Magufuli apangua hoja zote za Wabunge

Magufuli apangua hoja zote za Wabunge

Sasa hapo ndo kapangua nini? Pamoja na hiyo unayosema kapangua, bado kuna tatizo la foleni mjni Dar es Salaam. Tufikie mahali watanzania tuache ushabiki maana siasa haitatufikisha popote. Magufuli kuna mazuri anafanya. Ila Tatizo la nchi yetu huwa hatufikirii miaka mia moja (100) ijayo. Kwa mfano ni kwa nini kusiwe na mpango kabambe angalau miaka mia ijayo kwa mji wa Dar es Salaam ambao utahusisha usafiri wa train za umeme kwa maana ya underground, trum, na mabasi kama hayo ya DART? Hii ni pamoja na kuainisha miundo mbinu hiyo mapema ili baadaye kusiwe na gharama kubwa kuja kuijenga na kufidia watu. Bado tuna mawazo mafupi kama ndengu!!!! Dar es Salaam bado ni kakijiji fulani ambako kamejipa hadhi ya jiji. Hakuna chochote hapo ni uchafu na miundo mbinu isiyo na kiwango. Watu wanajenga ovyo tu, maji ni shida, barabara hata za vumbi zimetushinda, watu wengi masikini na serikali haioni shida angalau kuja na ramani mpya ya jiji ambayo utekelezaji wake hautajali nani ataongoza serikali. Wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? Kama gharama ni lami kwa nini tusianze hata kwa barabara za vumbi. Watu wapangwe vizuri nawenye kufidiwa wafidiwe ili jiji lipangwe vizuri!!! Acheni siasa na mtembee miji ya wenzetu muone.

that's very true indeed!!! tatizo hata vijana wamekuwa kama vikongwe ni siasa tu, kila jambo ni siasa!
 
Wadau, namsikiliza kupitia TBC1. Hakika Magufuli amejibu kikamilifu hoja zote za wabunge na kila mmoja ametulia na kuridhika majibu haya. Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga itakamilika ndani ya miezi miwili ijayo baada ya Kuwait Fund kutoa bilioni 16 ambazo zitatosha kwa ajili ya kazi hiyo. Pia amesema kuwa hakuna mgogoro wa kusimamia sheria baina yake na Waziri Mkuu na ndo maana wanaenda kuimarisha mizani nchini. Pia ameeleza hatua zinazochukuliwa kupunguza msongamano Jijini Dar es Salaam na amesema kuwa jiji hilo halipo miongoni mwa majini yenye msongamano mkubwa wa Magari Duniani. Amesema Wakala wa Barabara vijijini utaanzishwa kupitia TAMISEMI. Amewatahadhalisha wabunge kuwa kuwa ujenzi wa barabara si sawa na kupika chapati au maandazi. Una stage zake ambazo ni sehemu ya ujenzi. Amesema kuwa Korea ya Kusini ambao wamejenga daraja la Mkapa ndio watakaojenga daraja la Sealander. Barabara zenye urefu wa Kilometa 86 ambazo zilikuwa za Manispaa jijini Dar es Salaam zimechukuliwa na TANROADS ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.

amezungumziaje barabara zake zinazoumuka ndani ya mwaka???
 
Magufuli muongo sana halafu anawafanya wenzake wajinga kwa msaada wa spika barabara km 13 anasema km7 kandarasi anadai tena hadharani yeye anakataa kana kwamba wenzake hawafuatilii kibwa kuliko eti miezi 2 barabara iyakwisha wakati sio kweli na mnaomtetea mje hapa baada ya miezi miwili na majibu ya hiyo barabara kuisha
 
Magufuli ni mwongo sana. Kwa mara ya kwanza sasa wabunge wamegundua uongo wake, thats why anapata wakati mgumu kuipitisha bajeti yake. Ukweli ni kwamba serikali haina hela ya kuwalipa wakandarasi na wako hoi kabisa. Serikali imefilisika na Mkosamali yuko right.

huo ndo ukweli ndo maana anakwepa kujibu swali kati ya pesa zitakazopitishwa ni zipi zinaenda kulipa madeni?na ndo maana hataki kutoa ratiba ya miradi itaisha lini maana hana uhakika wa pesa amebaki tu kusema mikataba imesainiwa
 
Wadau, namsikiliza kupitia TBC1. Hakika Magufuli amejibu kikamilifu hoja zote za wabunge na kila mmoja ametulia na kuridhika majibu haya. Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga itakamilika ndani ya miezi miwili ijayo baada ya Kuwait Fund kutoa bilioni 16 ambazo zitatosha kwa ajili ya kazi hiyo. Pia amesema kuwa hakuna mgogoro wa kusimamia sheria baina yake na Waziri Mkuu na ndo maana wanaenda kuimarisha mizani nchini. Pia ameeleza hatua zinazochukuliwa kupunguza msongamano Jijini Dar es Salaam na amesema kuwa jiji hilo halipo miongoni mwa majini yenye msongamano mkubwa wa Magari Duniani. Amesema Wakala wa Barabara vijijini utaanzishwa kupitia TAMISEMI. Amewatahadhalisha wabunge kuwa kuwa ujenzi wa barabara si sawa na kupika chapati au maandazi. Una stage zake ambazo ni sehemu ya ujenzi. Amesema kuwa Korea ya Kusini ambao wamejenga daraja la Mkapa ndio watakaojenga daraja la Sealander. Barabara zenye urefu wa Kilometa 86 ambazo zilikuwa za Manispaa jijini Dar es Salaam zimechukuliwa na TANROADS ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.

dogo inaonesha Magufuli anakukuna sana mpaka unakunika,hivi Magufuli what is so special alichokifanya cha kumsifia na kusema kapangua hoja,hebu uwe serious mdau,yaan wewe mwisho wa upeo wako ndo unaona magu amefanya makubwa sana???,seriously???hata kama hutembei soma basi ujifunze nchi za wenzatu kama Malaysia,Korea wamefanya nini??maana we were together in the same level in 1960s-1970s
 
huo ndo ukweli ndo maana anakwepa kujibu swali kati ya pesa zitakazopitishwa ni zipi zinaenda kulipa madeni?na ndo maana hataki kutoa ratiba ya miradi itaisha lini maana hana uhakika wa pesa amebaki tu kusema mikataba imesainiwa
Naona mmevurugwa nyie
 
Magufuli ni mwongo sana. Kwa mara ya kwanza sasa wabunge wamegundua uongo wake, thats why anapata wakati mgumu kuipitisha bajeti yake. Ukweli ni kwamba serikali haina hela ya kuwalipa wakandarasi na wako hoi kabisa. Serikali imefilisika na Mkosamali yuko right.
Makandarasi gani ameshindwa kuwalipa?
 
Kama hujamuelewa Magufuli inawezekana una tatizo binafsi.
Mkuu, kuna wengi humu ambao ni misukule ya UKAWA kazi yao ni kubisha tu hata kama wanauona ukweli. Nimefurahia sana Magufuli alipokuwa anampa za uso Mnyika kuwa hajasoma bajeti yake na kama ameisoma, hakuielewa
 
Bunge tayari limepitisha bajeti ya wizara ya ujenzi.Hongera sana Magufuli kwa kujibu hoja kwa ufanisi mkubwa na kwa facts hata Deo Filikunjombe amethibitisha hili mapema leo wakati akichangia hotuba ya wizara hii,tunahitaji sana mawaziri wa namna hii kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Yaani bilioni 16 za kujenga barabara zetu tunasubiri "Kuwait Fund" ila bilioni 60 za posho bungeni serikali inatoa, tena kiwango cha posho wanasema ni kidogo, kwa siku sabini!
 
Kama hujamuelewa Magufuli inawezekana una tatizo binafsi.

nimuelewe kwa lipi pesa ya watanganyika inateketea hovyo miradi ipo chini ya viwango,inasuasua,imekwama,pesa hakuna,msongamano wa magari dar umemshida yeye na serikali yake mzigo ya ccm,amekuwa dumilakuwili leo anasema anasimamia sheria mbona anapata kigugumizi kwenye malori kuzidisha uzito?au na yeye kapozwa?mbona habomoi jengo la tanesco pale ubungo ambalo lipo kwenye hifadhi ya barabara?ila ni halali kubomoa vibanda vya watanganyika bila hata kuwalipa fidia halali?
 
Magufuli ukishindana nae kwa hoja utaumia wewe
 
magufuli porojo nyingi ashukuru leo makinda alikuwepo angemkuta zungu ndo angekoma. haiwezekani barabara inatengewe hela miaka mitatu mfululizo hamna kinachoendelea alafu unaleta ushabiki
 
Wadau, namsikiliza kupitia TBC1. Hakika Magufuli amejibu kikamilifu hoja zote za wabunge na kila mmoja ametulia na kuridhika majibu haya. Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga itakamilika ndani ya miezi miwili ijayo baada ya Kuwait Fund kutoa bilioni 16 ambazo zitatosha kwa ajili ya kazi hiyo. Pia amesema kuwa hakuna mgogoro wa kusimamia sheria baina yake na Waziri Mkuu na ndo maana wanaenda kuimarisha mizani nchini. Pia ameeleza hatua zinazochukuliwa kupunguza msongamano Jijini Dar es Salaam na amesema kuwa jiji hilo halipo miongoni mwa majini yenye msongamano mkubwa wa Magari Duniani. Amesema Wakala wa Barabara vijijini utaanzishwa kupitia TAMISEMI. Amewatahadhalisha wabunge kuwa kuwa ujenzi wa barabara si sawa na kupika chapati au maandazi. Una stage zake ambazo ni sehemu ya ujenzi. Amesema kuwa Korea ya Kusini ambao wamejenga daraja la Mkapa ndio watakaojenga daraja la Sealander. Barabara zenye urefu wa Kilometa 86 ambazo zilikuwa za Manispaa jijini Dar es Salaam zimechukuliwa na TANROADS ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.

Hakika mkuu,Magufuli kiboko yao
 
Mimi ni mmoja wa wakandarasi tunaoidai TANROADS jumla ya Sh 443bn. Hatuongei tu

kampuni yetu pekee inadai 5 bilion na mhandisi mshauri ameidhinisha na hatujalipwa tangu December. cha ajabu mradi wetu umetengewa 2 bilion za kuendekea na kazi.
kipindi cha nyuma tanroads kwenye website yao walikua wanaweka tarehe za mradi kuisha na gharama.kwa sasa wametoa hizo informatuon.
 
Mkuu, kuna wengi humu ambao ni misukule ya UKAWA kazi yao ni kubisha tu hata kama wanauona ukweli. Nimefurahia sana Magufuli alipokuwa anampa za uso Mnyika kuwa hajasoma bajeti yake na kama ameisoma, hakuielewa

Mimi huwa nawafananisha na watu waliofungwa vitambaa vyeusi usoni, wanakwenda tu ilimradi bila kujua njia.
 
Back
Top Bottom