenyekevu mkubwa
 
hiyo haipingiki makufuli ikulu yake....na wajiandae vizuri,hana mchezo katapila letu
 
Ndugu watanzania, tutumie nafasi hii inayokuja mara moja katika miaka 5 kutokomeza ufisadi. Hii ni nafasi muhimu sana. Tusipoitumia vizuri ndio unaweza kuwa mwisho wa hata hiki tulicho nacho - ambacho si haba.

Katika nafasi ya urais tumchague Dr Magufuli kwani ni msafi kuliko mpinzan wake mkuu Lowassa. Uadilifu ni suala la muhimu sana.

Tusitegemee hata siku moja mtu ambaye ana historia ya ufisadi katika utumishi wake wa miaka mingi ageuke ghafla uzeeni au katika umri mkubwa na kuwa mwadilifu. Mbwa mzee hafundishwi mbinu mpya. Atabaki vile vile.

Na mtu ambaye sio mwadilifu hawezi pambana na ufisadi. Hawezi kuwa anaiba peke yake na kuwazuia wengine wasiibe.

Kwamfano, Mobutu akiwa anapiga ufisadi Zaire aliwahi kuwaambia wasaidizi wake kuwa kama ni kuiba waibe kidogo kidogo sio kwa mkupuo.

Fisadi hafisidi peke yake.

Chukua hatua. Ipende Tanzania. Chagua Magufuli
 
mkuu tutokomeze na yale mafisadi yaliyouza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa na mchana kweupe. pia yalizigawia nyumba ndogo zake kama shamba la bibi.
 
Escro !!! Twiga kupanda ndege !!! na utuambie baada ya fisadi Lowasa kutoka ccm yamebaki mafisadi mangapi huko ccm ? usitutie ujinga wewe sisi tunajua cha kufanya hatuhitaji maelekezo yako
 
Ndugu watanzania, tutumie nafasi hii inayokuja mara moja katika miaka 5 kutokomeza ufisadi. Hii ni nafasi muhimu sana. Tusipoitumia vizuri ndio unaweza kuwa mwisho wa hata hiki tulicho nacho - ambacho si haba.

Katika nafasi ya urais tumchague Dr Magufuli kwani ni msafi kuliko mpinzan wake mkuu Lowassa. Uadilifu ni suala la muhimu sana.

Tusitegemee hata siku moja mtu ambaye ana historia ya ufisadi katika utumishi wake wa miaka mingi ageuke ghafla uzeeni au katika umri mkubwa na kuwa mwadilifu. Mbwa mzee hafundishwi mbinu mpya. Atabaki vile vile.

Na mtu ambaye sio mwadilifu hawezi pambana na ufisadi. Hawezi kuwa anaiba peke yake na kuwazuia wengine wasiibe.

Kwamfano, Mobutu akiwa anapiga ufisadi Zaire aliwahi kuwaambia wasaidizi wake kuwa kama ni kuiba waibe kidogo kidogo sio kwa mkupuo.

Fisadi hafisidi peke yake.

Chukua hatua. Ipende Tanzania. Chagua Magufuli

Usafi wa chama je,
Sisi tunaangalia usafi wa chama pia
 
Naona mafisadi na waliokosa uadilifu na waliozowea kuishi ccm kwa kupiga dili wanaendelea kukumbilia ukawa baada ya Magufuli kusema atawashughulikia....
Kwa taarifa yenu mtu wa kazi Magufuli ana mkono mpana na atawafuata huko huko mlikokimbilia ili mje kurudisha mali ya umma!

Nasikia wengine wanataka kutorokea nje ya nchi!!wapeni taarifa hata hukoMagufuli atawafikia tu.

#HAPAKAZITU
 
Magufuli nadhani unatambua chanzo kikubwa cha ufisadi na wanasiasa kuwa wafanya biashara nadhani na naamini mabadiliko ya kweli Kama kweli unania nayo hanabudi kunadi kurudisha azimio la arusha na chaku shangaza hata cc tunaoamini katika mabadiliko azimio limewekwa pembeni kwahiyo tutaendelea na mfumo unaozalisha mafisadi.........Mwisho ni ushauri wangu wa kweli mabadiliko yakweli ya kimfumo na kiutendaji ni kulirudisha azimio la arushaHakuna mabadiliko ya kweli bila ya kurudishwa kwa azimio la Arusha....
 
Au walau angeongea neno kuhusu katiba mpya ambayo pia ingebana kiasi hawa mafisadi. Lakini ataanzia wapi wakati chama chake ndio kimevuruga katiba ya wananchi? Chama chake ndicho kilichoua azimio la Arusha - ataanzia wapi kulirudisha? yote hayo ni kwenda kinyume na chama chake ndio maana naamini Magufuli pamoja na unafuu wake kwenye ufisadi hawezi kamwe kukibadilisha chama chake na mfumo wake wa kifisadi, zaidi chama kitamfanya awe fisadi zaidi.
 
Magufuli nadhani unatambua chanzo kikubwa cha ufisadi na wanasiasa kuwa wafanya biashara nadhani na naamini mabadiliko ya kweli Kama kweli unania nayo hanabudi kunadi kurudisha azimio la arusha na chaku shangaza hata cc tunaoamini katika mabadiliko azimio limewekwa pembeni kwahiyo tutaendelea na mfumo unaozalisha mafisadi.........Mwisho ni ushauri wangu wa kweli mabadiliko yakweli ya kimfumo na kiutendaji ni kulirudisha azimio la arushaHakuna mabadiliko ya kweli bila ya kurudishwa kwa azimio la Arusha..

Hawezi kufanya lolote hizo ni kilele za kwenye majukwaa tu.
hiyo nafasi ya kugombea urais kapewa na hao mafisadi....ataanzia wapi?
kina Ridh1 wanazindua huduma za kampuni ya Viatel 15/10/2015 wakati mwanzoni watanzania tulidanganywa kuwa ni wawekezaji ...KUMBE NI INVESTMENT YA BABA NA MWANA!
WATANZANIA TUAMKE!
NCHI IMEKUWA MALI YA FAMILIA YA JK?
DAWA NI KUIONDOA CCM MADARAKANI TU!
BURIHANI BABA WA TAIFA!
 
magufuli angekuwa anauwezo wa kupambana na rushwa angeanza na hii rushwa inayombea saiv kumuingiza madarakani.otherwise ni danganya toto, mafisadi nyangumi ndo yanapambana kumuingiza madarakani saiv, vip tena aje kuwageuka? hana uwezo huo.
 
Back
Top Bottom