Magufuli apigilia msumari kwa mafisadi

Magufuli apigilia msumari kwa mafisadi

Musoni unashabikia usichokijua mwulize Mwenyekiti wako kwani mafisadi hajuwapeleka mahakamani? Huwezi kumshtaki muhusika mwenza hata Huyo Magufuli hana uwezo
 
Asije akapelekwa yeye tu ,,,Mgombea wa Uraisi wa awamu ya Tano ya CCM atakaeshindwa vibaya sana ,na lazima ahojiwe kuhusu mauzo ya Nyumba na kama haitohi miradi yote ya barabara ichunguzwe maana barabara zimejengwa chini ya viwango na ni barabara zinazosababisha ajali kuliko barabara zozote zile barani Afrika huchangia kwa kiasi kikubwa maafa ya Watanzania ,gari zikipishana tu ajali ,umeona wapi kama si Tz pekee ! CCM hooi ?
 
Nikimbie jukwaa kwa sababu gani? Nilijiamini fisadi Lowasa akiwa CCM. Na sasa sina mashaka akiwa Upinzani. Ameshapigwa mapemaa ndo maana kila kona anahaha kusaka kura

Upeo wako wakufikiri unazidiwa hata na inzi,hiyo nguvu kubwa wanazotumia ccm kusaka kura huoni?.
 
Wadau, kwenye mikutano yote ya kampeni, mgombea Urais kwa tiketi ya CCM amesema kwa sauti kuwa hatakuwa na msamaha na mafisadi. Haya yametuibia na kufilisi nchi yetu. Ameahidi kupambana nayo kwa nguvu zote ambapk ameahidi kuanzisha mahakama maalum kwa ajili ya mafisadi na majizi.

Sasa Magufuli anakaribia kuapishwa kwani kwa jinsi hali ilivyo, ameshashinda uchaguzi. Sasa nawapa salamu kwa niaba yake hao mafisadi kujisalimisha ili washtakiwe na hizi mahakama zetu za kishkaji kwani mahakama ya Magufuli itakuwa ni balaa tupu.

Nasikia kuna mengine yamekimbia nchi. Ila Magufuli atayafuata huko huko yaliko. Kuna mengine yamehama chama kwa kudhani kuwa yakienda CHADEMA yatakuwa salama zaidi. Yanajidanganya

Ni upumbavu kukejeli Mahakama na taaluma za watu kwa "kufikiri" kuanzisha Mahakama nyingine!

Hakuna jipya kutoka CCM, Magufuli alisema hatawaangusha na atafanya yale aliyoyafanya JK! Na kama hukumbuki ndiye huyu huyu JK aliyewaomba "mafisadi" warudishe fedha vinginevyo atawataja! Seriously, Rais wa nchi!
 
kwa msimamo alioutoa katika mikutano yake yote ya kampeni, mh magufuli atawaweka pagumu na kuwaanikka mafisadi wote, nchi itashuudia fedha zilizoibiwa zikirudi kwa wanyonge. rai yangu kwa watanzania wote kuwatumpe mtumishi huyu ambaye ni wazi haogopi kujitoa kunufaisha umma wa watanzania kwa kuwajibisha wazenmbe na mafisadi wote.

haki ya nani , kura yangu kwa magufuli, kiboko ya mafisadi

Sasa si atabaki peke yake kwenye chama maana no! hata chama chake kitawajibishwa kwa ufisadi wake.
 
Wadau, kwenye mikutano yote ya kampeni, mgombea Urais kwa tiketi ya CCM amesema kwa sauti kuwa hatakuwa na msamaha na mafisadi. Haya yametuibia na kufilisi nchi yetu. Ameahidi kupambana nayo kwa nguvu zote ambapk ameahidi kuanzisha mahakama maalum kwa ajili ya mafisadi na majizi.

Sasa Magufuli anakaribia kuapishwa kwani kwa jinsi hali ilivyo, ameshashinda uchaguzi. Sasa nawapa salamu kwa niaba yake hao mafisadi kujisalimisha ili washtakiwe na hizi mahakama zetu za kishkaji kwani mahakama ya Magufuli itakuwa ni balaa tupu.

Nasikia kuna mengine yamekimbia nchi. Ila Magufuli atayafuata huko huko yaliko. Kuna mengine yamehama chama kwa kudhani kuwa yakienda CHADEMA yatakuwa salama zaidi. Yanajidanganya

Kwa nini Jakaya hakupambana na hao mafisadi hadi amwachie zigo Magufuli?
 
Ndugu zangu nawasalimu.

Kwenye Uzi huu nawaomba tuondoe ushabiki.

Napenda tujadili kwa Pamoja, nchi yetu imekumbwa na kashfa mbalimbali iwemo Richmond, Escrow na nyengine nyingi. Sasa swali ni Je, katika kashfa zote hizo, Magufuli alishawai kusikika popote ama Bungeni akikemea ufisadi huo? Kwenye kampeni zake amesikika akisema atapambana na rushwa, atajenga mahakama maalum ya kushughulikia mambo hayo, sasa ameahidi hili kwa moyo wake wote au ni kuwadanganya watanzania tu.

Tutafakari Pamoja
 
Ufisadi imekuwa kete ya kuingilia ikulu kwa ccm utadhani ufisadi huo ulifanywa na kanu au zanu -pf

kama mafisadi wangemkimbia magufuli (anavyojinadi) chama kingebaki viti tu hadi yeye angekimbia.
 
Wanakimbiza vivuli vyao wenyewe. Mie kwetu HARAMU KBS SAWA NA MUISLAM NA KAFRI!!!!
 
Magufuri amepambanaa na ufisad kwa vitendo kafukuza wabadhilifu weng sana katika kila sekta aliopita
 
Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali ambazo tumesoma na kusikia katika vyombo vya habari inaonekana na yeye ni FISADI wa kutisha.
 
Nafikiri kama angekuwa na uchungu na mafisadi asingethubutu kwenda kwa mh. Vijisenti nakumnadi kuwa huyu ndiye jembe lake! hii nafikiri ni danganya toto.
 
Ufisadi imekuwa kete ya kuingilia ikulu kwa ccm utadhani ufisadi huo ulifanywa na kanu au zanu -pf

kama mafisadi wangemkimbia magufuli (anavyojinadi) chama kingebaki viti tu hadi yeye angekimbia.

Ulifanywa na Lowassa, sasa yupo ukawa !
 
Back
Top Bottom