Magufuli apangua hoja zote za Wabunge

Swali moja kajikanyaga lakini la pili ndio hajaligusa na ndio linamaana
Kua ktk Bajeti hii,ni kiasi gani kitakwenda kulipa madeni ya wakandarasina kipi kitabakia ilikimalize hizo kandarasi
 
Swali moja kajikanyaga lakini la pili ndio hajaligusa na ndio linamaana
Kua ktk Bajeti hii,ni kiasi gani kitakwenda kulipa madeni ya wakandarasina kipi kitabakia ilikimalize hizo kandarasi
Kulipa madeni ya wakandarasi si sawa na kulipa deni la sukari dukani. Ameeleza magufuli kuwa madeni ya wakandarasi hulipwa baada ya kuwasilisha certificate ya kazi iliyofanyika.
 
Hivi huyu Kiwanga ana akili timamu kweli? Yaani ni zaidi ya comedy
 
magufuli anapiga porojo anarukaruka anakwepa inshu

Magufuli ni mwongo sana. Kwa mara ya kwanza sasa wabunge wamegundua uongo wake, thats why anapata wakati mgumu kuipitisha bajeti yake. Ukweli ni kwamba serikali haina hela ya kuwalipa wakandarasi na wako hoi kabisa. Serikali imefilisika na Mkosamali yuko right.
 
Bahati mbaya wabunge hawana habari za kina kuhusu barabara hizi. Wakandarasi wamekopwa hela wamefilisika hadi wanajinyonga! Enzi za Mkapa wananchi hawakukopwa kiasi cha kufilisika! Ukitaka kufilisika ingia kwenye wizara ya magufuli!
 
Sasa hapo ndo kapangua nini? Pamoja na hiyo unayosema kapangua, bado kuna tatizo la foleni mjni Dar es Salaam. Tufikie mahali watanzania tuache ushabiki maana siasa haitatufikisha popote. Magufuli kuna mazuri anafanya. Ila Tatizo la nchi yetu huwa hatufikirii miaka mia moja (100) ijayo. Kwa mfano ni kwa nini kusiwe na mpango kabambe angalau miaka mia ijayo kwa mji wa Dar es Salaam ambao utahusisha usafiri wa train za umeme kwa maana ya underground, trum, na mabasi kama hayo ya DART? Hii ni pamoja na kuainisha miundo mbinu hiyo mapema ili baadaye kusiwe na gharama kubwa kuja kuijenga na kufidia watu. Bado tuna mawazo mafupi kama ndengu!!!! Dar es Salaam bado ni kakijiji fulani ambako kamejipa hadhi ya jiji. Hakuna chochote hapo ni uchafu na miundo mbinu isiyo na kiwango. Watu wanajenga ovyo tu, maji ni shida, barabara hata za vumbi zimetushinda, watu wengi masikini na serikali haioni shida angalau kuja na ramani mpya ya jiji ambayo utekelezaji wake hautajali nani ataongoza serikali. Wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? Kama gharama ni lami kwa nini tusianze hata kwa barabara za vumbi. Watu wapangwe vizuri nawenye kufidiwa wafidiwe ili jiji lipangwe vizuri!!! Acheni siasa na mtembee miji ya wenzetu muone.
Unayosema yatawezekana tu kama mipango yetu itafanywa na wataalamu badala ya wanasiasa. Wanasiasa wana maisha mafupi kimpango siyo zaidi ya uchaguzi ujao! Bahati mbaya sana kwa barabara zinaenda au zinaunganishwa na siasa, ndiyo maana mpaka zinaorodheshwa kwenye ilani zao za uchaguzi kana kwamba wakitengeneza hizo basi ndiyo tumefika Kilele cha maendeleo yetu! Kwa sababu hii hakuna anayeahangaika na reli maana haina makini kubwa kisiasa.
 
Back
Top Bottom