gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
MAGUFULI: KIONGOZI WA AINA YAKE
Sipendi sana kujadili watu. na hapa najadili katabia tu nilikokaona kwa kiongozi huyu.
Magufuli ni kiongozi wa ajabu. Ameanza kuliongoza taifa kiaina. Magufuli ameishachukua form ya kuomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi NEC. Nilijua kuwa atachukua form kutoka NEC baada ya kuichukua na nishtukia naona picha za misafara ya waliomsindikiza. Sijui walijuaje? Kama angetangaza kuwa siku fulani na saa fulani atachukua form sijui watu wangekuwa kiasi gani?
Yeye ameishakamilisha kazi ya kuwapata wapiga kura wa kumdhamini. Majuzi nilishtukia yuko Bukoba mjini amekuja kutafuta wapiga kura wa kumdhamini. Watu wachache walijua na wengine nilisikia wakilalamika kuwa kwa nini haikutangazwa ili wakafurike. Naona anatumia mtindo wa CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITANGAZA. Nao (mtindo wake) una maana kubwa kwa nchi yetu, maana kelele zimetufikisha pabaya. Nakumbuka wakati wa Mkapa ilikuwa kama hivi hivi. gazeti la Uhuru siku ile amechukua form habari ilitoka kushoto chini ya ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari '------ Na Mkapa achukua form' Ilikuwa habari ya mengineyo. Niliyaona 1995. Nayaona na 2015.