Magufuli apangua hoja zote za Wabunge

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Wadau, namsikiliza kupitia TBC1. Hakika Magufuli amejibu kikamilifu hoja zote za wabunge na kila mmoja ametulia na kuridhika majibu haya. Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga itakamilika ndani ya miezi miwili ijayo baada ya Kuwait Fund kutoa bilioni 16 ambazo zitatosha kwa ajili ya kazi hiyo.

Pia amesema kuwa hakuna mgogoro wa kusimamia sheria baina yake na Waziri Mkuu na ndo maana wanaenda kuimarisha mizani nchini. Pia ameeleza hatua zinazochukuliwa kupunguza msongamano Jijini Dar es Salaam na amesema kuwa jiji hilo halipo miongoni mwa majini yenye msongamano mkubwa wa Magari Duniani. Amesema Wakala wa Barabara vijijini utaanzishwa kupitia TAMISEMI.

Amewatahadhalisha wabunge kuwa kuwa ujenzi wa barabara si sawa na kupika chapati au maandazi. Una stage zake ambazo ni sehemu ya ujenzi. Amesema kuwa Korea ya Kusini ambao wamejenga daraja la Mkapa ndio watakaojenga daraja la Sealander.

Barabara zenye urefu wa Kilometa 86 ambazo zilikuwa za Manispaa jijini Dar es Salaam zimechukuliwa na TANROADS ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.
 

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Ametoa jibu nini kusema kuwa barabara ya kusini haijakamilika kwa sababu alipata ajili ya Helkopta ......acheni usanii
 

prs

JF-Expert Member
Feb 22, 2013
2,645
2,000
Amesema..Amesema..Mchakato..Tunampango..Amewatahadharisha...

Siku tukiacha kuridhika na maneno ya wana-Siasa badala ya Vitendo ..Tutaendelea..

Eti Amepangua Duuh..!! Ushabiki wa Mpira kwenye Maisha ya Wa-Tanzania..!?!? :(
 

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Ameulizwa na mkosamali kuwa yeye atoe ratiba za ujenzi wa hiyo miradi na anadaiwa kiasi gani , anaishia kupiga porojo tu
 

Birds in bush

Member
Sep 15, 2013
42
0
Sasa hapo ndo kapangua nini? Pamoja na hiyo unayosema kapangua, bado kuna tatizo la foleni mjni Dar es Salaam. Tufikie mahali watanzania tuache ushabiki maana siasa haitatufikisha popote. Magufuli kuna mazuri anafanya. Ila Tatizo la nchi yetu huwa hatufikirii miaka mia moja (100) ijayo. Kwa mfano ni kwa nini kusiwe na mpango kabambe angalau miaka mia ijayo kwa mji wa Dar es Salaam ambao utahusisha usafiri wa train za umeme kwa maana ya underground, trum, na mabasi kama hayo ya DART? Hii ni pamoja na kuainisha miundo mbinu hiyo mapema ili baadaye kusiwe na gharama kubwa kuja kuijenga na kufidia watu. Bado tuna mawazo mafupi kama ndengu!!!! Dar es Salaam bado ni kakijiji fulani ambako kamejipa hadhi ya jiji. Hakuna chochote hapo ni uchafu na miundo mbinu isiyo na kiwango. Watu wanajenga ovyo tu, maji ni shida, barabara hata za vumbi zimetushinda, watu wengi masikini na serikali haioni shida angalau kuja na ramani mpya ya jiji ambayo utekelezaji wake hautajali nani ataongoza serikali. Wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? Kama gharama ni lami kwa nini tusianze hata kwa barabara za vumbi. Watu wapangwe vizuri nawenye kufidiwa wafidiwe ili jiji lipangwe vizuri!!! Acheni siasa na mtembee miji ya wenzetu muone.
 

MAKAH

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,589
0
Ameulizwa na mkosamali kuwa yeye atoe ratiba za ujenzi wa hiyo miradi na anadaiwa kiasi gani , anaishia kupiga porojo tu

ni mtu wa ajabu sana huyu - anazungumzia kumpa mkosamali ILANI YA CCM - hiyo si sahihi - hayo ni matusi kwa bunge na wapinzani
 

Rajab Makoba

Member
Apr 24, 2014
21
20
Mwambie azijibu hoja za Mkosa mali kwanza kwani Madeni ni zaidi ya bill.400
Na ilani ya uchaguzi inakwisha mwakani.
Amepangua nini sasa.hebu jibu wewe umsaidie.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Mwambie azijibu hoja za Mkosa mali kwanza kwani Madeni ni zaidi ya bill.400
Na ilani ya uchaguzi inakwisha mwakani.
Amepangua nini sasa.hebu jibu wewe umsaidie.
Mkosamali ameleta porojo tu. magufuli ni zaidi ya vichwa vyote vya UKAWA
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Magufuli: kila barabara ina time framework hivyo ni vigumu kuweka ratiba ya kumaliza mikataba yote
 

Rajab Makoba

Member
Apr 24, 2014
21
20
Mnge mpa nafasi basi ya kugombea Urais
Kwetu yeye ni wakawaida tu na ndio maana anashindwa kujibu hoja za Mkosamali.
At the same time wabunge wenu wote hawana swali hata moja.ni sisi tu ndio tunao uliza.Ohooo!.. Nimejua kazi yenu na wingi wenu ni kwa ajili ya kugonga meza tu nimejua.
Alafu hotuba ya jamaa yenu imejirudia kama ya mwaka jana tu alafu nyie mnapiga meza tu ni sisi ndio tumegundua hilo.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Hoja ya Mkosamali imepigwa chini na Spika ameagiza kila mbunge aombe ratiba ya ujenzi wa barabara za kwenye maeneo yake na atapewa
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Mnge mpa nafasi basi ya kugombea Urais
Kwetu yeye ni wakawaida tu na ndio maana anashindwa kujibu hoja za Mkosamali.
At the same time wabunge wenu wote hawana swali hata moja.ni sisi tu ndio tunao uliza.Ohooo!.. Nimejua kazi yenu na wingi wenu ni kwa ajili ya kugonga meza tu nimejua.
Alafu hotuba ya jamaa yenu imejirudia kama ya mwaka jana tu alafu nyie mnapiga meza tu ni sisi ndio tumegundua hilo.
Hoja ya Mkosamali imejibiwa kikamilifu na Madam Spika kamsaidia sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom