Yaani bilioni 16 za kujenga barabara zetu tunasubiri "Kuwait Fund" ila bilioni 60 za posho bungeni serikali inatoa, tena kiwango cha posho wanasema ni kidogo, kwa siku sabini!
Everything that is wrong with Africa. Mizee mizima na vitambi vyao inakuja EU kuomba hela, wakati wanaowaomba hela wanashindia sandwich kutwa nzima.
Yani maviongozi ya Afrika ni kama yamechuliwa.creativity sifuri, kwao achievement kubwa ni kuomba na kupewa. ukisikiliza bajeti ni msaada, mkopo, msaada, mkopo. hivi na familia zao ndio wanaziendesha hivi? ni lini kutakuwa na fiscal responsibility?
kwa nini maendeleo ya TZ yategemee hisani ya watu wa EU, Uarabuni na Asia? hivi nani aliwahi kutwambia wale watu hawana matatizo yao? hawa waingereza kesho kutwa wanapiga kura ya kujindoa EU, kwani wamechoka kugeuzwa financial beneficiaries,na wazungu wenzao.sasa jiulizeni, kama ndugu zao pua na mdogo, wanawakana, itakuwa sisi tuliopigwa jua la Ikweta karne kwenda, karne rudi?
Viongozi wa Tanzania, ni muda muafaka kubadili mentality zenu za uongozi, kuanziza hapo maendeleo ya dhati (trickel down economy) yataonekana. hii plastic economy mnayoitengeneza ina mwisho wake. Hakuna cha dezo duniani, watakuja kudai vyao siku moja. mjiandae kulipa.